Brenda Mihanjo, msomi mwenye Masters aliyejikita kwenye ufundi seremala

Hivi unakisoma unakiandika ? Kina click kichwani ?

Sasa alieamua kusoma vocational Wakati wa likizo akiwa chuo na alieamua Kumaliza chuo akaenda hiyo vocational ..Wana utofauti gani Sasa ?

Yani wewe shida yako ni kwamba kwanini karudi kusoma veta wakati ana Masters haha . Kwamfano angeamua kufundishwa na fundi seremala nyumbani ...bado ungekompleini ?
Mbona hushangai ana Masters alafu anapika chakula au anafanya usafi ....kupika na housekeeping ni vocational piaa. Ukiona mtu kaenda kusomea hizo ni ili uwe kiprofesional zaidi
 
In this world everything is about money we kalia hayo mavyeti yako wenzako wanacheki fursa za kutoboa na wanatoboa wewe baki na mivyeti yako uendelee kulipwa laki 5

Watu siku hizi wanacheki wapi kwenye mtonyo a uhakika.

Binafsi nina kashahada fulani kananipa ugali tu ila nataka niingie veta nipigie short course fulani nianza piga side hustle ikiwezekana niingie kitaa mazima maana fursa naiona

We kalia micheti yako na attitude zako
 
Umeelewa nachosimamia kwenye huu uzi?
Mkuu sipingi watu kusoma veta, napinga watu kutumia muda vibaya na kichsgua koxi kwa mihemko.
Hizo fursa ulizoziona basi watu wazichangkie mapema sio wa
Some kufuata madarasa bali waangalie soko lipoje.
Wewe unaenda veta kuongeza side hustle ni sawa , sio mtu anapiga master,anakosa muelekeo ndio anachagua veta.
Veta waende wakiwa shuleni muda wa likizo au wajifunze ujuzi wowote mtaani wakiwa bado wapo shule wasisubiri kufuliandio waende vocational.
Mi binafsi nilijifunza kusuka nyungo ila huo ujuzi sijautumia kwa kuwa sina muda ila nimejipanga ntautumis huo ujuzi na ntaongezea ubunifu wangu mwenyewe na nimeona ukijifunza kusuka nyungo unaweza tumia formula ile kusuka mikeka, vikapu, mazuria, mapambo nk
Nilipokuwa dip nilitumia muda wa likizo kusoma comp application( excel power point, words), sasa hivi najiongezea mwenyewe adv xcel na VBA ili niweze kuwa full package ms app
kwa hio sipingani na wewe kupata ujuzi wa aina yoyote ile ila tusisubiri kukosa ajira ndio tutafute ujuzi wa ufundi kwani ufundi upo mwingi tu mtaani ni muda wako tu na maamuzi tena unaweza fundishwa bila hela.
 

Mjifunze kusechi info zaidi za mtu, na sio kujiandikia tu unaishia kuonekana huna la maana.

Ana MBA, utafikiri mtu haitumii kwenye business yake.

Mjiongeze aiseee, unatia aibu na wenzako wengine humu. Acheni wivu.

 
Oya, umezingua
 
Jifunzeni kutambua vitu mapema, kwa kuwa mlichelewa kujitambua basi fanyeni hivyo kwa ndugu zenu,watoto wenu wanafunzi nk.
Mambo ya kudakia vitu ukubwani yalishapitwa na wakati hata serikali ililiona hilo ikabadili umri wa kuanza shule.
Kijana unaanza kutumia you tube baada ya kumaliza chuo ? Unajitambua wewe ! chuo kuna mpaka wifi za bure.
kila kitu unachokiona kimezungumziwa kwenye mtaala na vitabu vya shule ila hamuwagi serious mkiwa shule kusikiliza, kuuliza kwa makini na kusoma kwa makini.
Maktaba kuna mavitabu ya kila aina hamuyasomi,kuna mashirika yanasambaza majarida ya bure shuleni hamsomi, siku za nyuma nilikuwa napata majarida ya mashhidi wa Jehova ya kiswahili na kingereza bure. yamesheni habari zote za kuamsha interest kwa vijana sasa nyie mlisubiri mpaka mmalize university ndio mpate interest you tube ! mlichelewa sana kujitambua na ni uzembe wenu na ina wagharimu muda wenu.
msihalalishe uzembe wenu uwe common kwa kila mtubai jamii ya yote.
Kama ndio mmejitambua sasa hivi changamkieni fursa haraka mwende huko veta ila kuna ujuzi mwingi sio selemala tu.
Samahani mimi nilizaliwa mitaa ya uswahilini wewe labda ulizaliwa huko lupembe Vijijini hatuwezi kuwa na maono na exposure sawa. Hata mimi na mtu aliezaliwa kariakoo/masaki au mwanza mjini hatuwezi fafana, hivyo nachokiona kwenue mlikosa information na pengine mlisoma shule za kata na walimu wenu wengi walitoka vijijini hawana maono yoyote.
 
Mimi sielewi hoja nini? Huyu mama ana degree ya bussiness na masoko na anafanya businesss cha ajabu nini? Alisomea business afanye bussines.Ndivyo inatakiwa
 
Toka mwanzo angesomea uselemara, mpaka level 3, na diproma na angesomea ualimu wake wa veta.
 
Kwahiyo ukisoma BCOM inabidi ukasimamie biashara za watu, huwezi ukafungua biashara yako ukatumia hiyo BCOM kuisimamia kama alivyofanya huyu?
Ndio shida ya elimu zetu hizi sometimes zinakuwekea mipaka ya kufikiri
 
Mkuu hivi unaweza kupewa tenda kubwa ya kusambaza assets ukiwa huna kampuni ?
Acha ubishi Huyo dada ana kampuni, na anamafundi wanaofanya hizo kazi yeye ni mara chache sana kuwa site, kazi yake kubwa ni kutafuta tenda na kufanya dizaining ya kile mteja anataka, Sasa utasemaje masters yake haijamsaidia si kasomea business administration Kwani anayofanya sio bisness?? Kwenda veta ni kuongeza ufahamu juu ya idea ya biashara anataka kufanya, utasemaje amepoteza muda?? Kwamba masters haina kazi?
 
Kwa hio hata kujifilia na kufagia ndani eti ni career choice?
Kwahiyo ukisoma BCOM inabidi ukasimamie biashara za watu, huwezi ukafungua biashara yako ukatumia hiyo BCOM kuisimamia kama alivyofanya huyu?
Ndio shida ya elimu zetu hizi sometimes zinakuwekea mipaka ya kufikiri
Kuna watu nawajua hawajawahi shika nyundo ila wanauza asset, hao ndio wafanya biashara
Huyu ni fundi kama mafundi wengine na huenda hata assets zake hazina tofauti yoyote na mafundi wa lasaba.
Mtu amefeli kwenye fani yake mna paka paka rangi.
Jipangeni mnapochagua fani za kusomea vinginevyo mtaishia kutapa tapa kama panya buku.
Mmekosa miongozo ndio maana mnatapa tapa mara hiki mara kile, be focused guy!
Kubadili career inakubalika na kuna misingi na hatua za kubadili career moja kwenda nyingine, hapa TZ watu wengi hawabadili career bali wanashindwa kupata mahali pa kutumikia hizo kila na hawana ubunifu wowote katika career mama waliosomea kwa miIaka mingi na matokeo yake ndio ka huyo dada amechenji gia angani/ amejiongeza.
Watu wakubwa kama wewe huwa ni ngumu sana kuwabadili fikra hivyo simamia unacho amini ila mnapata hasara ya muda. Kuwekeza kusoma kitu miaka mingi halafu unakuja kufanya kitu tofauti ni matumuzi mabaya ya muda ndio maana wasomi wa kibongo wanachelewa sana kuzijua ramani .
Learn to start early, kama wewe ulipoteza maboya hakikisha halitokei kwa watoto wako.
 
Huyo dada ana kampuni, na anamafundi wanaofanya hizo kazi yeye ni mara chache sana kuwa site
Kichwa cha habari hakikusema hivyo hii ni nyongeza yako. Kingesema hivyo ningeunga mkono.
Habari imeandikwa
''Brenda Mihanjo aliejikita kwenye ufundi seremala " sio kama ulivyo andika wewe.
Maelezo ya mtoa mada yanasema kijana ana workshop keko na mafundi wanne hata vifaa vya kutosha hana , wewe unasema anakampuni mbona mnanichanganya, nikuamini wewe au mtoa mada ?
 
Huyo sistaree anaingiza mpunga wakutosha tu haijalishi kasoma nini na kwa level gani

Kwenye maisha tunaeza angalia unapata mahitaji yako? kwa level ipi na kwa ubora gani sasa hapo utakuta mwenye PhD, msanii, MD, welder, muuza mchele, wana same standard

Ni sawa na wale wanabishana dini hii nzuri hii mbaya hii haitakufikisha kwa Mungu, ila sisi tunaangalia je unasababisha discomfort ya namna yoyote kwa mtu mwingine au kwako? Kama jibu ni hapana basi hata kama huna dini me naona utamkuta Mungu vizuri tu

Kwahyo status yako haina chakufanya na ubora wa maisha utakayoishi, muhimu ni kumake money wazee
 
Mimi sielewi hoja nini? Huyu mama ana degree ya bussiness na masoko na anafanya businesss cha ajabu nini? Alisomea business afanye bussines.Ndivyo inatakiwa
Jamaa linaponda hapo sijui lina akili sawa sawa kweli

Mtu ana MBA n anafanya biashara jamaa linataka awe kajiliwa ndio aonekane wa maana

Hiz mentality ndio hufanya waty wengi wawe masikini vizazi na vizazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…