Brenda Mihanjo, msomi mwenye Masters aliyejikita kwenye ufundi seremala

sabuwanka

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
690
751
Brenda, msomi mwenye 'masters' aliyejikita kwenye ufundi seremala

Kote duniani vijana walio wengi wamepata elimu, lakini changamoto kubwa imekuwa ni suala la ajira, hivyo wanaamua kuutumia ujuzi wao kama muarobaini kukabiliana na changamoto hiyo.

Dar es Salaam. “Vijana wengi tukimaliza kusoma tunasubiri ajira, lakini hatuhangaiki kutafuta fursa za kazi, kazi zipo nyingi sana Tanzania, ni vijana kuchakarika kuziona hizo fursa na kuanza kuzitumia,” alisema Rais Samia Suluhu Hassan, Januari 07, 2022 katika maadhimisho ya kilele cha matembezi ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Suala la kusubiri ajira baada ya kumaliza masomo kama alivyosema Rais Samia, ni tofauti kwa Brenda Mihanjo (33). Licha ya kuwa na elimu ya Shahada ya Uzamili ya usimamizi wa masuala ya biashara (Masters), aliiweka kando na kuanza kujihusisha na ufundi seremala.

Mwananchi ilifanya mahojiano na Brenda ili kujua nini kilisababisha ajiingize kwenye kazi hiyo, iliyozoeleka kufanywa na wanaume na pia ni msomi wa elimu ya juu.

Anasema kitu kilichomshawishi kufanya shughuli hiyo ni kupenda bidhaa za mbao asilia.

Anasema kuwa mwaka juzi ndio alijiunga rasmi kwenye ufundi seremala, akijifunza nyumbani na baadaye akaenda Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya ufundi Stadi (Veta) kusomea ufundi seremala kozi fupi ya miezi mitatu.

Anabainisha kuwa alikuwa anavutiwa na jinsi mbao zinavyoweza kudizainiwa bidhaa mbalimbali, hivyo akatamani kufahamu namna vinavyotengenezwa

“Napenda sana bidhaa za mbao asilia, navutiwa na mitindo ya bidhaa mbalimbali watu wanazotengeneza kutokana na mbao na mwonekano wake,” anasema.

Anafafanua: “Kwa kweli nilipata changamoto sana ya kwenye vipimo na ndio kilichonipeleka Veta...Maana kutojua vipimo kulinipa shida ya kuagiza mbao, kuna wakati nilikuwa ninazidisha au kupunguza kwa sababu ya kutokujua vipimo kamili. Kwa kweli sitasahau hili jambo,” anasema.

Hata hivyo, Brenda anasema mwanzoni alikuwa anakutana na changamoto ya watu kutokumuamini kwa sababu ni mwanamke, lakini sasa hivi wameanza kumuamini.

“Hii kazi inachukuliwa ni ya kiume, pia watu wanaofanya useremala wanadharauliwa na kuonekana ni maskini.

“Kwa hiyo wakati naanza watu walikuwa hawaniamini kabisa, mtu anaona akinipa kazi yake nitamharibia, lakini sasa hivi namshukuru Mungu wameanza kuniamini, hivyo napata oda nyingi,” anasema.

Anasema, wapo watu ambao wanamcheka na kumdharau kwa sababu ana elimu kubwa lakini ameamua kuwa fundi seremala, lakini yeye hawajali watu hao.

“Hii ndiyo kazi yangu na ninaichukulia kama nyingine, najua ningeamua kuwa na mgahawa au duka la mavazi hakuna ambaye angeshangaa. Lakini niliamua kuchagua useremala nikiwa na nia ya kuwa na biashara kubwa Tanzania yenye kuzalisha samani na bidhaa nyingine za mbao za kuuza ndani na nje ya nchi.

“Na najua kuwa ni sekta inayolipa kama ikifanywa kwa usahihi. Kwa hiyo kwa ujuzi, elimu na maono niliyonayo kuhusu hii kazi najua naweza kufika sehemu nzuri,” anasema.

Kuhusu mafanikio anabainisha kuwa amefungua karakana yake maeneo ya Chang’ombe mkoani Dar es Salaam pamoja na kuajiri vijana zaidi ya wanne wa kumsaidia kazi.

Mbali na hayo, anasema ameweza kutengeneza samani kwa kampuni mbalimbali pamoja na wazungu.

“Mafanikio sio makubwa, lakini nimefanikiwa kuwa na karakana yangu na pia kuajiri vijana ili wanipe nguvu ya kuzalisha bidhaa nyingi zaidi.

“Lakini pia napata oda nyingi sana kwa sasa tofauti na nilivyoanza na nyingi nazipata kutoka katika mitandao ya kijamii, hususan Instagram,” anasema.

Anaeleza kuwa haikuwa kazi rahisi, lakini alisimamia kile alichokipenda na kuamua kukifanya.

Anasema kuwa alipokuwa anataka kufanya kazi hiyo watu wengi walimkatisha tamaa, lakini yeye alipambania kwa kuwa alikuwa na nia.

“Najivunia sana, kwani nilivyoanza mwanzo na sasa ni tofauti, yaani sio Brenda yule aliyekuwa na vyeti vya elimu ya juu bila cheti cha ufundi seremala.”

Brenda anawashauri wanawake wasikate tamaa na wasimamie mawazo wanayoyaamini kwa sababu hakuna kazi ya mwanamke au mwanamume, vyote vinawezekana, kikubwa ni nia tu pamoja na kujiamini.

Anaongeza kuwa malengo yake ya baadaye ni kuja kufungua kiwanda kikubwa cha kuzalisha samani mbalimbali.

“Niamini mimi hii ndoto ya kuanzisha hiki kiwanda itafanikiwa, tofauti na watu wanavyodhani, kazi ya kuchonga samani ukiwa na soko la uhakika inalipa sana.

“Na nikifanikiwa najua nitatatua tatizo la ajira kwa vijana wengi, hususan wasomi kama mimi ambao wanaamini zaidi kupitia ajira,” anasema.

Hata hivyo, anasema changamoto anayokutana nayo kwa sasa ni mashine ndogo aliyonayo ya kupasulia mbao, hivyo kumlazimu kutoa gharama kupeleka mbao kwenye mashine kubwa.

Brenda anasema kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kupanua karakana yake ili iendane na vigezo vinavyohitajika.

“Nilipumzika kwa muda wa miezi miwili ili kufanya tathmini, kuangalia wapi nilikosea, ili ninapouanza mwaka nianze na kasi na mabadiliko zaidi, na hii itanisaidia kufikia malengo yangu haraka,” anasema Brenda.

Historia yake kwa ufupi

Brenda ambaye ni mama wa mtoto mmoja amezaliwa mwaka 1988 mkoani Dar es Salaam. Alianza elimu ya msingi mwaka 1995 katika Shule ya Msingi Kurasini na baadaye alijiunga na Shule ya Sekondari Zanaki ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha nne.

Anaeleza kuwa baada ya kuhitimu kidato cha nne alifaulu na kujiunga kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Tambaza.

Anaongeza kuwa alipomaliza kidato cha sita, mwaka 2010 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akisomea shahada ya awali ya biashara na masoko, na mwaka 2012 alisoma stashahada ya uzamili katika diplomasia ya uchumi.

“Mwaka 2019 nilisoma Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara (MBA), niliyoisoma katika chuo cha Eastern and Southern Afrika Management Institute (ESAMI),” anasema.

Gazeti la mwananchi 10/01/2022
 
Akili mtu wangu

Acha matozi waendelee kuvaa kata K wakati wenye purpose ya maisha wanapiga kazi

Mba itampa good vision ya bishara yake

Wale wa kata K siku hiI wameamua kuzitumia kabisa badala ya kuchapa kazi…. Wakijitahidi saana wanajigeuza mifugo ya majimama
 
Back
Top Bottom