Elias Msuya
Senior Member
- Dec 23, 2011
- 173
- 671
DAR. Mkurugenzi wetu wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia, pamoja na Mtaalamu wa Rasilimali, Miradi na Uwekezaji Leonard Magere, wameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi na wametakiwa wametakiwa kuripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi kati, Dar es Salaam, kesho Julai 16, 2025.
Soma pia: Brenda Rupia akamatwa na Polisi
Brenda alikamatwa Julai 12, 2025 akiwa katika mpaka wa Tanzania na Kenya, eneo la Namanga akielekea nchini Kenya na baadae alitegemea kusafiri kulekea nchini Ujerumani, wakati Magere naye alikamatwa siku hiyo hiyo katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) akielekea nchini Uingereza.
Soma pia: Polisi wakiri kumshikilia Magere
Taarifa iliyotolewa na CHADEMA leo Julai 15, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Diaspora, John Kitoka imesema chama hicho kinafuatilia kwa karibu mwenendo wa jambo hilo wakitaka haki, uwazi katika mchakato mzima.
“Tunaishukuru jamii ya Watanzania, wanachama na wapenzi wa Chadema kwa mshikamano na uungwaji mkono mnaoendelea kuonyesha katika kipindi hiki kigumu.”