BRELA bado kuna harufu ya rushwa na uzembe

aliisaac1000

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
407
272
Wadau, mimi ni mjasiria mali ambae nilikuwa nataka kufungua kampuni yangu, kwa utaratibu wa BRELA unatakiwa ulete proposal ya jina la kampuni yako na system yao inafanya search ili kuhakiki jina hilo, kama hakuna mtu mwingine mwenye jina kama lako basi system italirudisha na kulipa okey. Hicho ndicho kilichofanyika kwa jina la kampuni yangu kupitishwa na system yao online.

Chakushangaza maafisa wa BRELA pamoja na system yao kulipa okey jina la kampuni yangu, wao walilikataa na kunitaka nibadili jina lingine kitu ambacho kilinishangaza na sikukiafiki.

Hata nilipotaka kulalamika kwa mkubwa wao niliwekewa vipingamizi vingi, kwakuwa nilikuwa nimeshatumia gharama kadhaa kwa kuamini jina lilikuwa limeshapita na kukubaliwa.

Ndipo nikatonywa na baadhi ya watu ambao walishakumbwa na kadhia hiyo kuwa hiyo ilikuwa ndio utamaduni wao wa kukuyumbisha na kukuwekea vikwazo ili utoe chochote.

Ningetoa chochote basi jina la kampuni yangu ningebaki nalo. Kwa kuwa na mimi nilikuwa sikutambua mbinu hiyo, ilibidi nihangaike tena kwa kupata jina jingine kitendo ambacho kimenichukua wiki 2 na usumbufu na gharama zisizo na msingi.

Naomba serikali kutumbua hili jipu linaloitwa BRELA bado wanaishi dunia ya mwaka 47!!

Sent from my IM-A860L using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom