Breaking news:wachezaji wote waliofungiwa yanga wasitishiwa adhabu azabu !

Nadhani hapa ndipo wale ambao walikuwa hawajuajua wanao vuruga soka letu watatambua.

1: Kutofaa kwa Tenga
Tenga tangu aingie madarakani, kwa ushawishi wa rais wa nchi amepata sponsorship kubwa kuliko marais wote wa TFF na FAT waliopita. Chaajabu hakuna chochote cha maana alichokifanya kwenye soka. Huku akiwa mtu aliyecheza mpira zamani, ameshindwa kuelewa nini kifanyike ili kuokoa soka letu. Kama kuna mtu anajua chochote cha maana alichofanya Tenga aniambie. Usije ukaniambia eti kaongeza masponsor kwenye soka, au kaleta kocha ...... hivyo sio visions tunazotaka kutoka kwa kiongozi wa juu

2. Uwajibikaji
Katika nchi hii kumekuwa na tatizo la uwajibikaji si tu kwa viongozi wa nchi bali hata kwa viongozi wa vitu mbali mbali ikiwemo TFF, vilabu n.k. Tenga alipoingia madarakani alianza kutumia utaratibu wa kamati kuongoza soka, kwa tunaojua, ni kuficha udhaifu wake wa kufanya maamuzi. Kamati hizi utitiri zimefanya soka letu kuwa la kishabiki sana. Kamati zenyewe ameziunda bila kuweka balance ya interest za vilabu. Mfano unakuta kamati yote ina wajumbe ambao ni wapenzi wa timu fulani. Huu ni udhaifu wa moja kwa moja wa rais wa TFF aliyeziunda. Kupeka kazi kama hii mtu anatakiwa ku-declare interest yake mapema na iwe kwenye records. Tenga hajalazimisha ili pia in udhaifu.

Kitendo hiki cha kamati huku ikijua haina mamlaka ya kufanya maamuzi fulani, ikafanya na kuathiri soka letu ni kitendo kisicho kubalika ambacho kwenye nchi yenye uwajibikaji wanatakiwa wajiuzulu mara moja. Kuna watu mpaka kesho wanatumikia adhabu iliyotolewa na kamati hii pasipo kuwa na mamlaka hayo.

Tenga kushindwa kutambua kuwa kamati hii haistahili kufanya maamuzi, hata kulaani watu mbali mbali waliokuwa wanahoji jambo hili, ni kosa ambalo anastahili awajibike mara moja.

Tenga kumpongeza refa aliyechezesha mechi ile hali akijua kuwa kuna rufaa zimekatwa ni kosa la kushawishi maamuzi ya vyombo alivyoviunda, na anapaswa kujiuzulu mara moja.

3. Ushahidi
Hapa ndipo unashangaa na kujisemea kwamba watu alioko TFF na kwenye kamati hii ni wahuni. Iweje ushindwe kutoa ushahidi wakati tayari ulishautumia kuwadhibu watu. Iweje uanze kuandaa defence ya rufani waliyokata Yanga kabla ya kupeleka ushahidi ulioutumia awali kutengeneza adhabu?

Umakini huko wapi hapa?
 
Kwa namna hii tusitegemee soka la bongo kukua!bila nidhani ni bure!
alafu mijitu mingine nikiwaambia hakuna kuwapa simba za kijinga simba kwa kuwashinda waarabu wa aljeria wananiita hater.....
kwa upuuzi kama huu hata yesu aje sasa hivi hakuna kupiga hatua kwenye soka lenu bovu na la kifitini....

....upuuzi kama huu wa yanga na tff ni upuuzi ambao hata wapuuzi kama ngururuwe hawawezi kufanya.....
 
Back
Top Bottom