breaking news:inachekesha(swali)

breaking news:inachekesha(swali)

ni kweli Keisha ni Maasai?......nijuavyo mimi wapo,ila kwa mila zao zazamani,hawakutaka watoto outcasts,nimeshashuhudia mlemavu mmoja wa kimasai(sio wa ngozi) akihadithia changamoto alizozipata akiwa mtoto kwa kutishiwa uhai wake...ila ni mmoja tu,japo ipo kwenye utani its something we should dig and know why hawapo,na kama wapo kwanini hawaonekani?
 
Jamani me sijawahi ona I wish to c ni warefu wamesokota yale manywele yao wembamba navutia picha hapa

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
hivi ndugu zangu! mmeshawahi kumuona MMASAI ZERUZERU?


Binafsi sijawahi kumuona Mmasai albino au mwenye ulemavu wa viungo.

Mimi ninahypothesis ifuatayo kuelezea kwanini Wamasai Albino au mwenye ulemavu wa viungo hawapo (kama wapo ni wachache sana na wameanza kuonekana siku za hivi karibuni).

Si kwamba Wamasai hawazai watoto albino au wenye ulemavu mwingine la hasha ila kutokana na life style yao ya ufugaji wa kuhamahama, kuwa na mtoto mlemavu ulikuwa ni "mzigo" mkubwa kwa familia. Mlemavu huyo asingeweza kuchunga mifugo na mbaya zaidi ikifika kipindi cha kuhama inabidi abebwe pamoja na mizigo kwa umbali mrefu sana wanaotembea wakati wa kuhama. Nashawishika kuamini kuwa watoto wa Kimasai waliokuwa wakizaliwa na ulemavu walikuwa wakiuwawa kwa makusudi. Japo unaweza kudhani kuwa Alibino hawakuwa "mzigo" kama wale watoto wenye ulemavu wa viungo kwa kuwa wanaweza kutembea na kuchunga kama wasio na ulemamvu, lakini kumbuka kuwa Wamasai wanaishi katika mazingira kame kabisa, yenye jua kali ambalo ni hatari kwa Albino. Huyu mtoto albino naye alikuwa si productive maana yeye asingeweza kwenda kuchunga kwenye jua kali. Hivyo huenda nao pia walikuwa wanauwawa.

Si Wamasai pekee, Makabila mengi huko zamani yalikuwa yakiuwa watoto wenye ulemavu. Baada ya kupata elimu ya kidini na kidunia wengi wameelimika na hawawaui tena watoto wenye ulemavu. Kwa bahati mbaya au nzuri Wamasai (pamoja na makabila menginge yenye asili ya ufugaji) walichelewa kupokea "the Western Civilization" hivyo kendelea na utamaduni huo wa kuuwa walemavu kwa muda mrefu zaidi ya makabila mengine. Nadhani hii ndo sababu hasa kwa nini hakuna Wamasai albino au wenye ulemavu wa viungo, kama wapo ni wachache sana na wameanza kuonekana siku za hivi karibuni ukilinganisha na makabila mengine.

Kama unakubaliana na hypothesis hii usisahau kunipa "like".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom