Breakfast uswazi!!!

uswazi kwenu papo vizuri mkuu

huku napopajua mimi, kwanza mihogo ina kachumbari na chachandu zisizo na ushirikiano.. Mwendo wa sahani ya plastic na inalika kwenye mkeka kwa wastaarabu ila kwa kawaida kwenye floor iliyojichokea haina marumaru wala chochote zaidi ya mashimo

sambusa zenyewe ni za viazi, ukichukua chapati, bagia, vitumbua au maandazi bhasi jua utafungiwa kwenye gazeti ama ukibahatika utapewa vifuko laini vilee πŸ˜‚

uswazi hupati tabu ya chai maana kikombe hadi mia mbili na ishaungwa sukari na pembeni kuna foleni ya wamama wanauza kila kitu nje ya mlango tu, bufee ya hela yako tu 😊😊😊
 
Naona uswazi kwenu umeamua kufunga choo na hayo mangano yako na soseji, siku ukinya njoo utupeleke huko uswazi tukapaone😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…