sifi leo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 5,100
- 8,729
Habari tena wadau wa JF,
Nilitaka nitoe uzi uhuu, kama mrejesho kwa ule nilioutoa asubuhi ya leo kuhusu Tanesco Mkuranga baada ya kuomba mwenye namba ya mtumishi yeyote wa Takukuru ili anipe pesa zao nikatumbue jipu pale Tanesco Mkuranga.
Ndani ya masaa mawili tu nimepokea simu kutoka kwa Mtu wa Tanesco aliyetambulisha kama Juma Msuya wa Tanesco makao makuu, ameniomba radhi kwa kuchelewa kuunganishia umeme, na ameiahidi kulishugulikia tatizo ili kwa umakini.
Kwa kweli nimefarijika sana, kuona simu ya huyu kijana zaidi nimefarijika alivyoniomba radhi, na kuniambia kuwa si watumishi wote wa Tanesco wana tabia hizo, nami nakiri kabisa kuwa hapo si wote ila pale Mkuranga kuna tatzo kubwa sana, Meneja Tanesco Mkuranga anafanya kazi kwa mazoea sana.
Zaidi, naendelea kumpongeza huyu kijana kwa utendaji wake uliotukuka, ninaahidi ushirikiano mkubwa sana ili kuhakikisha watendaji wa namna hii wanaacha kulichafua shirika la umma, na kulipotezea fedha kwani kitendo cha mteja kulipia umeme, halafu haunganishiwi umeme kinasababishia shirika kukosa mapato kwa mwezi.
Natanguliza shukurani kwa uongozi wa JF (JamiiForums), uliowezesha sauti yangu kusikika panapo husika, lakini pia nitumie fursa hii kuwaasa watumishi wengine wa umma, kuwa mnaposoma taarifa hapa JF, zifanyieni kazi kama walivyofanya hawa Tanesco kwani wamekosa nini?
Wamenipigia simu, na nilichowaambia ndicho walichokuta kwenye mtandao wao, pili wameshauri nichukue hatua za kuvihusisha vyombo vya usalama katika kuhakikisha haki inatendeka.
Mimi nitumie fursa hii, kuwashukuru Tanesco makao Mkauu hata kama sijapata huduma yao, kitendo cha kunipigia simu kimenitia hamasa kuwa kweli ni watu walio tayari kusikiliza maoni ya watu.
Meneja Tanesco mkoa wa pwani hana budi, kueleza kurugenzi ya utawala makao makuu anaupungufu wa nini mpaka haicheleweshe serikali kuingiza fedha, jiulize kam angeungansha umeme miezi miwili iliyopita je serikali ingekuwa imeingiza shilingi ngapi kupitia kununua luku?
Pia nitumie fursa hii, kumtaka Juma Msuya anilinde maana hao vijana wakijua kuwa nimewasemea wanaweza unganisha ovyo umeme na kuniletea shida badae, kama wakiweza baada ya kuunganisha umeme waniruhusu nilete private technician ili akague, ndo wauwashe.
Kila la heri Msuya kwa kazi njema nadhani vijana kama nyinyi ndio tunao wahitaji katika ujenzi wa taifa. Maana staki niamini kuwa meneja wa Mkuranga, hakuona uzi wangu, atakuwa ameuona, ila amedharau kama ambavyo amekuwa akijibu kuwa watakuja ila hajali, wala hafanyii kazi anachokisema.
Sina ugomvi na meneja huyo ila anahitajika kutumikia umma kwa kujua kuwa yeye ni mtumishi wa umma na si bosi wa umma, analipwa na kodi zetu iweje asitutumikie kwa wakati?
Asante Kijana uliyenipigia simu kutoka Tanesco makao makuu.