Bravo Ismail Aden Rage....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bravo Ismail Aden Rage.......

Discussion in 'Sports' started by Sajenti, Aug 24, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Huenda kauli hii ikawa imeweka historia katika medani ya soka Tanzania. Mwenyekiti wa timu ya Simba Ismail Aden Rage amekanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa timu hiyo ina panga kuwafungia baadhi wachezaji wake tegemeo kwa tuhuma za kuhujumu timu hiyo katika mchezo na watani wao Yanga wa ngao ya hisani.

  Rage kwa mara ya kwanza kwa kumbukumbu zangu kwa kiongozi wa timu kama Simba alisema kuwa kufungwa kwao kulikuwa ni kimchezo tu na hakuna hujuma yoyote iliyofanywa na mchezaji au wachezaji wake. Alienda mbali zaidi kwa kuwaomba radhi wachezaji wote waliokumbwa na kashfa hiyo, ndugu na familia zao kutokana na usumbufu wowote walioupata kutokana na habari hizo.

  Tumezoa Simba au Yanga moja inapofungwa na mwenzie basi vumbi hutimka klabuni kwa wachezaji kutishwa, kusimamishwa, hata viongozi wenyewe kutimuliwa madarakani. Mfano mzuri kutimuliwa kwa Amiri Maftaha kutoka Yanga kufuatia timu hiyo kufungwa na Simba magoli 4-3.


  My take:
  Huu ndio uwanamichezo. Ni aibu katika karne hii kiongozi kushindwa kuelezea kushindwa kwa timu yake katika upande wa kiufundi zaidi na badala yake kupeleka tuhuma kwa wachezaji tu. Namshauri mtani pia Nchunga kujifunza kutoka Rage!!
   
 2. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Rage ni mwanamichezo halisi anaeishi in the game of football na huko ndiko hata sisi mashabiki tunapaswa kuelekea,watu wanatunga sentesi za uongo na wanataka tuamini hivyo!! Mgosi kukosa goli la wazi hakuanza leo, kwa hiyo kila anapokosa goli kachukua mshiko? Siyo Nchunga tu aige ,hii msg iwafikie mashabiki wote wa soka ambao wanapenda kusikiliza majungu.
   
 3. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Fabulous!!!..Zile karne za watu kuchapana mikwaju kisa eti timu imefungwa na mtaniwa jadi zimepita.
   
 4. D

  Dick JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huu ni ukomavu wa kimichezo, big up Rage!
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  well, interesting to hear that Rage Mkomavu kwa issue moja tu wakati managing sports is a heck of responsibilities. Rage ameogoza FAT na kuleta madudu makubwa, na leo kufanya jambo moja zuri aonekane mkomavu? Kwnai tusisubiri? Soon tutaanza kusikia ameiba milioni 50 au 60.
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mimi alichonifurahisha ni kuwaomba msamaha
  wachezaji waliotuhumiwa kuhujumu.....
   
Loading...