Bravo Dr Mwakyembe!lakini sidhani kama utaweza!

Bravo Dr Mwakyembe!lakini sidhani kama utaweza!

tenanzo2012

New Member
Joined
Jul 31, 2013
Posts
3
Reaction score
15
Habari za wikiend wana jf wezangu hopefully mpo poa!
Kwa takribani mwezi mzima sasa hbr kubwa ktk vyombo vyetu hbr hapa tanzania ni kuhusu watanzania wanaokamatwa au wanaojihusisha na biashara haramu ya uuzaji wa madawa ya kulevya!Nikiwa kama mtanzania mzalendo wa nchi hii sifurahishwi hata kidogo na habari hz kwani kwa kiasi kikubwa zimechafua sana sifa nzuri na jina la nchi yetu,lkn kubwa zaidi ni madhara wapatayo vijana wenzetu wanatumia madawa hayo,athar zake ni nyingi sana taifa linapoteza nguvu kazi kubwa na hata familia nyingi zinapata madhara makubwa sana!Lakini jana tumeona kwa mara yakwanza kazi ya kuanza kufichua mitandao ya watu wanajishughulisha na biashara hiyo haramu imeanza safari hii ikifanywa na waziri wa Uchukuzi Dr Harison Mwakyembe,nitumie fursa hii kwa namna ya kipekee kabisa kumpongeza waziri Mwakyembe kwa juhudi na hatua alizozianzisha kuwataja hadharani watumishi wasiokuwa waaminifu wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam walioratibu na hatimaye kupitisha madawa ya kulevya yenye thamani ya pesa za kitanzania bilioni6 kwenda nchini Afrika ya kusini! Hofu yangu kubwa naheshimu sana utumishi uliotuka wa waziri Mwakyembe lkn vita aliyoianzisha ataweza kuimaliza?kwa waswahili wanasema tatizo siyo kuuzunguka mbuyu tatizo ni KUUKUMBATIA MBUYU!Ilkumbukwe kwamba tunavyombo vingi ambavyo vilipaswa kuibua uozo huu lkn badala yake vipo kimya.ipo wapi tume inayohusika na udhibiti wa madawa ya kulevya,jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa,TAKUKURU mpaka Mwakyembe aje awafanyie kazi japokuwa sikatai kwamba nisehemu ya kazi yake kama waziri mwenye dhamana ya viwanja vya ndege nchini! Kukosekana kwa ushirikiano wa vyombo hivi ndio vinanifanya kujiuliza maswali mengi kwamba vita aliyoanzisha Mwakyembe atafanikiwa au ni nguvu ya soda tu?au pia ni katika juhudi za kuuzima huu mjadala ili wananchi waone kwamba hatua zimechukuliwa kama ilivyofanyika katika kashfa zingine kama vile Richmond, Meremeta, Mabilioni ya Uswizi nk!Naomba kuwasilisha!
 
Back
Top Bottom