Bradha wamekuibia demu wako

Speaker

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2010
Posts
6,324
Reaction score
2,244

Jamaa alikuwa bize anafanya mazoezi kando ya barabara,
baada ya jogging na kuruka kichura akaamua kupiga push up.

Wakati anaendelea na push up, mlevi moja akiwa njwiii akamsogelea na
kumuangalia kwa makini kisha akamwita;

Mlevi: Bradha, bradha, subiri kidogo bradha, hapa ni sehemu hatari.

Jamaa: Nini tena wewe mlevi?

Mlevi: Okay mi mlevi lakini nilitaka kukujulisha naona unananihii peke yako,
vibaka wamekwisha kuibia demu wako, angalia mwenyewe hapo chini
 
Nzuri lakini ungeipeleka kule chit-chat ingekuwa nzuri zaidi.
 
Hii kiboko, ndo sababu wajuvi wakadai kuwa POMBE sio chai. Kazi qeeeli qeli. Bazazi!
 
hii inabidi ihamie kwenye JOKES da hii kalii
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…