BRAC kuna Wapakistani na Wahindi wanafanya kazi bila vibali, serikali ifuatilie

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
57,664
32,147
Mbaya zaidi baadhi ya wafanyakazi wasio waminifu wa uhamiaji wamekuwa wakienda kuchota mzigo kila mwezi.

Tunaomba Waziri na mkurugenzi wa uhamiaji wafuatilieni hawa wanaleta wabangaladesh, wapakistan wakisema wanakuja kuona miradi yao wanaishia kufanya kazi.

Nenden pale Engine, nendeni Sinza ofisi zao na sehemu kibao wengine wameanza kukimbia mikoani, hawalipi ada yetu ya work permit.

Nani anawalinda?
 
Uhamiaji nao kama huwa siwaelewi! Haya wamepewa lead tuone utayari wao na hivi Waziri hakuna Naibu ni yakhe Hujui kitu!
 
Kuna mzungu aliniambia TZ ni nchi ambayo ni chaka la maharamia. Mtafuta vibali hasa ngozi nyeupe anamuita afisa uhamiaji nyumbani au hotelini, afisa ndiye anamueleza sheria itakayomlinda. Kesho afisa anarudisha passport ya mhalifu mahali walipoagana.
 
Kama hatutobadilisha tabia, wengi wetu, tuheshimu kazi zetu, tuzipende tufanye kwa bidii na uaminifu, makampuni na wafanya biashara wataendelea kuagiza wafanyakazi wake toka nje na serikali itawapa vibali , kwa macho yetu tunaona jinsi madereva walioajiriwa wanavyo pakia abiria katika magari ya matajiri wao wanapotumwa kazi au akiambiwa alale nayo awapitie wafanyakazi asubuhi basi, usiku inakuwa dalaala.

Mara zingine ukiwa na bahati kuwa na rafiki anafanya kazi dukani kwa mhindi, unaona anakuita dukani kuunua kitu chochote cha rahisi na ndani ya boxi anakuwekea music system, ukitizama pia visingizio vya uchelewaji kazini na livu za kufiwa na kuumwa usiseme.

Kuna mfanyabiashara gani yupo tayari kufanya biashara kwa hasara, ndipo anaona bora aagize wafanyakazi wa nje, anawatolea vibali anawaweka katika nyumba moja, wanawahi kazini, wanafanya kazi kwa bidii, biashara inaenda vizuri, serikali inapokea kodi kutokana na faida anayopata mfanya biashara. Hakuna mfanyabiashara anaependa kuagiza mfanyakazi nje kama kuna mtanzania ataifaya kwa bidii na uaminifu.

Sisemi watanzania wote si waaminifu, lakini wengi wetu tunapenda tunapenda kuishi maisha nje ya uwezo wetu, hali inayofanya tuingie katika kufanyakazi kazi zetu kiujanja ujanja.

Kitu tunachotakiwa kufanya ni kubadilika, kuwaonyesha wafanyabiashara na wawekezaji sisi ni wachapakazi, tunapenda kazi zetu na tunazifanya kwa uaminifu, lakini kupiga kelele waondoeni hao, na wengi wana vibali, na tukilazimisha kitachotokea ni wafanyabiashara wengi kufunga shughuli zao na kuondoka nchini na matokeo yake kuyakosesha mapato nchi.

Hawa wafanyakazi inawezekana wapo laki moja nchini, watanzania tupo wangapi tusio na kazi, je wakiondoka utaisaidia kwa pacenti ngapi watanzania tusiokua na kazi.
 
Ukiingia kiwanda cha A to Z utafikiri upo Gujarat.Kuna wahindi hadi wa kupalilia mabustani huko ndani ya Fence.Uhamiaji wakiingia wanatonywa.Hakamatwi mtu.Tanzania ni zaidi ya ujuavyo!
 
Kwa upande wa Arusha kwenye makampuni yanayojishugulisha na kilimo cha maua mbogamboga na mahoteli makubwa wamejaa wakenya amabo hawajui lolote wanalipwa mishahara mikubwa hawalipi kodi na wanaishi kinyume cha sheria hapa nchini wamulikwe na watimuliwe haraka sana
 
Kuna mzungu aliniambia TZ ni nchi ambayo ni chaka la maharamia. Mtafuta vibali hasa ngozi nyeupe anamuita afisa uhamiaji nyumbani au hotelini, afisa ndiye anamueleza sheria itakayomlinda. Kesho afisa anarudisha passport ya mhalifu mahali walipoagana.
Umesema jambo.
Ulichosema ni ukweli mtupu.
Uhamiaji kuna tatizo kubwa. Wamekuwa wakiwalinda wageni sana. Kuna maafisa wa uhamiaji wanatumika sana kulinda mahamia. Pia sisi wenyewe wananchi wa kawaida tunahusika. HRs kwenye makampuni mengi ya kigeni wanatumika sana kuwaunganisha hawa watu na maafisa wa uhamiaji. Kuna kampuni ya clearing and forwarding ni ya Muitaliano na Mswahili, Hawa jamaa walileta Mhindi kutoka India na kumuajiri kama CFO, alivyofuatilia kibali cha kufanya kazi uhamiaji akanyimwa. Lakini cha ajabu huyu Mswahili (shareholder na Mzungu) kaenda Uhamiaji kaongea na maofisa pale, basi huyu Mhindi mpaka leo anapiga kazi bila vibali. Wakaguzi wa Uhamiaji wanapokuja kukagua, Mhindi hupata taarifa mapema na hivyo siku hiyo haji kazini. Kwa hiyo ukiunganisha dots utapata picha kabisa jinsi gani maafisa wa uhamiaji siyo waaminifu wala wazalendo. Mhindi hupata taarifa kutoka huko huko uhamiaji, kwa hiyo anajua kabisa siku ambayo wakaguzi wa vibali vya wageni wanaenda kwenye kampuni yao. Yaani Watanzania tunashida. hatuna uzalendo kabisa, angalia mtu aliyepewa dhamana ya kusimamia sheria ndiye anayetumika kuwalinda wavunja sheria. Tumelogwa siyo bure
 
Mbaya zaidi baadhi ya wafanyakazi wasio waminifu wa uhamiaji wamekuwa wakienda kuchota mzigo kila mwezi.

Tunaomba Waziri na mkurugenzi wa uhamiaji wafuatilieni hawa wanaleta wabangaladesh, wapakistan wakisema wanakuja kuona miradi yao wanaishia kufanya kazi.

Nenden pale Engine, nendeni Sinza ofisi zao na sehemu kibao wengine wameanza kukimbia mikoani, hawalipi ada yetu ya work permit.

Nani anawalinda?
Jennister angetangaza kufuta vibali vyote halafu kila mtu aombe upya tu
 
Kwa upande wa Arusha kwenye makampuni yanayojishugulisha na kilimo cha maua mbogamboga na mahoteli makubwa wamejaa wakenya amabo hawajui lolote wanalipwa mishahara mikubwa hawalipi kodi na wanaishi kinyume cha sheria hapa nchini wamulikwe na watimuliwe haraka sana

Unadhihirisha utaahira wako hapo kwenye red. Hivi kuna mtu anaweza kuanzisha biashara yake halafu amchukue mtu ambaye hajui chochote amwajiri na kumpa mshahara mkubwa?

Wewe ndio hasa aina ya watu msiofaa kuajiriwa. Haya uliyoandika hapa ni kielelezo kuwa kwako wewe kufikiri ni anasa. Unapoona mwekezaji anaweka fedha zake kwenye mradi fulani, basi tambua kuwa lengo lake ni kupata faida na kamwe hakuanzisha biashara yake ILI TU AKUAJIRI WEWE au Mkenya. Kwa hiyo ukiona ameajiriwa mgeni maana yake anatarajiwa kuwa na ufanisi zaidi yako.

Kinachotusumbua sisi ni Malezi, Madesa, Vyeti, na Tamaa bila kutaka kufanya kazi. Sina shaka, kwenye Wizara ya Maliasili na Utalii kumejaa watu wenye DEGREE wa kutosha kuanzia juu mpaka chini, lakini leo hii angalia takwimu za utalii wa ndani......poor. Yote hii ni kwa ajili tu HATUWEZI KUINGIA MTAANI NA DEGREE ZETU kufanya uhamasishaji. SISI NI MABWANA MKUBWA.

Kesho wakiletwa Wakenya hapa wakaanza kupita mtaa kwa mtaa kuhamasisha utalii, badala tuige kwao tunawachukulia kama adui zetu. Mtanzania akipata DEGREE inamfanya awe BWANA MKUBWA badala ya kuwa VALUABLE ASSET. Tulieni tunyolewe, acheni wivu wa kike. Kama unaona biashara ya Maua na Mboga inalipa, anzisha ya familia yenu muajiri wacheza ngoma, kwenye siku 5 za kazi 2 wanaomba ruhusa.
 
Umesema jambo.
Ulichosema ni ukweli mtupu.
Uhamiaji kuna tatizo kubwa. Wamekuwa wakiwalinda wageni sana. Kuna maafisa wa uhamiaji wanatumika sana kulinda mahamia. Pia sisi wenyewe wananchi wa kawaida tunahusika. HRs kwenye makampuni mengi ya kigeni wanatumika sana kuwaunganisha hawa watu na maafisa wa uhamiaji. Kuna kampuni ya clearing and forwarding ni ya Muitaliano na Mswahili, Hawa jamaa walileta Mhindi kutoka India na kumuajiri kama CFO, alivyofuatilia kibali cha kufanya kazi uhamiaji akanyimwa. Lakini cha ajabu huyu Mswahili (shareholder na Mzungu) kaenda Uhamiaji kaongea na maofisa pale, basi huyu Mhindi mpaka leo anapiga kazi bila vibali. Wakaguzi wa Uhamiaji wanapokuja kukagua, Mhindi hupata taarifa mapema na hivyo siku hiyo haji kazini. Kwa hiyo ukiunganisha dots utapata picha kabisa jinsi gani maafisa wa uhamiaji siyo waaminifu wala wazalendo. Mhindi hupata taarifa kutoka huko huko uhamiaji, kwa hiyo anajua kabisa siku ambayo wakaguzi wa vibali vya wageni wanaenda kwenye kampuni yao. Yaani Watanzania tunashida. hatuna uzalendo kabisa, angalia mtu aliyepewa dhamana ya kusimamia sheria ndiye anayetumika kuwalinda wavunja sheria. Tumelogwa siyo bure

Kwa UKACHERO hatujambo, na majungu pia. Tukae chini ituume, kwa nini mtu aingie gharama zooote hizo kumleta mgeni na sisi tupo? Tunabaguliwa kwa rangi? Rangi yetu ni mbaya kiasi mtu awe radhi kutoa fedha kwa kazi ambayo tungeifanya sisi?

Tuache umwinyi. Tukipewa kazi tufanye sio kujikwida mavazi ya dukani na kazi hazifanyiki.
 
Sio kama nina watetea wakenya lakini siasa za ukabaila zimewafanya wenzetu wajue kuchapa kazi. Kwenye ukabaila kila business owner anathamini faida yake. Na wewe ukitaka kibarua chako kidumu na umfurahishe bosi fanya kazi. Pia hii imeweza kuleta motivation katika sehemu za kazi.

Ujamaa na ile dhana kuwa serikali inamiliki kila kitu ilileta watu kuwa wavivu. Ujamaa unahitaji nidhamu ya hali ya juu na ni jambo ambalo hao waasisi wake wamelishindwa.
 
Kwa upande wa Arusha kwenye makampuni yanayojishugulisha na kilimo cha maua mbogamboga na mahoteli makubwa wamejaa wakenya amabo hawajui lolote wanalipwa mishahara mikubwa hawalipi kodi na wanaishi kinyume cha sheria hapa nchini wamulikwe na watimuliwe haraka sana
 
Karma hawajui lolote wanafanya nini?

Kwa upande wa Arusha kwenye makampuni yanayojishugulisha na kilimo cha maua mbogamboga na mahoteli makubwa wamejaa wakenya amabo hawajui lolote wanalipwa mishahara mikubwa hawalipi kodi na wanaishi kinyume cha sheria hapa nchini wamulikwe na watimuliwe haraka sana
 
Jennister angetangaza kufuta vibali vyote halafu kila mtu aombe upya tu
Waziri wao ametenguliwa Jestina akae mkao wa kutimua. Waziri mpya afute vibali vyote wapewe deadline ya kurenew. Iundwe team maalumu/ JWTZ ikihusishwa maana polisi wameshindwa kulisimamia hili. Centre ya kurenew iwe Dodoma hapana Dar. Ikipita deadline wafanyakazi wapewe ruksa kupeleka wahusika ngazi ya juu. Tutanyooka tuu
 
SIO VIBALI TU, UNAEMPA KIBALI LAZIMA ACHUJWE KWA KINA KAMA KUNA UMUHIMU WA YEYE KUJA MAANA VIJANA GRADUATES WENGI WAKO BENCHI HUKU DARASA LA SABA INDIA/EUROPE/MIDDLEAST/SA ANAKUJA KUWA BOSS
 
mtoa mada acha upuuzi si utoe taarifa kwenye mamlaka husika hata serekali ya mtaas wachukuliwe hatua
 
mtoa mada acha upuuzi si utoe taarifa kwenye mamlaka husika hata serekali ya mtaas wachukuliwe hatua
Sindiolmaana mpuuzi ukaja kuandika huku badala ya kumjulisha mkeo kunanini of is in kwao
 
SIO VIBALI TU, UNAEMPA KIBALI LAZIMA ACHUJWE KWA KINA KAMA KUNA UMUHIMU WA YEYE KUJA MAANA VIJANA GRADUATES WENGI WAKO BENCHI HUKU DARASA LA SABA INDIA/EUROPE/MIDDLEAST/SA ANAKUJA KUWA BOSS
kwaio mtu anaona ni bora amuajiri darasa la 7 wa India kuliko mtanzania. hii inaonesha watanzania ni zero kabisa. tukizuia wahindi kufanya kazi nchini izo biashara zitafilisiwa na watanzania ndani ya miezi miwili
 
Sio kama nina watetea wakenya lakini siasa za ukabaila zimewafanya wenzetu wajue kuchapa kazi. Kwenye ukabaila kila business owner anathamini faida yake. Na wewe ukitaka kibarua chako kidumu na umfurahishe bosi fanya kazi. Pia hii imeweza kuleta motivation katika sehemu za kazi.

Ujamaa na ile dhana kuwa serikali inamiliki kila kitu ilileta watu kuwa wavivu. Ujamaa unahitaji nidhamu ya hali ya juu na ni jambo ambalo hao waasisi wake wamelishindwa.
umeongea kitu kizuri sana. Tanzania hatuwezi kushindana na nchi nyingine kwasababu sisi bado tuna ile mentality ya ujamaa tumezoea kupewa sio kujituma hatuko competitive. katika soko la ajira hakuna mtu atakupa tu kazi kisa wewe ni mtanzania wakati kuna wakenya au wa Pakistan wako tayari kafanya hiyo kazi kwa nusu ya mshahara wako
 
Back
Top Bottom