timetoloveyourself
JF-Expert Member
- Mar 24, 2015
- 206
- 206
hajawai kunipa ata sent tano zaidi ya kuninunulia soda,ni mkorofi nimejaribu kumbadilisha nimeshindwa labda nikuletee wewe ujaribu.anasema hua anaspend na rafiki zake zaidi navyomjua ni chapombe
Ni mtihani huo!! vumilia kidgo zaid. Mambo mazuri hayapo mbali. Endelea kuhope one day mambo yatakuwa Yes
pole sana dada, ikiwa nafsi yako inakufanya umuone hutaweza kufanya nae maisha kwa kigezo au vigezo ulivosema ni bora uachane nae mapema ili usje ishi kwa maumivuuuuu, usitegemee kumbadilisha mtu mkiwa tayari ndoani,ni wanaume wachache sana hubadilika kwa uweza wa mungu mwenyezi,wengi huzidi kuwa matatizo,sasa bora uyaache mapema utulie ukimsihi mungu akupe mume wa kufanana nawe.
Mweleze hizo weakness zake mpe muda wa kujirekebisha,asipojitambua achana nae.
Kikubwa rudi kwa muumba wako tubu kwa nadhiri na vifyungo vyote ulivyowahi wekeana na huyo mpenzi ili mungu akutengenezee njia ya wewe kupata mwenzi wa kuendana nawe, usisahau hatua muhimu za kupata mume huanza katika urafiki mwema, uchumba,mapenzi ndoa takatifu.
duuuuh, ananuna?? mchunguze vizur isije ikawa hajakamilika uanaume wake huyo!!
bythe way, hapo kuna kitu ''mapenzi'' alafu kuna ''kipato'' na elimu ndani yake!!
;;;;;;tafakari chukua hatua;;;;;;;;
Hali zenu wana Jamii forum naombeni ushauri wenu,
Mimi ni msichana wa miaka 28 nina degree Bcom,boyfriend wangu ana miaka 34 ni mwalimu serikalini.tulipoanza uhusiano nilikua mpweke tukaingia kwenye mahusiano,yeye kutokana na umri kwenda anatafuta mtu wa kuoa.
Huwa anagusia kuhusu ndoa mi namwambia kwanza ajiandae kimaisha either asome afikishe level ya degree au kama ana njia mbadala ya maisha, cause kama mimi sina kazi ni ngumu kuishi kwa kutegemea mshahara wake nikajipa mahope mayb nitulie nae ipo tu siku atawini maisha kila siku namkazania asome au abadili kazi navyomuona mwenzangu hana haraka ya kukazana kimaisha.
Kinachoniboa hua ananiomba hela ya matumizi wakati mwengine hadi nauli anaomba,sim yake katupa anatumia yangu na aliniambia sometimes anapandaga daladala bila nauli,jamani mtu gani wa kuanza nae maisha huyu? Natamani nimuache ila ntaanzia wapi,kumpenda nampenda ila maisha yanamshinda hua anamuombaga hadi mama yake ela, msinitukane mnishauri.alafu ana wivu mpaka nakosa amani akipiga simu nisipopokea kanuna.
Hajawai kunipa ata sent tano zaidi ya kuninunulia soda,ni mkorofi nimejaribu kumbadilisha nimeshindwa labda nikuletee wewe ujaribu.anasema hua anaspend na rafiki zake zaidi navyomjua ni chapombe
Catalyya;
Nakuonea huruma sana. Mapenzi yako kwa huyu mtu yamekumaliza kabisa. Unakataa kukubali kuwa kuna kitu kinacho kushikiza kwake. Angalia kasoro ulizotupa hapa kuwa umeziona kwake; 1. Umemzidi kielimu na ukimshauri aongeze kisomo hataki. 2. Hajiwezi hata kukununulia zawadi yeyote kwani hakuna siku utamkuta na mia ndo maana anaomba kwako na kwa mamake. 3. Mbaya zaidi ni chapombe.
Nikuulize swali la kizushi tu; Unakiu ya kuolewa? Kama ni ili kusudi watu waseme wewe ni Mrs. wa flani, leo usiku chukua vyombo vyako hamia kwake. Asubuhi ukiamka msalimie ma mkwe umwambie umekuja nyumbani. Harusi tayari hiyo.
Ila kama unahitaji mume wa kukuinua maishani na muishi kwa mafanikio, huyu hakufai. Usijaze seva hapa jf
Naonanga kama venye wewe unatafutanga kujibebesha lifetime luggage!
Hali zenu wana Jamii forum naombeni ushauri wenu,
Mimi ni msichana wa miaka 28 nina degree Bcom,boyfriend wangu ana miaka 34 ni mwalimu serikalini.tulipoanza uhusiano nilikua mpweke tukaingia kwenye mahusiano,yeye kutokana na umri kwenda anatafuta mtu wa kuoa.
Huwa anagusia kuhusu ndoa mi namwambia kwanza ajiandae kimaisha either asome afikishe level ya degree au kama ana njia mbadala ya maisha, cause kama mimi sina kazi ni ngumu kuishi kwa kutegemea mshahara wake nikajipa mahope mayb nitulie nae ipo tu siku atawini maisha kila siku namkazania asome au abadili kazi navyomuona mwenzangu hana haraka ya kukazana kimaisha.
Kinachoniboa hua ananiomba hela ya matumizi wakati mwengine hadi nauli anaomba,sim yake katupa anatumia yangu na aliniambia sometimes anapandaga daladala bila nauli,jamani mtu gani wa kuanza nae maisha huyu? Natamani nimuache ila ntaanzia wapi,kumpenda nampenda ila maisha yanamshinda hua anamuombaga hadi mama yake ela, msinitukane mnishauri.alafu ana wivu mpaka nakosa amani akipiga simu nisipopokea kanuna.
Maelezo yako hayajajitosheleza mshahara anaopata unaenda wapi? kama wote anakupa wewe kwanini asikuombe,muda mwingine wewe unatakiwa uwe na akili yakujiongeza kwa huyo mpenzi wako jinsi gani umfanye awe bora kama wanaume wengine siku zote tabia hubadilishwa na mtu na mtu mwenyewe niwewe wakumbadili