Boyfriend ananitegemea

Boyfriend ananitegemea

Cataliyya

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
781
Reaction score
378
Hali zenu wana Jamii forum naombeni ushauri wenu,

Mimi ni msichana wa miaka 28 nina degree Bcom,boyfriend wangu ana miaka 34 ni mwalimu serikalini.tulipoanza uhusiano nilikua mpweke tukaingia kwenye mahusiano,yeye kutokana na umri kwenda anatafuta mtu wa kuoa.

Huwa anagusia kuhusu ndoa mi namwambia kwanza ajiandae kimaisha either asome afikishe level ya degree au kama ana njia mbadala ya maisha, cause kama mimi sina kazi ni ngumu kuishi kwa kutegemea mshahara wake nikajipa mahope mayb nitulie nae ipo tu siku atawini maisha kila siku namkazania asome au abadili kazi navyomuona mwenzangu hana haraka ya kukazana kimaisha.

Kinachoniboa hua ananiomba hela ya matumizi wakati mwengine hadi nauli anaomba,sim yake katupa anatumia yangu na aliniambia sometimes anapandaga daladala bila nauli,jamani mtu gani wa kuanza nae maisha huyu? Natamani nimuache ila ntaanzia wapi,kumpenda nampenda ila maisha yanamshinda hua anamuombaga hadi mama yake ela, msinitukane mnishauri.alafu ana wivu mpaka nakosa amani akipiga simu nisipopokea kanuna
.
 
Naonanga kama venye wewe unatafutanga kujibebesha lifetime luggage!
 
Kama huo upendo wako utakula utalipa ada utajenga nyumba endelea kumng'ang'nia na kumpenda
 
Acha kulia lia mbona shilole(shishi baby) hatusikii akilalamika nauku yeye ukiangalia dhana ya kutegemewa anategemewa kweli.
 
Ni mtihani huo!! vumilia kidgo zaid. Mambo mazuri hayapo mbali. Endelea kuhope one day mambo yatakuwa Yes
 
Maelezo yako hayajajitosheleza mshahara anaopata unaenda wapi? kama wote anakupa wewe kwanini asikuombe,muda mwingine wewe unatakiwa uwe na akili yakujiongeza kwa huyo mpenzi wako jinsi gani umfanye awe bora kama wanaume wengine siku zote tabia hubadilishwa na mtu na mtu mwenyewe niwewe wakumbadili
 
Wavivu wanajulikana.

Ndege wafananao huruka pamoja..

Beckham sio mpumbavu kumuoa victoria ,,,,, eva longoria na tony parker,,

wavivu kwa wavivu,, wanaojituma kwa wanaojituma,,, ndio maisha ya kisasa yanavyotaka,,
 
Anakutegemeaje wakati huna kazi? Fafanua acha kumsingizia mtoto wa mwanamke mwenzio.
 
.....mfungulie miradi awe anasimamia atokapo skuli...

Naona tatizo lako
1. ni elimu yake
2. kutokupenda kuchacharika
3. Wivu
***mpe mwaka mzima tena wa mategemeo nawe ubadili mawazo unayojijengea juu yake
 
maelezo yako hayajajitosheleza mshahara anaopata unaenda wapi? kama wote anakupa wewe kwanini asikuombe,muda mwingine wewe unatakiwa uwe na akili yakujiongeza kwa huyo mpenzi wako jinsi gani umfanye awe bora kama wanaume wengine siku zote tabia hubadilishwa na mtu na mtu mwenyewe niwewe wakumbadili

Hajawai kunipa ata sent tano zaidi ya kuninunulia soda,ni mkorofi nimejaribu kumbadilisha nimeshindwa labda nikuletee wewe ujaribu.anasema hua anaspend na rafiki zake zaidi navyomjua ni chapombe
 
.....mfungulie miradi awe anasimamia atokapo skuli...

Naona tatizo lako
1. ni elimu yake
2. kutokupenda kuchacharika
3. Wivu
***mpe mwaka mzima tena wa mategemeo nawe ubadili mawazo unayojijengea juu yake

Tatizo sio mchakarikaji wala hajui kusave mshahara wake,angekua mchakarikaji ningemvumilia wivu wake,japo ana miaka mitatu ualimu.ila nna kaka yangu ni mwalimu kajisomesha saivi anamalizia degree yake na amechukua mkopo anajenga japo amekaa miaka kumi serikalini
 
Achana naye; kama mtulinga wake mali sana utammegea siku mojamoja ukiwa kwako wakati unaperuzi kipya kinyemi
 
Wanawake mnaweza umewezeshwaNafikiri kama kweli unampenda usiangalie elimu au status yake! jaribu kupanga mipangilio mizuri ya maisha yenu ya baadae natumaini mtatoka kama kweli unampenda lakini,

Ila kama lengo lako ni kipato ie mumeo awe na kipato au elimu same level to you itatake time nawe age inadhidi songa sidhani kama utapata hata huyo mwalimu.
 
Wavivu wanajulikana.

Ndege wafananao huruka pamoja..

Beckham sio mpumbavu kumuoa victoria ,,,,, eva longoria na tony parker,,

wavivu kwa wavivu,, wanaojituma kwa wanaojituma,,, ndio maisha ya kisasa yanavyotaka,,

Kwel kabisa hujakosea ata kidogo watu hichi kitu hawatambui sijui kwa nini
 
Wanawake mnaweza umewezeshwaNafikiri kama kweli unampenda usiangalie elimu au status yake! jaribu kupanga mipangilio mizuri ya maisha yenu ya baadae natumaini mtatoka kama kweli unampenda lakini,

Ila kama lengo lako ni kipato ie mumeo awe na kipato au elimu same level to you itatake time nawe age inadhidi songa sidhani kama utapata hata huyo mwalimu.

Mwenzangu mme anitegemee sio boyfriend ambae kesho anaeza akakuacha na hisia zake za wivu.angekua wa kubadikika angekua amefanya chochote ndani ya hiyo miaka mitatu labda atakuja kupata wa kumbadilisha ila kwangu haelekei kubadilika
 
Back
Top Bottom