Botswana:Wageni waanza kufungasha virago


Jamani wakenya siku hizi wako kama wahindi vile yaani kila nchi wamejazana...hapa tz wamejazana wengi wametuchukulia kazi zetu sisi wabongo, uganda nao wapo botswana SA, hivi kenya hakuna kazi au tatizo liko kwanini hawakai nchini mwao?
 
Karibu home...wale washikaji zangu sijui inakuwaje...let me find them
 
karibuni mkaribie sana, msiogope siasa kwani tunakaribia mwisho wa serikali kuendekeza siasa
 
Njooni bhana, mje mjionee yanayojili hapa bongo, ila usitegemee eti serikali itajua umerudi na inahitaji mchango wako, walaa. Bongo ilishauzwa siku nyingi siku hizi kila mtu ana chacharika kivyake, siku ya kufa ikifika unaishia zako
 
Nyie mje tu, ila nyie ndio mjitune kuendana na mambo yetu msituletee mambo ya kutaka kuiga mambo ya Botswana. Narudia tena, rudini nyumbani lakini mjue huku sio Botswana.
 
NIMESIKIA MADAKTARI WALE WALIOGOMA NA WENGINE KUFUKUZWA KUWA WANAKUJA HUKO, WANALIPA VIZURI SANA NA MAISHA NI SIMPLE, WASUBIRINI BANA MUWAONESHE MITAA KIDOGO. UKIONA KWAKO KWAFUKA MOSHI, UJUE KWA MWENZIO KWAUNGUA! wellcome back, nauza viwanja huku chaline,bagamoyo,morogoro! mkifika mtujuze
 

Jithamini usisubiri kuthaminiwa.
 
Jamani wakenya siku hizi wako kama wahindi vile yaani kila nchi wamejazana...hapa tz wamejazana wengi wametuchukulia kazi zetu sisi wabongo, uganda nao wapo botswana SA, hivi kenya hakuna kazi au tatizo liko kwanini hawakai nchini mwao?

hawa jamaa kwanza kupata shughuli kwenye ofisi zao ni ishu mfano KCB! alafu ni wanaubinafsi mno, kule kwao wageni wakifanya uwekezaji wao hawaendi kuwasupport wala nini, kama wabongo wengi wamefunga sana supermarkets zao na hata kuna bank moja ya hapa tz ilifungua tawi kule, ikabidi walifunge wenyewe. lakini sisi huku wamewekeza mabank, supermarkets na hotels na tunawasupport vya kutosha, ila wao warasimu mno. nchi yao karibia inakuwa maskani ya kina bokoharam,janjawid,alshabab,nk.
 

Karibuni,ila msimalize hela ya kuhonga kidogo wakati mna set mambo yenu huku Bongo

 

kuna maelfu ya watswana wamegraduate nje mwaka jana na mwaka huu, wanazurula tu mitaani euro na asia na hata govt yao hawajui watawaajiri vipi wote. Hayo mawazo ya "watatukumbuka" epukana nayo. Govt yao iliwekeza kwenye elimu na hayo ndiyo matunda sasa..
NB: Hawa madogo wamesoma ktk vyuo bora duniani sasa wewe ukienda kujitutumua na vyeti vyako vya tz usije kusingizia wanakubagua. Nina uhakika na niliyoyaandika
 

Mkuu,

Heshima yako.

Miaka 12 ulioisi Botswana si haba na kama ulijijenga kimaisha basi hutaweza kusumbuliwa na vijisenti vya kuhangaika kutafuta cha kufanya ukiwa Tanzania.

Rudi tu na uanzishe mpango wowote ule iwe biashara au mradi kwani utakuwa na mtaji wa kutosha.

Mtaji siku hizi sio pesa tu bali pia "intellectual property" ambapo inaweza kukuingiza benki na ukaongezea mtaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…