BoT yaja na mfumo bora wa uwekezaji taasisi, mashirika

BoT yaja na mfumo bora wa uwekezaji taasisi, mashirika

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
1583427379899.png


BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imesema imeandaa mfumo bora wa kuziwezesha taasisi binafsi na mashirika ya umma kuwekeza kwa faida badala ya kupata hasara katika shughuli za biashara na uwekezaji kwenye jamii.

Akizungumza wakati wa semina ya waandishi wa habari za uchumi na biashara, Meneja wa Idara ya Masoko na Fedha wa BoT, Tawi la Arusha, Lameck Kakulu, alisema kuwekeza kuna faida kubwa kwa kuwa mwekezaji ana fursa ya kujipatia faida kuliko hasara. Alisema kiwango cha riba kwenye dhamana za muda mfupi kilishuka kutoka asilimia 8.5 Agosti hadi asilimia 5.5 Desemba mwaka 2019.

Hata hivyo, alisema matokeo ya utekelezaji wa sera bora za fedha iliongeza ujuzi wa fedha kwenye benki kutoka wastani wa asilimia saba hadi nane hadi asilimia 20. Pia alisema ushiriki wa wawekezaji binafsi dhamana ilipanda kutoka asilimia mbili hadi kufikia asilimia sita. kuongezeka kwa uelewa kwa wawekezaji wa mashirika na taasisi binafsi.

Kakulu alisema kiwango halisi cha dhamana za muda mfupi na muda mrefu kilichopatikana ni Sh. bilioni 2,572.52 sawa na asilimia 103, wakati kiwango kilichokusudiwa kiliongezeka kwa asilimia 42, ukilinganisha na mwaka wa 2018/19. Kiwango kilichopatikana ni Sh. bilioni 1,192.69 na kiasi cha Sh. bilioni 1,379.38 zimetokana na dhamana za muda mfupi na mrefu.
 
Bank of Tanzania
A mother of other banks
...... of resort!!!!
 
Back
Top Bottom