BOT kusajili watoa huduma za fedha nchi nzima, wakiwemo mawakala wa fedha za simu na bima

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetengeneza Daftari la Kudumu litakalosajili watoa huduma za fedha nchi nzima, wakiwemo mawakala wa fedha za simu na bima kuanzia Julai mwaka huu.

Hatua hiyo, itawezesha nchi kuondokana na tatizo la watoa huduma vishoka. Utekelezaji wa usajili wa watoa huduma hao unafanywa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza inaanza Machi hadi Aprili mwaka huu.

Awamu ya pili itaanza Mei hadi Juni mwaka huu. Hivyo, kuanzia Julai mwaka huu watoa huduma za fedha watakaofanya kazi, ni wale tu waliosajiliwa na kupewa namba ya utambulisho, yaani QR Code.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam juzi na Mkurugenzi wa Mfumo wa Malipo ya Taifa(FRS) wa BoT, Bernard Dadi. Alisema hayo wakati akizungumzia mfumo huo kwenye mafunzo ya waandishi wa habari.

Alisema daftari hilo, litakuwa suluhisho kwa watoa huduma wa fedha wasio halali. Aliwataja wanaopaswa kusajiliwa kuwa: Ni matawi ya benki, mawakala wa benki, mawakala wa pesa kwa njia ya simu za mkononi, wakala au dalali wa bima, wakusanyaji wa malipo kwa njia ya kadi (POS), wakala wa hisa za masoko ya mitaji na dhamana na maduka ya kubadilisha fedha.

Pia huduma za bima katika taasisi za kiafya kama vile hospitali, vituo vya afya na maduka ya dawa, mashine za kutolea pesa (ATM), taasisi ndogo za kifedha (MFI) na vyama vya akiba na kukopa (Saccos).

Akizungumzia jinsi BoT itakavyoongoza utekelezaji huo, Dadi alisema BoT ni msimamizi wa taasisi zote za fedha na kibenki nchini, hivyo watoa huduma tajwa watasajiliwa kupitia mamlaka zao ambazo ni: Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC).

“Watoa huduma za fedha watasajiliwa na wasajili walioidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania, watoa huduma wote wa fedha nchi nzima wanatakiwa kuwaandaa wafanyakazi wao na mawakala washirikiane na wasajili katika kipindi cha usajili, Baada ya utekelezaji wake, mtoa huduma atapewa namba ya utambulisho ya kipekee iliyo katika mfumo wa QR code, sasa hapa wale wasio halali au wanaofanya kazi kwa kuwaibia wateja watakoma, maana tutakutambua kwa namba yako,”alisema.

Alisema baada ya usajili huo kufanywa, daftari hilo litaonesha maeneo ambayo huduma za kifedha, hupatikana nchi nzima na kuonesha eneo ambalo mtoa huduma yupo kijiografia.

Aidha, litarahisisha na kuzuia tabia ya wizi, kwani wakala atakuwa katika eneo linalotambulika. Iwapo atahamia sehemu nyingine, itamlazimu kutoa taarifa ili afanyiwe marekebisho kwenye taarifa zake.

Akizungumzia faida nyingine za kutumia mfumo huo, Dadi alisema utaratibu huo utawezesha njia nzuri ya kuwaongoza na kuwafuatilia watoa huduma wote wa fedha nchini. Hatua hiyo itaziba mianya ya wizi au utapeli, lakini pia kutoa picha kamili ya maeneo yanayohitaji kuboreshwa kwa huduma hizo nchini.

Awali Dadi alisema hatua hiyo imekuja baada ya utafiti kufanywa mwaka 2017 na kugundua kuna ombwe kubwa katika huduma hizo nchini.

Utafiti huo ulibaini kuwa unahitajika mfumo madhubuti wa kuwasajili watoa huduma wote ili watambulike, na kuondoa vichaka vya matapeli na watoa huduma wasio waaminifu. Utafiti huo ulibaini kuwa unahitajika mfumo utakaohifadhi data kwa watoa huduma hao ili kuleta suluhisho kwenye sekta hiyo
 
Magufuli anatamani yeye tu na kundi lake kina Makonda ndio wawe na pesa.

Anatamani kujua kila mtu ana kiasi gani, anapataje pesa na kutoka kwa nani !

Ni mwaka jana tu wamevamia bureau de change kwa kisingizio kuwa wanatakatisha pesa.

Kama hilo halitoshi wamebana mpaka SACCOS, MFIs, VICOBA na Sole Lenders.

Na sasa wamegeukia watu wa bima, mawakala wa simu na bank !

Tunakoelekea ni Magufuli tu na kundi lake ndio watakaokuwa wanamiliki pesa ya Tanzania na wewe kuipata mpaka uwapigie magoti.

Let's wait and see
 
Kweli aisee,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kuendelea Kama Kila kitu utakichukulia kwa mlengo wa kushoto! Penda kujifunza usichofahamu!/

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani watapandisha kodi?
Kutambua kila biashara ni ulinzi kwa walaji/wateja.
Hii inafaida kibwa sana japo kwa wakwepa kodi ni maumivi makali sana
Magufuli anatamani yeye tu na kundi lake kina Makonda ndio wawe na pesa.

Anatamani kujua kila mtu ana kiasi gani, anapataje pesa na kutoka kwa nani !

Ni mwaka jana tu wamevamia bureau de change kwa kisingizio kuwa wanatakatisha pesa.

Kama hilo halitoshi wamebana mpaka SACCOS, MFIs, VICOBA na Sole Lenders.

Na sasa wamegeukia watu wa bima, mawakala wa simu na bank !

Tunakoelekea ni Magufuli tu na kundi lake ndio watakaokuwa wanamiliki pesa ya Tanzania na wewe kuipata mpaka uwapigie magoti.

Let's wait and see

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi hii tunahitaji elimu hata wale waliopitia vyuoni bado hawajaelimika.
Kurasimisha/kutambua biashara au shughuli za kiuchumi ni jukumu mojawapo la serikali.
Kulipa kodi stahiki pia ni wajibu wa mwananchi, sielewi kwanini huyu ndugu amepaniki kiasi hiki
Mkaruka, Pumba

God save us
Mkaruka,
Wamezuiwa kwani?
Huwezi kuendelea Kama Kila kitu utakichukulia kwa mlengo wa kushoto! Penda kujifunza usichofahamu!/

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi hii tunahitaji elimu hata wale waliopitia vyuoni bado hawajaelimika.
Kurasimisha/kutambua biashara au shughuli za kiuchumi ni jukumu mojawapo la serikali.
Kulipa kodi stahiki pia ni wajibu wa mwananchi, sielewi kwanini huyu ndugu amepaniki kiasi hiki

Sent using Jamii Forums mobile app
Umesema kweli ndugu. Huyu ni mihemko tu kwahiyo hata usimshangae.
Pia nafikiri hawana exposure ya mambo ndio maana .

God save us
 
Pamoja na hayo waingilie kati mabank yanatoa mikopo kwa riba kubwa wapunguze mpaka asilimia 7 ,mikopo ni mzigo kwa sasa riba inaumiza tunachelewa sana kama BOT imewapunguzia bima watu wa mabank kwa nini wao hawazishushi riba zao.
Mabenki mara nyingi huchukua mikopo kutoka BoT. Na hao BoT huyakopesha hayo mabenki ya biashara kwa riba ya asilimia 9. Rejea HABARI NJEMA: Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yashusha riba kwa Benki kutoka 12% hadi 9%

Sasa wewe unataka wao wakopeshe walaji kwa riba nafuu zaidi ili wapate hasara ?

Mbona huwashauri Bot Wapunguze zaidi riba zao ?
 
Magufuli anatamani yeye tu na kundi lake kina Makonda ndio wawe na pesa.

Anatamani kujua kila mtu ana kiasi gani, anapataje pesa na kutoka kwa nani !

Ni mwaka jana tu wamevamia bureau de change kwa kisingizio kuwa wanatakatisha pesa.

Kama hilo halitoshi wamebana mpaka SACCOS, MFIs, VICOBA na Sole Lenders.

Na sasa wamegeukia watu wa bima, mawakala wa simu na bank !

Tunakoelekea ni Magufuli tu na kundi lake ndio watakaokuwa wanamiliki pesa ya Tanzania na wewe kuipata mpaka uwapigie magoti.

Let's wait and see

Mbona regulations za huduma za kifedha ziko dunia nzima? Nia ni kuhakikisha maslahi ya wote yanalindwa
 
Mbona regulations za huduma za kifedha ziko dunia nzima? Nia ni kuhakikisha maslahi ya wote yanalindwa
M PESA, Tigo Pesa, Airtel Money na mawakala wengine wa Bima whatever you name sio separate brands. Wale ni fleelacer tu wa makampuni yaliyopo kishareia. Sasa huu usumbufu wanaoupata ninwa nini ?
 
Back
Top Bottom