Boston celtics bingwa NBA 2023/2024.

Mnyunguli

JF-Expert Member
Dec 21, 2020
1,772
4,463
Na mchambuzi wa mchongo Mnyunguli

Yes nawaona mbali Celtics msimu huu wakienda kubeba hii ndoo baada ya kitambo kirefu cha miaka 16,mara ya mwisho kutwaa ubingwa huu ilikuwa 2008 dhidi ya Los Angeles Lakers wababe wa jimbo la Calfonia kwa series ya 4-2.

Celtics na Lakers ndiyo mabingwa wa kihistoria wa michuano hii mikubwa kabisa duniani ya mpira wa kikapu kila mmoja akiwa ametwaa ubingwa huu mara 17 huku Boston akipoteza fainal 5 kati ya 22 alizocheza na Lakers ya Lê bron James akipoteza fainali 15 kati ya fainali 32 alizocheza.

Msimu wa 2022 Boston alipoteza fainali dhidi ya Golden state warriors(GSW) kwa series 4-2 na msimu wa 2021 alipoteza fainali ya Ukanda wa mashariki kwa series 4-3 dhidi ya Miami heat.

Msimu huu naona vijana wao wakina Tatum na mkali brown wameimarika na hawataki utani kabisa kwani mpaka sasa msimu huu wanaongoza kwa series 2-0 dhidi ya Pacers katika mchezo wa fainali ya kanda.Ukanda wa mashariki yoyote atakayeingia fainali kati ya Dallas Mavericks na Minnesota sioni mpinzani wa kumzuia Bostoni kunyanyua kwapa ingawaje nao sio wanyonge sana hasa Minnesota aliyeshangaza Dunia kwa kumtoa bingwa mtetezi Denver Naggets kwa series 4-3.

Karibuni wadau wa Basketball binafsi nasimama na Boston celtics kwa msimu huu.Na sioni mpinzani wa kufika game 7 na hawa wababe team itakayojitahid sana itaishia game 6

Note:kwa wasioelewa maana ya series ni kwamba mechi za mtoano kwa ligi ya kikapu marekani(NBA) huwa wanacheza mechi 7 hivyo tunaziita series kwa atakayekuwa ameshinda machi nyingi kati ya saba basi huyo ndiye bingwa.

images (23).jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom