Bosi wa bodi ya kahawa anaendesha shirika la umma kama shirika lake binafsi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bosi wa bodi ya kahawa anaendesha shirika la umma kama shirika lake binafsi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JICHOBODI, Feb 27, 2011.

 1. J

  JICHOBODI New Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania Mheshimiwa Adolfu Kumburu anaendesha Shirika la Umma kama shirika lake binafsi ili kutekeleza ajenda zinazomnufaisha yeye binafsi.

  Mheshimiwa Kumburu baada ya kuajiriwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa alifumua muundo wa Bodi na kuunda muundo mpya. Muundo wake huo mpya hata kabla haujaidhinishwa na Serikali akaanza kuutumia kuengua wafanyakazi aliodhania watakuwa kikwazo katika kutekeleza maslahi yake binafsi kwa kuwahamisha na au kufuta vyeo vyao.
  Pale alipoona hawezi kutumia mabadiliko ya muundo akawafukuza kwa kuwabambikiza makosa.

  Baada ya hapo akaanza kuajiri wafanyakazi wapya anaofikiri atawatumia kutekeleza maslahi yake. Ajira zake hizo mpya hazijali mahitaji halisi ya Bodi kwani mahitaji halisi yanaweza kujulikana pale tu serikali itakapokuwa imeidhinisha muundo mpya wa Bodi ya Kahawa.

  Mkurugezi Mkuu huyu ameingia ubia na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) ambazo anazunguka nazo Ulaya na Balozi za Ulaya Magharibi(EU) kuomba pesa kusaidia maendeleo ya kahawa ambapo pesa zinazotolewa kwa NGOs hizo zinawanufaisha wao binafsi.

  Mheshimiwa Adolfu Kumburu ameingiza Bodi ya kahawa katika malumbano na viongozi wa Mkoa ya Kigoma na Wilaya ya Tarime kwa kuandika waraka zinazolinda maslahi ya makampuni yanayogharamia safari zake za Marekani.
  Matokeo yake wakulima wamefikia hatua ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari (TBC-1) kumlalamikia.

  Bila ya kujali makubaliano yaliyofanywa baina ya serikali na wawekezaji kuwaruhusu waanzishe vinu vya kukoboa kahawa ilikuboresha kahawa ya Tanzania amefuta leseni ya kununua kahawa mbivu (Cherry buying license ) ili kulinda maslahi ya Kilicafe ambayo alishiriki kuiunda wakati akiwa Technoserve isipate ushindani. Hii ni kuwahujumu wakulima kwani ushindani ngazi ya mkulima unaongeza kipato cha mkulima na ndiyo sera ya serikali. (Kuna wasiwasi kama hapokei mishahara miwili kwa kuendelea kulipwa pia na Technoserve)

  Ameshindwa kumwajili afisa utumishi ili aendeshe shirika kama mali yake binafsi kwa kuhita wajumbe wa menejimenti wa kila kikao kwa kutegemea ajenda. Anaalika wajumbe wale tu anaoona hawatahoji ajenda zake za siri.

  Wakati mwingine maamuzi ya vikao vya wakuu wa Idara anayageuza kuwa maamuzi ya menejimenti.

  Ameunda kamati ya nidhamu ambapo yeye akiwa ndie mtuhumu kwenye kikao cha nidhamu anageuka kuwa Mwenyekiti. Wakati akiwa Mwenyekiti anachofanya ni kuhakikisha anahalalisha tuhuma zake. Baadae anageuka kuwa ndiye mtoa adhabu. Kwenye vikao hivi hashirikishi hata chama cha wafanyakazi.

  Matokeo ya yote haya Mheshimiwa Aldolfu anaendesha shirika la umma bila ya kujali sheria, kanuni na taratibu za kuendesha mashirika ya umma. Wafanyakazi amewafanya kuwa mali yake binafsi ambapo haki za msingi anazitoa kama zawadi.

  Kwa muda mfupi aliokaa Bodi ya Kahawa, amejilimbikizia mali inayotokana na mahusiano na hizo NGOs pamoja na posho anazojilipa kwa kukaa muda mwingi akiwa safari. Hata hizo siku chache anazokuwa ofisini anazitumia kwa vikao ambavyo navyo anajilipa posho.

  Wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa wamemuandikia barua ya wazi Waziri wa Kilimo kumuomba aingilie kati kulinda maslahi ya Taifa ili shirika la umma lisigeuzwe mali ya mtu binafsi.
   
 2. H

  HakiMoja Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh waziri wa Kilimo mbona hushughulikii swala hili la bodi ya Kahawa? Au nako kuna kuchakachua? Mkurugenzi Mkuu bado anatunyanyasa na kutuhamisha bila kuzingatia haki ya watumishi. Tunakosa pakuegemea jamani. Nae awajibishwe.
   
 3. m

  matengo Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika kutapatapa tunasikia aliwaleta waganga wa kwao ofisini kujizindika asingolewe. Pia anatumia pesa za umma kuwahonga wakubwa ili wapeleke taarifa zisizo sahihi kwa Waziri. Je TAKUKURU mko wapi.
   
Loading...