Boris Yeltsin: Rais ‘chapombe’ aliyetoroka ikulu usiku kusaka msosi

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,353
2,137
Hebu vuta picha, ni saa nane za usiku unakimbizana na muda kuwahi kurudi nyumbani baada ya kuchelewa kwenye mihangaiko yako, ukiwa unakatiza mitaa ya karibu na ikulu, unakutana na kitu kinachokufanya usiyaamini macho yako.

Unakutana uso kwa uso na mheshimiwa rais, akiwa anayumbayumba kutokana na kuzidiwa na pombe, tena akiwa amevaa bukta ya kulalia tu, yuko bize kusimamisha teksi eti zimpeleke kwenye mgahawa ambao uko wazi akanunue msosi kwa sababu anasikia njaa kali. Utahisi upo ndotoni si ndiyo?

Basi kwa taarifa yako tukio kama hilo limewahi kumkumba aliyekuwa Rais wa Urusi, Boris Yeltsin. Wakati wa utawala wa Rais Bill Clinton, mwaka 1995 alimualika Yeltsin, akiwa rais wa urusi wakati huo kwenda kumtembelea kwenye ikulu ya White House jijini Washington.

Sifa kubwa ya Yeltsin, kabla hajawa rais, alipokuwa rais na mpaka alipostaafu, ilikuwa ni kupiga mitungi mpaka anakuwa chakari. Basi baada ya shughuli zote za kiofisi kukamilika ikulu, jamaa alianza kujimiminia Vodka kwa uchu mpaka akawa tilalila. Kibaya alikuwa anakunywa bila kugonga msosi.

Akapitiwa na usingizi lakini mishale ya saa nane za usiku, alizinduka, pombe zikiwa bado kichwani na kukumbuka kwamba hakula usiku huo zaidi ya kupiga maji. Kutokana na njaa iliyokuwa inamsumbua, mheshimiwa akaona isiwe tabu, akatoka akiwa amevaa bukta na kuwazidi ujanja walinzi wa ikulu, akaingia mitaani na kuanza kupiga kelele kusimamisha teksi impeleke kununua pizza.

Walinzi wa ikulu kuja kushtukia, mheshimiwa huyo tayari alishafika Pennsylvania Avenue huku akiendelea kufanya mambo ya kilevi,wakagundua kuwa kumbe mtu huyo alikuwa rais wa urusi, wakawa wanajiuliza imekuwaje awapite bila kumtambua?

Harakaharaka wakaenda kumchukua na kumrudisha ndani huku mlinzi mmoja akitumwa kwenda kumnunulia pizza kwani mwenyewe bado alikuwa akilalamikia njaa.

Kutokana na itifaki za ikulu ya Wite House, tukio hilo lilifanywa kuwa siri kubwa kuanzia siku linatokea mpaka miaka kumi baadaye, Rais Clinton ndiye aliyeamua kulisimulia alipoamua kuandika kitabu cha kumbukumbu za maisha yake.

Kwa mara ya kwanza tangu kutokea kwa tukio hilo, Clinton alimsimulia mwandishi Taylor Branch aliyeandika kitabu cha historia ya Clinton kilichopewa jina la The Clinton Tapes: Wrestling History with the President.

Baadaye kitabu hicho kilichapishwa kikiwa na maelezo ya tukio hilo ambapo Clinton alieleza jinsi alivyopewa taarifa na walinzi wake kwamba mgeni wake, Rais Yeltsin alikutwa barabarani akiwa na bukta tu, akisimamisha teksi ili akanunue pizza.

Kuchapishwa kwa kitabu hicho kikiwa na siri hiyo ya rais wa Urusi, kuliufanya uhusiano wa nchi hizo mbili ambao tayari ulishaanza kuwa na ufa mkubwa, kuzidi kuwa tete, Warusi wakawa wanaona Rais wao amedhalilishwa.

Rais Yeltsin alifariki miaka miwili iliyopita baada ya kuugua. Kibongobongo ungemfananisha Yeltsin na nani? (Just joking)...

Imeandaliwa na Hash- Power kwa msaada wa mitandao.
Boris yeltsin.png
Drunk.jpg
 
Nampenda sana Boris moja kati ya viongozi wahache "Machepele" kuna video nakumbuka aliitwa kwenda kuhutubia kwenye meza kuu kukawa na mawaziri wanawake, jamaa akam"Poke" bibie akaruka akapiga kelele..lol

Lakini romours has it kwamba alikua na some sort of mental/ psychological trauma!

Nachekaga sana video zake akibembea..hahah
 
Huyu alikuwa robotoid. Huyu alipanda vyeo kwa njia za udanganyifu,kwa kuficha kwamba yeye alitoka katika familia tajiri,jambo ambalo ni kosa kule Urusi. Nashukuru kamba umesema hiyo hadithi ni ya uongo. Mimi nimeamini nilipoambiwa wapo watu wanaweza kufanya levitation. Niliamini nilipiambiwa mtu anaweza kutoweka hapa,akatokea mahali pengine. Lakini kuambiwa mgenu anaweza kuipita Secret Service akaenda nje,hiyo sikuwa tayari kuamini. Labda Clinton alikuwa anataka kuongea juu ya Yesu. Hii item ilitokea katika gazeti kule Marekani. Kwamba mtu mmoja alifika White House akasema,Mimi Yesu,nataka kuongea na rais. Akaulizwa,How did you pass Security?. Clinton alipopata habari,akasema mlete huyo mtuOval Office. Clinton akaongea na Yesu,Clinton pamoja na mtu mmoja mwingine. Inasemekana Clinton ndie zaidi alikuwa anaongea,Yesu alikuwa anasikiliza tu.
 
Clintoni aliongea na Yesu?
Andrew ushapiga vyombo vyako nini?
 
hii nayo imetulia wajina
 
Punguza kidogo kufanya hizo mnazoita meditation na mitandao huku unapoelekea unaweza onekana chizi.
 
ed25c833e9b46e6179514814355d7992.jpg

Hebu vuta picha, ni saa nane za usiku unakimbizana na muda kuwahi kurudi nyumbani baada ya kuchelewa kwenye mihangaiko yako, ukiwa unakatiza mitaa ya karibu na ikulu, unakutana na kitu kinachokufanya usiyaamini macho yako.

Unakutana uso kwa uso na mheshimiwa rais, akiwa anayumbayumba kutokana na kuzidiwa na pombe, tena akiwa amevaa bukta ya kulalia tu, yuko bize kusimamisha teksi eti zimpeleke kwenye mgahawa ambao uko wazi akanunue msosi kwa sababu anasikia njaa kali. Utahisi upo ndotoni si ndiyo?

Basi kwa taarifa yako tukio kama hilo limewahi kumkumba aliyekuwa Rais wa Urusi, Boris Yeltsin. Wakati wa utawala wa Rais Bill Clinton wa Marekani, mwaka 1995 alimualika Yeltsin, akiwa rais wa Urusi wakati huo kwenda kumtembelea kwenye Ikulu ya White House jijini Washington.

df3b4806e34a8f5cb54f2585cdcba0de.jpg

Sifa kubwa ya Yeltsin, kabla hajawa rais, alipokuwa rais na mpaka alipostaafu, ilikuwa ni kupiga mitungi mpaka anakuwa chakari. Basi baada ya shughuli zote za kiofisi kukamilika ikulu, jamaa alianza kujimiminia Vodka kwa uchu mpaka akawa tilalila. Kibaya alikuwa anakunywa bila kugonga msosi.

Akapitiwa na usingizi lakini mishale ya saa nane za usiku, alizinduka, pombe zikiwa bado kichwani na kukumbuka kwamba hakula usiku huo zaidi ya kupiga maji. Kutokana na njaa iliyokuwa inamsumbua, akaona isiwe tabu, akatoka akiwa amevaa bukta na kuwazidi ujanja walinzi wa ikulu, akaingia mitaani na kuanza kupiga kelele kusimamisha teksi impeleke kununua pizza.

Walinzi wa ikulu kuja kushtukia, rais tayari alishafika Mtaa wa Pennsylvania huku akiendelea kufanya mambo ya kilevi, wakagundua kuwa kumbe mtu huyo alikuwa rais wa Urusi, wakawa wanajiuliza imekuwaje awapite bila kumtambua?

Harakaharaka wakaenda kumchukua na kumrudisha ndani huku mlinzi mmoja akitumwa kwenda kumnunulia pizza kwani mwenyewe bado alikuwa akilalamikia njaa.

c8ab481e4c1e1d880f25acd80ff1dd8d.jpg

Kutokana na itifaki za White House, tukio hilo lilifanywa kuwa siri kubwa kuanzia siku linatokea mpaka miaka kumi baadaye, Rais Bill Clinton ndiye aliyeamua kulisimulia alipoamua kuandika kitabu cha kumbukumbu za maisha yake.

Kwa mara ya kwanza, Clinton alimsimulia mwandishi Taylor Branch aliyeandika kitabu cha historia ya Clinton kilichopewa jina la The Clinton Tapes: Wrestling History with the President. Rais Yeltsin alifariki miaka miwili iliyopita baada ya kuugua.

Credit: Hashim Aziz
 
Back
Top Bottom