Bora kutojua kuliko kujua vibaya

Bora kutojua kuliko kujua vibaya

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,348
Reaction score
1,097
Nyoka alipenya na kuingia katika karakana ya ufundi seremala.

Wakati nyoka anaingia alipita karibu na msumeno wa kukatia mbao, na kudhurika kwa kuchomwa na meno ya msumeno.

Kwa ujinga wa kutojua nyoka akahisi Msumeno unamuangamiza na akaugeukia na kuanza kuupiga msumeno .

nyoka alizidi kuumia mdomoni.

Kwa kutojua kitu gani kinamsibu kufanya aendelee kuumia , nyoka akaona ngoja akiue kabisa hicho, kwa kujiviringa katika msumeno , ili kisipumue na kukiua
Mwisho wake nyoka alikufa yeye badala ya msumeno.

Nini nataka kusema kuna wakati tunashikwa na hasira kwa wale waliotuumiza pasipo kujua tunajiumiza wenyewe.

Katika maisha ni bora kutojali hali , watu, Tabia na maneno ya watu, kwani yanasababisha kujiumiza wewe mwenyewe pasipo kujua.

Kwa sababu si kila kitu inabidi upambane nacho , vingine ni vya kupuuzia.

Kuna wakati ni kweli lazima upambane kwa ajili ya haki yako , lakini kuna wakati hapana ili kupunguza maumivu utakayopata .

Swala si kupambana ukiwa na hasira , ila kufahamu nini hasa kinatakiwa kufanywa kwa ajili ya furaha yako , ukuaji wako, maendeleo yako na umuhimu wa usalama wako pia.

Usije ukaruhusu hasira na jazba zikakujengea hatima yako .

Kwa sababu haijalishi unakumbana na matatizo ya aina gani , ila wewe una react vipi kwa matatizo hayo.

Kumbuka hiki mtu anayecheka anacheka kwa sababu amechekeshwa na mwenye furaha ,daima huwa hacheki ana tabasamu kwa sababu anafurahia. Daima FURAHIA

God bless you

Be inspired
 
Back
Top Bottom