Habibu B. Anga
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 6,557
- 25,716
Hapana shaka hata kidogo mziki wa Bongefleva umepanda chati kwa kasi sana kimataifa hasa barani afrika na wanamuziki wake wamekuwa na ushawishi mkubwa katika kiwanda cha muziki ndani na nje ya nchi..
Mpaka mziki huu umefanikiwa kufika hapo imekuwa ni safari iliyojaa milima na mabonde! Kuna ambao mziki umewapatia ajira na wametoka kimaisha na wapo ambao walichezea shilingi kwenye shimo la choo..
SEHEMU YA KWANZA: BIGGEST LOSERS
5. RAY C
Rehema chalamila (maarufu Ray C) alitikisa vya kutosha mwanzoni mwa miaka ya 2000 (2003 - 2007). Alijijengea mpaka image na heshima ya kuonekana ni moja ya malkia wa kiwanda cha mziki Tanzania akiwa sambamba na kina lady jaydee.! Dalili mbaya zilianza baada ya kuwa na ukaribu na Nako 2 Nako na hasa kiongozi wa kundi la N2N, lord eyez! Baadae wakanzisha mahusiano na muda si muda akajitumbukiza kutumia mihadarati and the rest is history.. Amepotea kwenye gem na hakuna tumaini kama atarudi!!
4. 20 percent
Mpaka sasa ndiye msanii namba mbili kwa kuzoa tuzo nyingi kwa usiku mmoja baada ya kuzoa tuzo 5 za KTMA mwaka 2013! Kuna kipindi ilikuwa kila nyimbo atakayoitoa muda mchache tu inageuka 'nyimbo ya taifa' inaimbwa mpaka na mtoto Mdogo anayejifunza kuongea.. Kizuri zaidi nyimbo zake zilikuwa na ujumbe kiasi hata leo hii ukisikiliza bado unaburudika.. Kilichotokea kwake mpaka kushuka na hatimaye kupotea kabisa kwenye gem anakijua yeye pamoja na producer wake Man water.. Sijui ni mibangi au walikorofishana tu lakini kiwanda cha mziki tumepoteza kichwa hapa..
3. MARLAW
Moja kati ya mazingaombwe ya Bongofleva ambayo bado siyaelewi mpaka leo moja wapo ni hii!! Inawezekana vipi mtu mwenye kipaji, mashabiki, na influence kama Marlawa anapotea moja kwa moja??? Tatizo ni nini? Familia? Mbona kuna wasanii wengi tu wanafamilia na wanafanya vizuri?? Au kampeni za siasa 2010 ndio zilimponza? Lakini mbona ni wengi walishiriki zile kampeni lakini mpaka leo bado wanafanya vizuri?? Alafu kinachoshangaza mpaka leo jamaa ukimsikiliza anaimba unaona kabisa bado anajua?? Sijui ni nini kimemkuta.. Lakini kuna kipindi alipokuwa kwenye ubora wake aliiteka Bongofleva yote!
2. CHID BENZI
Hakuna cha Joh Makini, hakuna cha stamina, hakuna Niki mbishi wala young dee au sijui young nani.. Huyu ndio alikuwa mfalme wa Bongo Hip Hop na alipokuwa katika ubora wake aliiweka Bongofleva nzima kwenye kiganja cha mkono wake.. Walaaniwe wauza unga wote!
1. MR. NICE
Alikuwa ndiye diamond wetu, Alikiba wetu, Navy kenzo wetu.. Mpaka leo bado sijaelewa kinagaubaga hasa nini kilitokea, alibahatisha? Alifanyiwa figusu? Watu walichoka nyimbo za watoto? Alijisahau au pace ya ukuaji wa mziki ilimshinda akajikuta anakaa benchi bila kupenda??
'Honorable' mentions.!
- Mb doggy
- Ferooz + Daz Nundaz
- Lord Eyez
- Wakali Kwanza
- Z-Anto
- Bwana Misosi
- Bushoke
- Dudu Baya
- Crazy GK
==========
SEHEMU YA PILI: BIGGEST WINNERS
Kuna wasanii ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kukua kwa muziki wetu lakini pia wamefanikiwa wao wenyewe binafsi kujijengea heshima kubwa na mafanikio ya kimaisha kupitia kiwanda cha Bongofleva...
Hawa ndio wasanii 5 niliowapa heshima ya kuwa biggest winners wa kiwanda cha Bongofleva..
5. Lady Jaydee
Kama kuna msanii mwenye roho ya paka basi huyu ni namba moja, haijalishi unampiga vita kiasi gani lakini atatafuta namna ya kuinuka na kusonga mbele.. Tangu atoke na albamu yake ya machozi iliyompa heshima ndani na nje ya nchi hajawahi kushuka kwenye game.. Radio mawingu wamejitahidi na bado wanajitahidi kumshusha lakini wapi?? Jaydee ameonyesha mfano kwa wasanii wengine kuwa unaweza kutoboa pasipo kuwa kibaraka wa Radio Mawingu! Sio umaarufu pekee lakini pia jide amefanikiwa sana kimaisha yote chanzo kikiwa ni muziki wa Bongofleva!! Tunapoongelea kuhusu 'Divas' huyu ndiye msanii wa kike diva hasa hapa Bongo.!!
4. Ali Kiba
Aliibuka mwaka 2006 na Cinderella, akaja kuitikisa Bongofleva na Nakshi Nakshi na ngoma nyingine kibao alafu akapotea kidogo. Akaja kuibuka tena 2014 na 'Mwana' na tangia hapo amebakia masikioni mwa watanzania..
Naamini huyu ni moja ya wasanii wenye potential ya kuja kuwa wakubwa Africa hapo baadae! Ana base nzuri ya mashabiki na anajua mziki..
3. Profesa Jay
Profesa jay, wa mitulinga, mti mkavu mwanalizombe ameonyesha power ambayo msanii anaweza kuipata kupitia Bongofleva! Mara nyingi ndiye anakuwa -credited kwa kuipa Bongofleva heshima ya kukubalika na watu wazima! Ni moja ya magodfather wa huu muziki!! Na kuonyesha heshima yake na anavyokubalika wananchi wakamchagua kuwa mbunge wao! Jambo la kufurahisha zaidi mpaka siku Jay anaingia kwenye siasa bado alikuwa hajashuka, bado alikuwa ana hit singles zinazosumbua mtaani (Kipi sijasikia & Tatu chafu)!
2. AY
Ambwene Yesaya ni moja ya watu wenye akili kubwazz kwenye hii industry! Kwanza hajawahi kutetereka kimuziki, toka adondoshe hit single ya 'Raha tu' amebakia kuwa moja ya A-list artists mpaka Leo! Kitu kikubwa zaidi AY kwa sasa amekuwa ni key player katika kuendesha muziki wa Bibgofleva.. Yeye ndiye aliyekuwa msanii wa mwanzo kabisa kusaidia wasanii wengine kufikisha muziki wao level za kimataifa! Yeye ndiye aliye-initiate collabo ya kihistoria ya Diamond na Davido, yeye ndiye aliyefanikisha Mavoko kwenda WCB na mambo mengine mengi.. Kwasasa AY ni moja ya watu muhimu zaidi kwenye management ya Bongofleva but still anaendelea kusumbua kimuziki (Zigo Remix)
1. Diamond Platnumz
OK, where do we start??? Kwa kifupi tuseme tu huyu ndiye icon wa muziki wa Bongofleva kwa sasa! Amefanikiwa kwa 100% kuupa heshima muziki wa Bongofleva Africa! Ukiongelea ile cream ya wasanii bora Africa yeye ni mmoja wao! Ametufikisha pale ambapo tulikuwa tunatamani na kupaota kila siku.. Jambo la kutia moyo zaidi bado hajabweteka kutokana na mafanikio hayo anaonekana ana kiu ya kufika mbali zaidi!!
Lakini kikubwa zaidi Diamond Platnumz ameanza kushift kutoka kuwa mwanamziki wa kawaida na kuwa 'Music Moguel'!!
Lebel yake ya Wasafi ndio yenye ushawishi zaidi hapa nchini kwa sasa! Kwa kifupi kila kitu ambacho Diamond anakigusa turns into gold!! Naamini atafika mbali sana..
Honorable Mentions
- Weusi
- Mwana FA
- Nay wa Mitego
- Shetta
- Ommy dimpoz