tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,424
- 4,768
Hata Bongo ukigusa vifurushi vya Wiki au Mwezi bei ni zaidi ya Hizo, usitetee kitu usichokijuaMara kadhaa utawasikia wabongo wanalalama saaana, kwamba kampuni fulani ya simu, vifurushi vyake ni ghali sana, na hivyo watahamia kwa mpinzani.
Bila shaka wengi wao hawajui kwamba vifurushi vyetu ni bei chee sana. Kuna nchi za Afrika ambazo kupiga simu na kutumia mobile data ni anasa kubwa.
Afrika kusini, ukiwa na MTN huwezi pata 1GB ya wiki 2 kama huna zaidi ya Tsh 25,000/=.
Jirani Kenya, SafariCom wanauza 1GB ya mwezi kama kwa Tsh 10,000/=.
Rwanda 1GB ya wiki MTN wanafanya zaidi ya Tsh 15,000/=.
Wakati Uganda 1GB ya week inauzwa na MTN kwa Tsh 8,000/=.
Hebu linganisha hizo gharama na upatacho Voda, Tigo, Airtel, Halotel na Smart!!!
Watanzania uzuzu na uelewa kufikiria mbali hatuna, utakuta mtu kashupaa anabisha sababu ya ulayman wake anajifanya kuongea ongea bila vigezo..!Unakosea kulinganisha hizo bei bila kuangalia pia pato la watu...kwa mfano pato la mmoja mmoja kwa mwezi katika nchi ulizotaja alifanani kabisa hivyo hata level ya manunuzi inaweza kuwa tofauti kabisa....
Naamini kabisa mfanyakazi wa serikali wa Tz anayelipwa mshahara wa laki 5 hawezi kununua kwa kifurushi cha data huko south na akafurahi...hii kwake inaweza kuwa ni mzigo mkubwa kulingana na pato lake
Halotel kwa data wako vizur usitudanganyeKuna kipindi tigo ilikuwa unapiga simu bure daily ukilipa 1500 tuu,
Ila naona muziki wa data unawaelemea sana sio tigo tuu mitandao yote nimetumia tigo, airtel, zantel, voda, smart, Halotel, sasatel, kote huko vifurushi vya data ni ngumu kumesa,
Kwa sasa tatu bora kwenye data ni
1. VodaCom Tz
2. Halotel Tz
3. Airtel Tz