Bongo Movie mnakera, kwanini hambadiliki?

Nimekumbuka yule jambazi msafi kavaa mask na risasi sasa yupo ndani kavua viati nje asichafue sakafu haya maigizo ata siyaangaliagi tena mara ya mwisho niliangaliaga movie ya YOLANDA

huyo jambazi ni genious sana mana kavua viatu ili asisikike aingie kimya kimya pekupeku.. big up majambazi wote wanaofanya hivo.
 
Ni kweli glory tatiz hawa jamaa zetu bana nakumbuka wakati fln ivi movie ilikuwa ikiisha wanasena toa naoni yako walkuwa wanaweka namba na email, ikafikia hatua wakaondoa kwa kile walichodai kwamba hawawezi kuproduce ktu ambacho kila mtu ataridhika nacho.

Kwa maan hiyo wao wanajiona ni wajuaji na hawataki comment za mashabiki wao basi ngoja wapambane ambae atakuwa anajitambua na kufanya vzr tutasuport kazi yake.

Wangemchukua mtu kama Tchidi Chikere wa Nigeria awape story ya kuact at least wangefanya vitu vya maana kuliko huu ujinga wanaofanya saivi.

Halafu wakati wenzao wanafight kwa gharama yoyote kuonyesha uhalisia hata kwa kitu kidogo tu, huku wanapambana kusave cost ilimradi muvi ikamilike itoke
 
Kwa Bongo sasa hivi tasnia ya filamu imekuwa ya hovyo kabisa...
Wasanii hovyo, maproducer hovyo!
Walishaambiwa mara kibao kuwa wanachokifanya hakiwavutii watazamaji na mbinu za kufanikisha hilo wanaambiwa, lakini hawa wasanii wanaona wakishatoa sinema moja wakishaonekana kwenye Tv wanajiona superstar!
Hawataki kujiongeza..
Filamu ni shule, wanaagiza kwa mazoea na kucopy!

Sasa kama producer ni huyo huyo
Director huyo huyo
Editor huyo huyo
Continity huyo huyo
Sound huyo huyo
Make up huyo huyo
Unategemea nini
 
Hilo la kushindwa kimaintain sauti na background music au effects ndo limenifanya niache kuangalia kabisaaa

Yan zile background sound sijui mziki hua nahisi tu jamaa mmoja anayejifunza kinanda anaenda anajipigia tu then wanakuja kuunganisha.

These cant take even time to learn hata kutoka kwa wenzao wanigeria

Filamu za kinigeria sound tu inakuvutia na kukupa munkari ya kuangalia movie
Na ninahisi wanazigharamia kabisa, maana unakuta ni wimbo wa maana kabisa tena mkali ambao mtu angetolea singo angetoka
 
iv najiulizaga kwanini wasiungane wafanye kitu kimoja kizuri navyosena kizuri namaanisha kuanzia script iwe ya kueleweka sio script inatosha daftari la mtoto wa chekechea tena like la vibox. Je tukisema tuangalie move na kutafuta kitabu cha hio move bongo move hio kitu ipo?. Wapo watu wenye kuandika script nunueni script hawajui mayo hio ni fani za watu tena majuu wanaheshimika sana. Sio mtu anaamka anachukua kamera anaelekea morogoro Mara posta utafikifi wanaenda kushoot video ya kwaya alafu akitoka hapo utasikia Nimefungua kampuni yangu!! dah seriously yani vikamera viwili na tuzagazaga kadhaa tuu wnawaza kufungua kampuni
wabongo mnavunja moyo
 
wabongo mna majungu
mimi sipendagi kuwekewa part1 na 2
 
Habar wapendwa,
Muda kidogo nimekuwa nafatilia kwa karibu sana kazi za wasanii wetu wa bongo,
Kiukweli zinachosha sana na mnatuchosha sisi watazamaji maan kazi za saiv hazina tofauti sana na za zaman maan zamani ilikuwa ukisoma maelezo ya Movie utakuwa ushaangalia film yote.

Tatizo langu kwenu ni kwamba mnashindwa kufanya mantaining ya Vocal na Background songs and effects kitu ambacho si sahihi kwani watazamaji wanahitaji kusikiliza maneno na cyo wimbo au background zenu kwa kuwa wanazo kwenye simu, flash, Pc, hard disk nk.

Kama haitoshi 95% ya actors wanaokuwa walinz wanakuwa wajinga wajinga au walemavu wa mikono nk hivi hamuoni hata kwa wenzenu wa Nigeria?

Suala wa wahusika kuvaa uhusika pia mnashindwa yaan mtu anapigwa rusasi anakufa alafu baada ya kudondoka chini anavuta nguo ili kitovu kisibaki wazi hiyo inakera sana.

Unakuta jambazi amevaa miwani myeusi na jaketi kubwa jeusi anavuta sigara au bangi na amekunja sura acheni kukalili maisha.

Nyie mshakariri kwamba siku zote watu ili wafanikiwe lazima waende mjini huo ni ushamba na nikupotosha jamii na kukatisha vjana walio vijijini tamaa kwani watajua ili wafanikiwe lazima waende mjini, huo ni upuuzi.

Unakuta mtu ana amka ile asubuhi amepaka make up, wanja, lipstick nk huo ni ushamba na haipo badilikeni na kama mkishindwa tutaendelea kuangalia film za nje hata kama ni ghari.

Akafu kwa mwendo mnataka mtusue hiyo haiwezekeni.

Ongeza kingine kinacho kukera.


Ukiacha kuziangalia hizi film zao ndipo watajirekebisha....Bongo muvi na wasanii wao wote ni feki tu, bora waache kuigiza tu wajiuze ili tujuwe kitu kimoja.
 
Back
Top Bottom