Muziki ni zaidi ya kujua kuimba na kuwa na sauti nzuri
Binafsi naamini hakuna mwanamuziki mkali wa sauti na tungo kama Ali Kiba
Diamond anajua kuimba kawaida na sauti ya kawaida sana isipokuwa Diamond anachowashinda wengine ni kujua kufanya muziki
Anachofanya Diamond ndio wanachofanya wenzetu mbele akina lil wiyne nk, kucheza na akili za wapenzi wako
Diamond amekwenda SA akatangaza anakwenda kufanya Video ya pesa kibao na wimbo.....hiyo peke yake ilimfanya kila mtu kutaka kuujua huo wimbo na hiyo video matokeo yake anaacha mjadala amabao haushi midomoni mwa wapenzi wake na kwenye media
Na kabla hauja chuja kakimbia mbio Nigeria kafanya remix na Davido na kutangaza video itakuwa ya dola kibao na itafanywa na jamaa waliotengeneza alingo ya P squre.....hii pekeyake ikafanya video kuwekwa tu youtube kupata viewers wa kutosha na akirudi kuna show za kutosha zinamsubiri
Sasa huyo Ali Kiba sijui na Beka toka watoe single sijui lini kimya na soko la sasa hivi lilivyo watu wakikusahahu kutoka ni ngumu sana
Diamond anajua yupo kwenye hit na ipo siku ata drop ndio maana amaekamatia hapo hapo ni kigongo juu ya kigongo kabla watu hawajamsahau anatoa kitu na majisifu na matangazo kibao......hii inamfanya kuwa juu na anapata mamikataba manono ya mamilioni kutoka makampuni kwasbabu ya umaarufu wake ambao anaulinda kwa gharama yoyote
Kingine ni kufanya mambo ambayo utahakikisha media inakutaja kila wakati...kwa Diamond akina wema ndio ngao yake kila kukicha Diamond diamond