Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,801
- 43,177
Habari zenu, poleni na majukumu ya kazi za leo. Niwatakie usiku mwema wale mnaotoka kazini saa hizi mrejee majumbani kwenu salama, wale mnaoingia kazini saa hizi niwatakie kazi njema.
Kuna siku moja hivi, ilikuwa mwaka jana Kasie alikutana na Bonge la Bwana uso kwa uso. Bwana huyo tulifahamiana kwa mara ya kwanza mwaka 2015 ila machachari na macho juu juu ya Kasie yakafanya Kasie na Bonge la Bwana wachelewe kuonana ana kwa ana. Ila tangu hiyo 2015 tulikuwa tunawasiliana hadi siku ya tukio mwaka jana...... Ambapo mara ya kwanza tulionana Samaki Samaki na hii ya 777 ilikuwa mara ya pili.
Nakumbuka nilikuwa natoka Bagamoyo kwenye tukio la kifamilia baada ya hapo nikawa naelekea Kigamboni kumsabahi rafiki yangu Laura.
Basi huku na huku nikampigia Bonge la Bwana ambae anaitwa Madata (sio jina lake halisi) ila huwa namuita hivo kwa sababu zangu binafsi. Nikamwambia nna hamu ya kukuona uko wapi, walau nikutie machoni tuu. Akanijibu niko 777 kuna mchuchu ana miadi nae hivo nikienda tunaweza kutana na huyo mchuchu mwingine ikawa tabu. Nikamwambia mie sigombaniagi Bwana banaa after all naheshimu privacy na mipango ya mtu so have fun on your date. Mie tutaonana siku ingine, akasema ndo maana nakupenda Kasie huwa unanielewa haraka bila makorofishano.
Basi mie nikaendelea na safari yangu nilipofika Tegeta Madata akanipigia na kuniambia Kasie, I missed you too. Huyu mchuchu mswahili nusu saa imepita tangu muda tuliokubaliana bado hajafika, umefika wapi? Nikajibu Tegeta, akasema fanya ufanyavyo pitia hapa 777 nikuone. nikamwambia mchuchu wako akija je!!! Akasema akija lazima ampigie yeye Madata ili amuelekeze alipokaa hivo hatutaonana, nikamwambia usinichuze bana ukanisababishia tukio.... Akasema usipokuja usinitafute tena looh .... Basi nikawa mpole, nilipofika afrikana nikashika ile barabara ya mbezi chini kama naelekea white sands ili nipite 777.
Nilifika 777 nikaelekezwa na walinzi mahali pa kupaki gari kisha nikampigia, wee Madata umekaa upande gani? Sio nianze kukodoa macho bar yote nakutafuta, akanielekeza na alipokuwa amekaa ninavoingia ananiona kuanzia mbali na nikiondoka ananisindikiza kwa macho hadi natoka nje. Kumbe alifanya makusudi kukaa hapo ili anitazame ninavokuja na ninavoondoka.
Nakumbuka nilikuwa nimevaa kibwebwe cha kitenge (kigauni), kichwani nime twist nywele zangu kipilipili bila rasta na chini nimevaa raba za DH huyoo kwa mwendo wa madaha utasema niko kwenye red carpet nikaelekea alikoketi Madata.
Hahahahaaaaa Bonge la Bwana Madata, nilimkuta anakula mishkaki hivo nikamuacha amalize kula ndo tusalimiane kivyetu vyetu. Nikawa nimesimama namwambia nimefurahi kukuona haya acha mie niendelee na safari yangu na wewe umalizie kula na umsubiri mgeni wako.
Akaniambia kwanza karibu uketi, nikamwambia hapana mie sikai, nikikaa hapa maongezi yatakuwa marefu halafu ntashindwa kwenda Kigamboni, nikawa nalalama kwa sauti ya wizi aniruhusu niende na nisikae hata. Akamuita mhudumu akamuomba alete maji ya kunawa, nikamwambia nooh thanks Madata sitokula akasema sijakukaribisha ule hii mishkaki kwanza sijaipenda ila ukitaka ntakuagizia yako. Nataka kunawa sili tena.... Nikamwambia kwa nini mbona hata ndizi hujala? Basi yalikuwa madeko ya hapa na pale alipomaliza kunawa akanyanyuka akanikumbatia kwanguvu ile ya kuniminya na kunibana kwake. Nami nikamkumbatia halafu nikamnong'oneza sikioni, unanibana sana kwako itasimama halafu utashindwa kukaa hahahahaaa akacheka sana halafu akaniachia ila akanifinya tumboni na kwenye mbavu.
Basi tukakaa akawa anaendelea na kinywaji chake, akasema nijuagizie nini? Mie nikamwambia nashukuru niko vizuri usiniagizie chochote wee endelea kunywa mie niende. Akasema basi ngoja nimpigie yule mchuchu asije nimwambie nimeondoka halafu tuendelee kukaa hapa kisha twende wote kigamboni. Nikamkatalia, kuwa si sawa kwa mchuchu japo kachelewa ila msubiri, mie nipo hata Cape Town tunaweza enda wote huyu mchuchu ni wa hapahapa.
Nikanyanyuka kuwa naondoka akaniambia nani kakuruhusu usimame looh nikasema leo mbona ntakoma...!! Nikakaa kisha nikamwambia, Madata naomba uniruhusu ninyanyuke niende. Akanishika mkono halafu tukanyanyuka wote, kumbatio lililofuata hapo hehehehehee nikamwambia Madata saa hizi bado mchana halafu ukinibana hivo kibwebwe kinanyanyuka kwa nyuma na kuwa kimini mapaja yote nje. Akaniachia ile nataka nigeuke nianze kuondoka, kumbatio tena ikabidi nimtanie ujue nakupaka kikwapa changu halafu mie ntaondoka na marashi yako. Akacheka akaniachia kisha akanifinya kwenye mbavu ili mradi tuu Mahaba uchokozi- sweet nothing movements.
Basi tukaagana vizuri nikaanza kuondoka tena kwa mwendo wa madaha hadi iliko parking. Sikugeuka nyuma hata kidogo asijeniambia rudii aahahahahaa.
Usiku alinipigia simu Kasie wewe, nimeshaunakili mwendo wako na ukipita mahali ntakugundua, akasema wakati nimekukumbatia kweli ilisimama maana nipples zangu zilimgusa kifuani kwake..... Akamalizia kwa kuniambia Kasie, you are my woman and you are my everything..... Nikamwambia una kiu na Mahaba eeehhh utalewaa heheheheee.
Nikamwambia siku tukionana tena ntataka tupimane uzito kwa kutumia mikono. Ile mnakaa kwenye viti halafu mikono mnaweka mezani kwa kuegemeza kiwiko kisha mnashikana viganja na kuanza kupimana nani atauvuta mkono wa mwenzie upande wa kushoto wa kila mmoja (iwapo mnapimana kwa mkono wa kulia). Bado hiyo siku haijafika....
Kiukweli Madata na Kasie ni wapendanao leo nimemkumbuka Madata, nampenda sababu nampenda.
Basi masimulizi haya yanasindikizwa na huu wimbo hapo chini....
Madataaa..... Kasie Matata Kadata juu yako.