Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 130
- 118
Maswa:Ni saa 22 tangu kuwekwa humu jamvini uzi uliokuwa na kichwa cha habari”Bonde la Ziwa Victoria mnataka kuwadhulumu wananchi wa kijiji cha Iyogelo,wilaya ya Maswa ardhi yao mliochimba bwawa?”leo mmefika katika kijiji hicho katika kitongoji cha Bugarama na kufanya tathimini ya maeneo ya wananchi waliolalamika kudai kutwaliwa kwa maeneo yao bila kushirikishwa.
Kwa kitendo hiki niwapongeze kwani mmeonyesha uwajibikaji mkubwa wa kuhakikisha haki za wananchi hawa wanne ambao ni Mwita Jilala Hinda,Gwisu Jilala Hinda,Lwenge Doma Malale na Mahona John Mathias inapatikana na wanalipwa fidia kulingana na taratibu zilizopo.
Naamini kabisa mtachukua muda mfupi kuhakikisha fidia hiyo wanalipwa hao wananchi wanyonge ambao sehemu kubwa ya ardhi yao waliitegemea kwa ajili ya kulima mashamba ili kupata mazao ya chakula na biashara ili kuendeleza familia zao.
Pia niipongeze Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa kwa kufuatilia jambo hili na kupata ukweli wake ambao ulitaka kupotoshwa na diwani wa Kata ya Binza,Aron Mboje na leo hii wananchi hao wamefikia hatua nzuri ya maeneo yao kufanyiwa tathimini ili waweze kulipwa fidia.
Pia nivipongeze vyombo vya habari vyote na waandishi wa habari wote waliopaza sauti juu ya jambo hili kwa kuwasemea wananchi wanyonge kwani walichokifanya ndiyo msingi mkubwa wa kazi yao na vyombo vyao.