Bomu la Nuclear omba lisikupate

Sazira kwetu

Senior Member
Aug 23, 2015
155
104
Kwema wana Jukwaa?

Baada ya salamu nirejee kwenye ada yangu ambayo kichwa chake cha habari bado hajijajitosheleza kuelewa naongelea nini.

Siku moja nilienda kumtembelea dada yangu anaenifuatia kwa kuzaliwa baada ya mimi, wakati anaolewa nilikuwa masomoni kwa hiyo sikuhudhuria harusi yake sasa nilipopata fursa ya kwenda kumtembelea kwake ndipo kisa cha bomu la Nuclear kilipo.

Baada ya kufika kwa dada yangu tukiwa wageni wake mimi nikiwa nimeambatana na mke wangu tulikaribishwa vizuru kwa kuandaliwa chakula kizuri na cha haja na dada yangu mpendwa.

Chakula tulichoandaliwa kilikuwa ugali wa mahindi na nyama ya kuku na baadae wali na nyama ya kuku, kwa kweli ugeni wetu ulikuwa mzuri sana tulikula na kushiba baada ya hapo tulipiga stori za maisha na shemeji yangu huku wife akipiga stori na wifi yake.

Usiku ulivyoenda tulilala na asubuhi kulipokucha tulipiga mswaki na kupewa chai na viazi vitamu vya kuchemsha na kiporo cha wali lakini mimi nilipenda sana viazi na kwa kuwa dada yangu kaolewa na mfugaji ili kusindikiza viazi nikaletewa maziwa ya mgando nikashushia kwa kweli ugeni wetu ulikuwa mzuri na enjoyable sana.

Baada ya chai tukaaga kuwa tunaondoka shemu na dada yangu walitupinga sana na kusema tuondoke kesho yake lakini tukawashinda hoja na wakakubaliana na ombi letu la kuondoka siku hiyo ila wakesema tusubiri chakula cha mchana tukasema sawa ila lazima tuondoke siku hiyo.

Tuliandaliwa chakula cha mchana kwa kupikiwa ugali na nyama ya kuku, maziwa ya mgando na wali tukala na kushiba vilivyo, baada ya hapo tukaoga na kusindikizwa na wanyeji wetu.

Njiani tumbo lilichafuka na kuanza kuunguruma na nikaanza kujamba hovyo hovyo ili kupunguza gesi ilijaa tumboni, sasa wadau usiombe hali hiyo ikukute utajuta na nadhani kila mmoja katika maisha yake alishawahi kuchafukwa na tumbo na kuleta tafurani mahala alipokuwa.Sasa tukiwa njiani nikiwa najikongoja taratibu na huku nikisoma uelekeo wa upepo unapoenda ili nikiachia ushuzi usilete kero na tufurahi kwa niliokuwa nao.

Ilifikia mda nikiwa nadanganya kwamba naenda kukojoa kumbe nilienda kujamba na kukaa kusubiri kijampo kiishe harufu ndipo nawakimbilia na kuungana nao.

Tulifika kituo cha usafiri na Mungu si athumani mda si mrefu toka tufike kituo cha basi tukapata usafiri, Gari likaondoka huku tumbo likiunguruma na kuuma uma kwa mda huo wote sikumwambia yeyote yule kwa kuhofia kuniambia maneno mabaya na kunifanya nijisikie vibaya.

Mungu hamtupi mja wake tukiwa njiani akaingia mama na watoto watatu umri wao ni kati ya miaka 8,5 na mdogo alikuwa wa kwenye ziwa, safari ikaendelea huku tumbo likiwa linauma na kuunguruma.

Tukifika mahala uzalendo ukanishinda na gari ilivyokuwa ikiyumba kushoto kulia nitatumia furusa hiyo kujibana makalio na kuuachia ushuzi Chiiiiiiiiiiiiiiiii na baada ya hapo kilichotokea usiombe ndugu yangu utazani panya kaoza, omba haya yasikutokee kila mmoja kwenye gari ni kutafutana na harufu haitaki kuisha mpaka abiria wote wakaomba dereva asimamishe gari abiria wapate hewa safi.

Masikini wa Mungu watu wote wakamshambulia mama wa watoto wale watatu na kila mmoja nyie watoto kwanini mnatuchafulia hali ya hewa.

Ndugu zangu hilo ndilo bomu la Nuclear lililobeba kichwa cha habari, wengi mtanidhihaki ila kwa kweli hali hiyo ilishawahi mtokea kila mmoja kwa nyakati tofauti katika maisha yake.

Mwisho tulishuka na kufika nyumbani na kwenda chooni na baadae nikaoga na kwenda kulala, tukiwa tumelala nikukumbushia mke wangu kwa kumwambia alijamba ni mimi basi alicheka sana mpaka sasa nikukumbushia bomu la Nuclear hucheka kila wakati.

Tupeane uzoefu katika hali kama hiyo ilipokukuta ulitatua vipi?
 
Teh teh! pole sana ndugu, maisha yana mengi, ila kula kwa KIASI ni jambo limfaalo kila mtu.
 
kiswahili chako sio kizuri....nina uhakika wewe sio raia wa nchi hii tukufu
 
Kule kwetu mpaka leo hawajui kama Mwanaume anajamba. Ila wewe unahadithia kabisa. Kweli jando ni muhimu sana.

Wewe ni mwanaume wa wapi?
 
Hahahhahahahhahaha u made my nyt nlikuwa na stress lkn zimeisha
 
Ni busara sana ukiwa una ratiba ya kusafiri usipende kula sana. Hata kama ni vinono na rojorojo za mbinguni
 
kiswahili chako sio kizuri....nina uhakika wewe sio raia wa nchi hii tukufu

Haha haaaaaaaaaaaaa mimi ni mtanzania kwa kuzaliwa tena nimekulia mikoa ya Kanda ya ziwa, mzaramo maneno gani yanatanabahisha mimi sio mtanzania? Usiku mwema mzaramo ila kama umeoa epuka bomu la Nuclear.
 
Frankly speaking wewe ktk maisha yako mpaka mda huu hajawahi kuchafukwa na tumbo? Usiseme kuwa mim ni mroho hapana hutokea hata kama hujala sana.
Mkuu haya mambo ya kuchafukwa sio mazuri bhaana,unajua watu wangejua wewe ndio unaejamba ,wangejua unawa BEEP,sasa hapo ungeona MIKONYEZO.
 
Back
Top Bottom