Bomoabomoa ya Mpanda ni vilio vitupu

Peacesmart

Senior Member
Joined
Apr 19, 2017
Posts
113
Reaction score
101
Bomoabomoa Mpanda ni Vilio Tupu, Mamia ya Nyumba Zabomolewa Wakazi wa maeneo ya Tambukareli, Mpanda Hotel na Msasani, wamejikuta katika sintofahamu baada ya Shirika la reli Mkoa wa Katavi kuwataka kubomoa nyumba zao baada ya kuvamia reli na mali zake.

Zoezi hilo ambalo limezikumba kaya takribani 200 kufuatia agizo hilo ambalo wakazi hao wamesema kuwa wao wanashangazwa vipimo vilivyotumika na shirika hilo.

Tutafika tu[emoji40]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dakika ya 8:03...... ndo mtaji wenyewe wa CCM....yaani anashindwa kuelewa nani aliyetoa maagizo na nani anatakiwa amuombe msaada
 
Mkuu nimefuatilia ni kweli na hilo zoezi limetembea mikoa kadhaa wengi hawana makazi so sad[emoji40]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dakika ya 8:03...... ndo mtaji wenyewe wa CCM....yaani anashindwa kuelewa nani aliyetoa maagizo na nani anatakiwa amuombe msaada
Watanzania wana maajabu sana, kuna mtu anafikiri hao wana uhuru tu wa kutekeleza hayo bila msukumo wa mkuu? Kazi ipo
 
Mhh mwaka huu, wagonjwa wa pressure watakuwa wengi mno...poleni sana...
 
Wanabomolea watu nyumba wakati hata huo mradi awamu ya kwanza tu haujaanza,serikali hata kama wanataka kuzibomoa wawape muda wananchi sasa haraka ya nini wakati hata morogoro hawajafikisha huo ujenzi sembuse mpanda. Huu ni uhayawani hiyo mpanda itafikiwa baada ya miaka 10-20 mbele ,Leo unawalaza nje wananchi wako ili iweje!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mama mwehu kweli hahaha ameachika kwa ajili ya kumpigia kampeni magufuri [emoji13] [emoji13] acha aisome namba sasa!! Hahaha wanawake tutulie kishabikia mijitu ya hovyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…