Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,998
Kwa mtu ambaye tokea alipokuwa waziri alionesha ujasiri wa pekee katika kubomoa nyumba, na kwamba alipokuwa waziri mara kadhaa "ngazi za juu" ilibidi wamzuie, pale munkari wake wa kubomoa nyumba ulipompanda, sio jambo la kushangaza kwamba sasa hivi akiwa ndiye Rais, hakuna tena wa kuzuia munkari huo pale unapopanda. wala haikushangaza kwamba mwaka ule ule wa kwanza wa utawala wake, JPM alianza kampeni kubwa ya bomoa bomoa. ilisitishwa sijui kwa sababu za kisiasa, lakini siyo kwa sababu JPM "anajali maisha ya watu" kama alivyotaka kutusadikisha Bashite hivi karibuni. lakini hakuweza kuuzuia munkari huo kwa muda mrefu. Bomoa bomoa imeanza tena...
Kwa hakika, Tanzania ina matatizo mengi sana. ujenzi holela ni mojawapo. Lakini ujenzi holela siyo msingi wa tatizo. ujenzi holela ni matokeo ya tatizo jingine. na tatizo hilo la msingi haliondolewi kwa kubomoa bomoa.
Ujenzi holela unatokana na usimamizi mbovu wa serikali. tunayo mipango ya miji yetu. kinachotakiwa ni usimamizi kuhakikisha kwamba ujenzi unafanyika katika maeneo yaliyotengwa kwa ujenzi wa nyumba au kwa viwanda au kwa makanisa. ni jukumu la Serikali kupeleka mahitaji muhimu katika maeneo hayo yaliyopangwa, mfano umeme, maji taka na safi, nk. Nchi nyingi za kiafrika zimefanikiwa katika hili. Jambo lingine muhimu sana ni kuhakikisha kwamba Serikali inawekeza sana kule ambako watanzania wengi wapo. Vijijini. Unaweza kushangaa kuambiwa kwamba katika awamu ya kwanza ya uongozi wa taifa letu, ambayo ilikazia sana uwekezaji vijijini - Rural Development programs, idadi kubwa ya watu ilibakia kule kule vijijini. wakulima walikuwa wanalima vizuri na kufaidika, na maisha yalikwenda. kilichotakiwa ni kuendelea kuwekeza huko ili idadi kubwa ya watu iwe na ajira huko huko.
Lakini serikali zilizofuatia zilifikiri kwamba kuwekeza vijijini sijui ni ushamba? maana tangu awamu ya pili ilivyoondoa ruzuku ya kilimo, kwa hatua tatu, awamu ya tatu ilipigilia msumari kwa kuibuka na "soko huria", ambapo walanguzi waligeuka wanunuzi wakubwa wa mazao, na kuvuruga mfumo mzima. awamu ya nne iliibuka na KILIMO KWANZA, ambapo watu walipiga hela kulia, kushoto, juu na chini. na awamu hii nayo wala haisomeki kwa lolote kuhusu kilimo.
Wakati awamu ya nne iliibuka na miradi ya "MACHINGA COMPLEX" ili kujaribu kushughulika na wingi wa vijana mijini, ufumbuzi ambao si ufumbuzi. unatibu homa badala ya kutibu malaria. matokeo yake watu wengi zaidi wanazidi kumiminika mijini. awamu ya tano inaibuka na ma-fly over, kuboresha miji yetu. yote hiyo inakwepa tatizo la msingi: THE RURAL FACTOR. Suala la Vijijini. bila kupata ufumbuzi wa nini kifanyike katika vijiji vyetu, hakuna ufumbuzi wowote utakaokuwa wa maana.
Kumiminika watu mijini kunaweka presha katika mipango miji. watu wanajenga popote, ili mradi wajenge. na kwa sababu wanakuja mjini bila mpangilio, bila kazi maalum ya kuwaweka mjini, wanalazimika kuishi maeneo ambayo hayapimwi na hayauzwi. na wanaishi hapo pia ili kurahisisha kuingia na kutoka mjini. watu kama hao hata ukiwahamisha na kuwapa viwanja mabwepande, wataviuza na kurudi mabondeni. kule mabwepande watafanya kitu gani? na hawana uwezo wa kusafiri kuja mjini kufanya vishughuli vyao.
Sasa unapokuwa na nchi ambayo haioneshi ujasiri wa kukabili matatizo kwa hekima na heshima ya kibinadamu, na ipo tayari kubomoa nyumba vyovyote iwavyo, ndio unafika hapa tulipo. Ila tofauti ni kwamba Bomoa bomoa chini ya urais wa JPM, ni bomoa bomoa inayofanyika WITH ZEAL. yaani kuna hamasa ya pekee. unapata hisia kwamba kuna mtu au watu hapa ambao wanapata "nishai" ya pekee wakibomolea watu. ni sawa na addiction. ukiwa mbomoaji wa majumba daima utakuwa mbomoaji tu. ni sawa na kula nyama ya mtu.
Maana hata kama kuna tatizo la ujenzi holela, kuna njia pia za kibinadamu za kutatua hilo tatizo. hii ya kubomoa bomoa ni msiba mkubwa sana kwa wahanga wa ubomoaji.