Bomoa bomoa ya machinga iendelee kwani ni zao la mwendazake

Bomoa bomoa ya machinga iendelee kwani ni zao la mwendazake

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,132
Reaction score
24,438
Walisulubishwa na mgambo wa jiji na vitu vyao vikamwagwa na kubebwa,nimecheka sana kwani wanavuna walichokipanda

Katika watu ambao siwezi kuwasamehe ni machinga na hao wenye vibanda kando ya barabara kwa dhambi ya kumsapoti jiwe

Hawa watu 2020 walimsupport jiwe kukabidhiwa nchi, mtu ambaye utawala wake ulitesa watu, wakaungana nae na kuhakikisha anashinda na kuwatukana wapinzani

Nyie machinga hatujasahau nyie mlikuwa mnatukana wapinzani na wapenda haki na kuwa na upendeleo kwa kumuunga mkono jiwe na kuunga mkono harakati za jiwe kuwakandia wapinzani

Sasa yamewakuta, wacheni mnyooshwe, uzuri mlowachagua ndo wanawatiya adabu,mama anaupiga mwingi leo nimeona mkinyanganywa bidhaa zenu zote, na mabanda yenu kubomolewa na kuchukuliwa mbao zote za mabanda,mabati kila kitu, mlizoea kudekezwa na jiwe na hayupo na alizikwa na vitambulisho vyenu kule Chato..

Nimeona manyanya, viazi, vitunguu, na vitu vyote vikimwagwamwagwa na kuharibiwa na mgambo wa jiji, hili ni funzo kwenu muache kutumika kisiasa siku nyengine oneni sasahivi hakuna wa kuwatetea tupo bize na mema ya awamu ya sita nyie vuneni mlichokipanda.

Leo nimecheka sana, angalau mabanda ya kuku yatapungua sasa nchi ya ahadi ya jiwe ilikua ni nchi ya viwanda lakini badala yake ikawa ni nchi ya mabanda ya machinga kila mahali, ilifika mahali mtu unakosa hata pa kupark gari yako, ajali zinatokea kwasababu ya vibanda kuziba barabara
Wapita njia wanagongwa kwasababu pa kupita hakuna ni vibanda vimejaa
Foleni inakua kubwa mtu unakosa hata barabara ya mchepuo kwasababu ya vibanda uchwara bidhaa zenyewe sasa ni low quality!!!!

Lazima waondolewe kabisa, waliua biashara zetu za maduka,mimi ni maduka na kodi nalipa,frem nalipia, kijana wa dukani namlipa wewe unakuja kujenga banda lako la hovyo la miamzi mbele ya duka langu na unauza same product!!!!Na hulipi kodi wala nini!!huo si upuuzi?Ni kichaa tu anaweza kummiss mwendazake wallah....Na machinga ni zao la mwendazake waacheni washughulikiwe tu
 
Back
Top Bottom