bomoa bomoa nchi nzima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

bomoa bomoa nchi nzima

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Dec 8, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  BOMOABOMOA kubwa na ya muda mrefu inatarajiwa kufanyika katika maeneo mengi ya miji na vituo vikuu vya biashara nchini ambapo serikali itachukua viwanja, nyumba, mashamba ya watu na kuwafidia wenye mali na wapangaji wao kwa nia ya kutekeleza mradi mkubwa wa kununua, kujenga na kuboresha nyumba bora za bei nafuu kwa wingi kwa ajili ya watu wa vipato vya aina mbalimbali.

  Taarifa za awali za kutekeleza mradi huo zilizowekwa katika mtandao wa Benki Kuu (BoT), Oktoba mwaka huu, zinaeleza kuwa bomoabomoa hiyo ni sehemu ya matokeo ya utekelezaji wa mradi huo utakaoanza kufanyika baada ya Benki ya Dunia kuipa Serikali ya Tanzania mkopo wa kuanzia shughuli za ujenzi wa nyumba bora kwa wananchi wake.

  Kwa sasa kwa mujibu wa Ripoti ya Bajeti ya Kaya (HHBS) ya 2007, familia nyingi zinazoishi vijijini sawa na asilimia 92.3 zinamiliki nyumba ambapo sehemu kubwa ya wakazi wa mijini sawa na asilimia 45 hawamiliki nyumba huku wakazi wa jiji la Dar es Salaam sawa na asilimia 61.2 wakiongoza kwa kuwa wapangaji katika nyumba wanazoishi.

  Hata hivyo, asilimia 67 ya nyumba za Watanzania wote zina sakafu ya udongo huku asilimia 65.1 zikiwa na kuta za miti, majani, udongo au mawe wakati asilimia 43.9 zimeezekwa kwa nyasi, miti na udongo.

  Mradi huo ambao awamu ya kwanza ya maandalizi yake inatarajiwa kuanza katikati ya mwaka 2010, unatarajiwa kusimamiwa na BoT ambayo ndiyo wakala wa serikali katika uchukuaji wa mkopo huo na utaanzisha chombo (mortgage liquidity facility au MLF) ambacho kitakuzwa kwa hatua mbalimbali ili kitekeleze jukumu kutoa nyumba bora kwa njia ya mikopo.


  Katika hatua ya kwanza ya utekelezaji, kitatoa huduma yenye lengo la kukuza soko la kukopesha nyumba. Chombo hicho kitatoa mkopo wa muda mrefu utakaowezesha watu wengi kuanza kukopa nyumba bora zitakazokuwa zimeshajengwa tayari na kuanza kulipa taratibu wakiwa wanaishi katika nyumba hizo.

  Chombo hicho kitasaidiwa na Benki ya Dunia kupata fedha za kuanzia na kitaendelea kupata mikopo kutoka katika benki hiyo na taasisi nyingine za fedha mpaka kitakapoanza kujiendesha chenyewe na kujenga mtaji mkubwa wa kufanya shughuli zake na kuhusisha wadau wengine ndipo benki hiyo itajiondoa polepole ili kiwe cha kudumu na kiendeleze shughuli yake ya kukopesha nyumba.


  Katika hatua ya pili chombo hicho kitaanza kutoa mikopo ya muda mrefu kwa miaka mitano au zaidi na mazingira ya utoaji huduma ya mikopo hiyo yataendelea kuboreshwa mara kwa mara ili kuhakikisha mikopo hiyo inatolewa kwa watu ambao wana uwezo wa kurudisha.

  Katika hatua ya tatu sekta binafsi itakabidhiwa mikopo na maeneo ya kujenga nyumba zitakazokaliwa na watu wa vipato mbalimbali kwa kutumia teknolojia ya ujenzi nafuu kwa kufuata sheria ya mipango miji ili ziuzwe kwa watu watakaopewa mikopo ya kununua nyumba.

  Taarifa hiyo ambayo ni ya awali imebainisha kuwa taarifa kamili ya mradi huo itatolewa kwa lugha za Kiingereza na Kiswahili mara itakapokamilika ili wananchi waipate na kwa sasa uandaaji wake umeshawahusisha wadau kutoka Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam ambako utafiti wa awali ulifanyika.

  Hata hivyo, wataalamu walioandaa taarifa hiyo waliotajwa kwa majina ya Saada Juma na Bashiru Abdul wamebainisha kuwa mradi huo utatekelezwa nchi nzima lakini katika hatua iliyofikiwa bado maeneo yatakayohusika katika utekelezaji wa mradi huo hayajabainishwa.

  “Bado hatujaainisha maeneo husika na shughuli zitakazofanyika katika maeneo hayo ambazo baadhi zitahusisha watu kulazimika kuhama katika maeneo wanayoishi bila kupenda na au kuchukuliwa kwa ardhi yao na kukatazwa kutumika kwa mali zilizopo katika maeneo yao,” ilielezwa katika taarifa hiyo.

  Baadhi ya wadau wengine waliohusishwa katika uandaaji wa taarifa hiyo ni pamoja na BoT, Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benki ya CRDB, Benki ya NMB na Benki ya Azania.

  *Fidia kwa waathirika

  Hata hivyo wote watakaokumbwa na bomoabomoa hiyo pamoja na wapangaji wao wanatarajiwa kufanyiwa tathimini ya mali zao zitakazoathiriwa na shughuli hiyo ambayo ni ya muda mrefu na kulipwa kabla ya kutakiwa kuhama na au kuanza kwa shughuli hizo.

  “Malipo yatafanyika kwa kila jengo ambalo litavunjwa kwa ajili ya kumhamisha mtu au kama litaathirika kutokana na kuanza kwa ujenzi wa nyumba bora.

  “Vyumba kama sehemu za biashara, majiko, maghala au stoo, baraza, vyoo, visima na uzio utakaovunjwa vitafanyiwa tathimini sawa na itakayofanyika kwa mtu atakayevunjiwa nyumba nzima na malipo yatafanyika kwa kuzingatia gharama za ujenzi kwa thamani ya soko ya wakati husika na gharama ya kujenga upya majengo hayo italipwa,” imeeleza taarifa hiyo.

  Ardhi ambayo ipo wazi ambayo itachukuliwa italipwa kulingana na ukubwa wake na bei ya soko ya eneo husika na kama itakuwa imepandwa mazao au imetayarishwa kwa ajili ya kupanda mazao, malipo yatajumuisha bei ya vibarua katika eneo husika kwa wakati husika na muda ambao ulitumiwa na vibarua hao kuandaa shamba husika.

  Aidha wakulima watakaolazimika kutoa mashamba yao watapewa ardhi nyingine ya kulima na watalipa gharama za kibarua za kuandaa shamba husika kwenye ardhi nyingine ambayo watakabidhiwa na itajumuisha gharama za awali za kuandaa ardhi, kulima, kupanda, kupalilia mara mbili na kuvuna na fedha hizo zitazingatia bei ya soko ya kufanya shughuli hiyo.

  Kama shamba litakuwa na mazao ya biashara na ya chakula, malipo ya mazao hayo yatazingatia bei ya mazao hayo kwa mwaka uliopita pamoja na ongezeko la bei litakalotokana na mfumuko wa bei, na kwa mazao ya miti ya kudumu malipo yake yatahusisha bei ya mazao kwa mti na historia ya uzaaji wa mazao ya mti husika.

  Miti ya pori italipwa katika malipo ya kijiji. Hata hivyo maeneo ya kufanyia ibada yakiwemo ya misikiti na makanisa pamoja na maeneo ya matambiko na makaburi yametengwa kuwa maeneo ya kitamaduni na takatifu na ili kuepuka mgongano na jamii mradi huo hautayahusisha.
   
 2. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo habari umetoa source gani??
   
 3. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  yaani yale vile vibanda vya miti vilivyokandikwa udongo vinavyohitaji major repair au kujengwa upya kila baada ya masika moja ndio wanaita "nyumba" ?

  plizzzz gimme a break for the sake of my sanity!!!
   
Loading...