Bomoa Bomoa Mabondeni inauma, ila Hakuna namna kuondoka Lazima

spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,599
3,223
Wakuu,
Hili zoezi la kubomolea waishio mabondeni mie naliunga mkono, hata kama nitaonekana kituko mbele ya baadhi ya wadau.

1997/1998 nilikuwa nasoma sekondari hapa Dar hivo elnino niliiona Kwa macho yangu.

Nitaongelea Bonde la Mto Msimbazi peke yake kama mfano.
Nilikuwa nikiishi Segerea, kulikuwa na daraja la Chuma lililojengwa na jeshi pale Segerea seminary tulikuwa tukivuka kwenda Stakshari hadi banana. Lilisombwa na maji, na maji Yale yalikuwa yanaanzia huku seminary mpaka upande wa pili huku Karakata- umbali wake ni kama mita 600-800.

Njia ya Kinyerezi ilikuwa haitumiki maana hapakuwa na watu wengi kama leo.

Ukija hapa Baracuda maji yalianzia linapoanzia Bonde tu, namaanisha ni kama mita 300 kutoka bar yenyewe ya baracuda linapoanzia Bonde hadi machinjioni vingunguti, nyumba hazikuwepo zote zile.

Naomba niseme kwamba ukitoka Aroma hospital kama unakuja relini kuna Ghorofa upande wa kushoto pale yalikuwa ni maji ingawa nyumba nzima haikufunikwa. Ilisuffer sana muulizeni mwenye nayo.

Tabata Matumbi darajani hapakuwa na Viwanda sana kama Leo, kama mnakumbuka hata mwaka Juzi tu kunamakontena yalisombwa toka ktk godown na kuwekwa barabarani Mandela.

Eneo lile watu wamemwaga vifusi na kuziba mto completely.

Kuna siku moja maji yalitoka milimani Morogoro bahati nzuri ilikuwa mchana kuna mtu alikufa alikuwa amelala maeneo ya Tabata, maji yalimzunguka pia Maji yalivunja kuta za magodown ulizeni ktk kile kiwanda cha nguo NIDA', Azam tv na maeneo ya jirani nakumbuka yalivunja na kuingia viwandani mchana mchana. Hadi upande wa bonde la mabibo.

Guys, hii sii ya kutunga bali ni ukweli mtupu. Ubishi huu na lawama lawama zisizo na msingi ipo siku maiti zitasombwa hadi Indian Ocean tushindwe hata kuzika maiti. Yale maeneo ni hatarishi kupita ubishi huu usio na tija.

Makamba RC miaka hiyo alijaribu kupiga mikwara, watu wahame lakini hakusikilizwa. Viongozi wamekuwa linient kupita kiasi na siasa ktk kila jambo. Hii ni hatari sana.

Ningeomba television za kipindi hicho ITV,dtv,cten na star TV waoneshe Yale mafuriko maana kuna kuna watu hawaelewi.

Serikali ningeiomba kama inaweza iwape japo viwanja ingawa wa mabwepande waliviuza na Leo hii wanalia Tena.

Kisarawe njia ya kuja Mlandizi kuna Maeneo mengi na ni mapori waje waanzishe Makazi. Eneo salama.

Kuziba mito kunasababisha kushindwa kupumua na matokeo yake maji yanafura, Kwa kuyaziba kila sehemu ipo siku yatazagaa mpaka airport mpaka kambi ya jeshi Gongo la mboto na mitambo ya Gesi kinyerezi.

Mimi Nina ushauri kidogo ingawa fani yangu sio ya uhandisi wa Civil.

Jangwani pale serikali imekosea kujenga Barabara za chini, maana hakuna pia madaraja ya kumpitisha maji ya kutosha zaidi ya kuwa ni barrier tu. Barabara mpya ya Kampala-Entebbe inaweza kuwa somo zuri Kwa wahandisi wetu. Tazama uzi chini

Wameipandisha juu mita kadhaa juu ivi na kutoa fursa ya maji kupita bila shida.

Naomba tujifunze na tuelimike.

To have an incident is unfortunate, to have an incident and learn nothing from it is unforgivable.

Entebbe-Kampala Highway | U/C - Page 5 - SkyscraperCity
 
Last edited:
Hata hawa hawataki kubomolewa?
 

Attachments

  • 1452082157774.jpg
    1452082157774.jpg
    18.3 KB · Views: 50
Wazitoe, huu utakuwa ni wehu.

Ni zoezi gumu lakini hakuna njia Nyingine
 
Umeandika ukweli mtupu mkuu ,nilikuwa chuo 97/98 najua mvua za el-nino zilivyovuruga nchi
 
Umeandika ukweli mtupu mkuu ,nilikuwa chuo 97/98 najua mvua za el-nino zilivyovuruga nchi

Ninatatizwa na nini hasa watanzania wanataka.

Hii pia inanipa somo Kwa nn baadhi ya viongozi wanaitwa madikteta au Kwa nn huamua kuwa hivo
 
Sawa tu nakubali watu wanatakiwa waondoke maeneo hayo!
Lakini serikali ingetumia ustaarabu kidogo kuwaondoa watu huko
1)wangewaorodhesha wenye nyumba zote na kuwatafutia eneo kubwa na kuwajengea
Vijumba (kama police post)kwa kila mwenye nyumba
2)wahakikishe hivyo viwanja wanapata wale tu waliyo bomolewa syo kuruhusu vigogo wa manispaa na wafanyakazi wake kujipaa viwanjaa wao na kujimilikisha
Hadi kufanya wahanga wa ubomoaji kukosa viwanja
3)serikali isiruhusu tena mwananchi kurudi kujenga ktk eneo lililobomolewa...Ikiwezekana wa weka sign board kubwa yenye kusema hakuna ruhusa kufanya makazi ktk eneo hilo

Ovaaa
 
Wajameni mjini kutamu jamani,ila nyinyi ndio hamuwaelewi wanamaanisha nini
images
images
images
images
 
Sawa tu nakubali watu wanatakiwa waondoke maeneo hayo!
Lakini serikali ingetumia ustaarabu kidogo kuwaondoa watu huko
1)wangewaorodhesha wenye nyumba zote na kuwatafutia eneo kubwa na kuwajengea
Vijumba (kama police post)kwa kila mwenye nyumba
2)wahakikishe hivyo viwanja wanapata wale tu waliyo bomolewa syo kuruhusu vigogo wa manispaa na wafanyakazi wake kujipaa viwanjaa wao na kujimilikisha
Hadi kufanya wahanga wa ubomoaji kukosa viwanja
3)serikali isiruhusu tena mwananchi kurudi kujenga ktk eneo lililobomolewa...Ikiwezekana wa weka sign board kubwa yenye kusema hakuna ruhusa kufanya makazi ktk eneo hilo

Ovaaa

Zoezi hili si la hapa Dar tu ni nchi nzima.

Fidia gharama yake ni kubwa labda wale wenye offer na Gari

Naunga mkono kuweka alama au kila Bonde kama wanachofanya tanroad

Serikali iwaadabishe waliohusika kutoa hati maeneo hayo.
 
Last edited:
Wabolewa wakaisome namba
Hili sio zoezi la kufanyia ushabiki kiongozi, japo inauma kuona nyumba zikishushwa kama uyoga... ni zoezi gumu sana!
Imefikia mahali tujifunze, unapotaka kujenga lazima ujiridhishe kupitia mamlaka zinazohusika. Sio vitu cya kutolea rushwa coz huwezi kujua baada ya miaka 20-30 ni nani ataongoza nchi.
Leo nilipita wizara ya ardhi, kuna watu kama sisimizi asee!!
 
Hongera mkuu kwa uzi wako

Shukrani kiongozi.
Mie nadhani ni jambo jema ku speak out pale serikali tunapofanya jambo zuri ingawa linauma. Siku zote tumekuwa tukilalamikia serikali lakini ktk hili mie naiunga mkono kabisa
 
Last edited:
Back
Top Bottom