Bomoa bomoa kutua mjini Maswa

Bomoa bomoa kutua mjini Maswa

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,698
Reaction score
2,262
BOMOA-BOMOA-1.jpg
​

WANANCHI waliojenga kwenye vyanzo vya maji wametakiwa kubomoa nyumba zao kwa muda wa siku saba ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa wilaya hiyo.

Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Maswa (Mauwasa), wilayani Maswa, imewataka wananchi kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Dk. Seif Shekalaghe, la kuondoka kwa waliojenga ndani ya mita 60 kutoka vyanzo vya maji na madakio yote ya maji yanayopeleka katika bwawa la New Sola, ambacho ndicho chanzo kikuu kinachosambaza katika vijiji 11, kijiji cha Zanzui.

Akizungumza katika uwekaji alama ya X katika nyumba hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mauwasa,Mhandisi Merchades Anaclet, alisema katika utekelezaji wa operesheni hiyo hakutakuwa na majadiliano na kuwataka watu wote waliojenga ndani ya vyanzo hivyo kubomoa wenyewe.

Alisema operesheni hiyo imezingatia Sheria ya maji na itasaidia upatikanaji endelevu wa maji, hivyo amewataka wananchi wapishe vyanzo vya maji kwa hiari kabla ya nguvu kutumika kuwaondoa.

“Tunawaomba wananchi waanze kuvunja nyumba zao wenyewe kabla ya muda tulioutoa kwa kuwa kinyume cha hapo, tutavunja sisi na gharama zitakazotumika watazilipa watu wote waliohusika kuvamia vyanzo hivyo,” alisema.

Alisema kuwa ombwe la wananchi na taasisi za serikali kujenga katika vyanzo vya maji ni tatizo sugu nchini linalohitaji tiba ya
kisheria ili kuepuka athari za uhaba wa maji zinazojitokeza na zitakazojitokeza miaka ya baadaye.

Hata hivyo, ubomoaji huo umepokelewa kwa hisia tofauti na wakazi waishio katika maeneo hayo huku wakilalamika kutoandaliwa kuondoka katika nyumba zao na wengine kudai kupatiwa viwanja na idara ya ardhi Wilaya ya Maswa.

Wananchi hao ambao ni waathirika wa ubomoaji wameiomba serikali iwapatie maeneo mbadala licha ya kuyamiliki maeneo hayo kihalali na kulalamikia kuwa bomoa bomoa hiyo huenda ikarudisha nyuma maendeleo ya wananchi.

Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Maswa,Vivian Christian, alisema idara yake haijawahi kugawa viwanja kwa ajili ya ujenzi wa makazi, biashara au taasisi katika eneo hilo la vyanzo vya maji na kuwataka wote wenye madai hayo kufika ofisini kwake wakiwa na nyaraka zinazoonyesha uhalali wa kupatiwa viwanja hivyo

Chanzo: Nipashe
 
Hivi mbona hapa TZ karibu kila kitu kinaanza kwa mtindo wa kushtukiza? Yaani hata kufanya usafi ni mpaka rais aliposema ndipo "kila mtu" akanzisha kwenye wilaya yake. Madawa ya kulevya vivyo hivyo. Mkuu wa mkoa Dar alipoanza kufuatilia wanaojihusisha na madawa ya kulevya ndipo mikoa mingine nako tukasikia vita vimeanza. Sheria za hifadhi za barabara na reli zipo miaka yote. Mbona ni sasa tu ndipo bomoa-bomoa imeanza ili kuondoa waliojenga kwenye hifadhi hizo? Nadhani badala ya kuitwa "Bongoland" tunatakiwa tuitwe "Kurupukaland"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inatokana na utawala uliopo.
 
Back
Top Bottom