unanitaka
JF-Expert Member
- Oct 7, 2014
- 2,178
- 1,045
Habari tulizozipata kutoka Uganda zinasema kuwa tarehe 9 Aprili, 2016 Ujumbe wa Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini- Prof. Sospeter M. Muhongo, Katibu Mkuu- Prof. Ntalikwa, Naibu Katibu Mkuu- Dkt. Juliana Pallagyo, TPDC na TPA, walikuwa nchini Humo kuiwakilisha Tanzania kuhakikisha wanatoa ushawishi kwa Serikali ya Uganda kukubali Bomba la kusafirishia mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda Hadi Bandari ya Tanga litapitia Tanzania, wamefanya kazi nzuri ya kuitetea Tanzania kiasi cha kuwanganganya wapinzani wake kutoka kenya. Timu hii iliyopewa baraka zote na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli ilitumwa Kwa kazi maalum ya kuwashawishi Uganda, imeonyesha msimamo mkali wa kizalendo katika kuhakikisha wanaweka maslahi ya Taifa la Tanzania mbele wakati wa kutoa mada mbele ya wataalam wa Serikali ya Uganda.
Taarifa za kina zinaeleza kuwa Baada ya Tanzania kutoa mada kwa Serikali ya Uganda ikiwemo Kina kirefu Cha Bandari ya Tanga chenye uwezo wa kuchua meli kubwa za mafuta, vivutio na maeneo ambapo Bomba la mafuta ghafi litapita, Serikali ya Uganda ilionyesha wazi kukubaliana na hali halisi na kile kilichowasilishwa na wataalam wa Tanzania. Mtoa taarifa wetu ameendelea kutujuza kuwa ilipofika zamu ya Serikali ya kenya kutoa mada, kulitokea sintofahamu kati yao wenyewe kwa wenyewe na kufikia mahali kutoelewana hasa baada ya kugundua taarifa nyingi zilizowekwa zilikuwa hazina uhalisia kuruhusu mradi kupita Kenya na kufikia hatua ya kugoma kuwasilisha mada zao kwa Serikali ya Uganda. Baada ya majadiliano ya muda mrefu waliamua kutoa taarifa yao kwa kupunguza baadhi ya taarifa ambazo nyingi zilikuwa ni kupotosha ukweli wa mambo, hata hivyo walionyesha wasi wasi mkubwa sana katika baadhi ya maeneo hasa kina cha Maji ya Bandari katika Bandari ya Mombasa na Lamu, Suala la fidia kuwa gumu katika nchi ya Kenya, eneo ambalo Bomba litatakiwa kupita kuna miinuko mingi na kuhitaji vituo vingi vya kuongeza nguvu ya kusukuma mafuta na kubwa lenye utata la Usalama katika Ukanda ambao inasemekana kundi la Alshabab wamekuwa wakiteka watu na kufanya mashambulizi.
Taarifa zinaeleza kuwa Wataalamu wa Uganda walipokuwa wakifanya majumuisho yailiochukua maoni ya Tanzania na Kenya walipendekeza wazi wazi kuwa Bomba lijengwe kutoka Hoima (Uganda) hadi Bandari ya Tanga (Tanzania). Inasemekana uamuzi wa Uganda umezingatia masuala ya msingi ya Usalama na gharama kubwa Kama Mradi utapita Kenya.
Taarifa za Ndani ya kikao hicho zimebainisha kuwa Kenya wamekataa kusaini Minutes za Mkutano kati yao (Kenya) na Uganda (mwenye mafuta ghafi) kwa sababu Kenya haitaki pendekezo la Uganda la kuchagua Bomba lijengwe kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga Port (Tanzania), hii ni kutokana na kuhofia kukosa Mradi huu. Mimi Kama mwandishi na mchambuzi sioni sababu ya hawa wakenya kukataa kwani mradi huu ni wa kibiashara na siyo wa ki-itifaki na wenye Uamuzi ni wa Uganda wenyewe.
Hadi Sasa tunasubiri kupata taarifa rasmi baada ya kikao Cha Mawazi kitakachofanyika Tarehe 11 Aprili, 2016 Jijini Kampala Uganda, na baadae kufuatiwa na kikao Cha Marais wa nchi tatu (Kenya, Uganda na Tanzania). Vikao hivyo viwili (2) vitatumika kutoa taarifa ya uamuzi wa Wataalamu wa Uganda wa chaguo la Hoima (Uganda)-Tanga Port (Tanzania)
Na Mwandishi wetu