Bomani avionya vyombo vya usalama

Bomani avionya vyombo vya usalama

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,483
MWANASHERIA Mkuu mstaafu, Jaji Mark Bomani, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kufuata misingi ya sheria katika utendaji wao wa kazi.

Bomani amevitaka pia kuzingatia sheria katika matumizi ya silaha kwenye matukio mbalimbali wanayokabiliana nayo.

Kauli hiyo aliitoa wakati wa Kongamano la Maadili ya Waandishi wa Habari lililofanyika jijini Dar es Salaam jana likiwa na kaulimbiu ya ‘Wajibu wa Vyombo vya Habari Kupambana na Kauli za Chuki na Itikadi Kali.’

Alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya vyombo vya dola kuwapiga watu bila kufuata sheria ambazo zinakataza kufanya hivyo, lakini mambo hayo yanatokana na uelewa mdogo.

Aliongeza kuwa hata maandamano na mikutano yoyote inapozuiwa pia ni lazima vigezo na sheria zifuatwe ili kila mmoja au kinachofanyika kimezingatia sheria na si uonevu au upendeleo.

“Sheria inaweka wazi ni maeneo gani vyombo vya dola vinaweza kutumia silaha za moto, lakini siku hizi naona mambo yanakwenda ndivyo sivyo,” alisema.

Bomani aliitaja Sheria inayohusu kumiliki au kubeba silaha ambayo ni Sura Na. 223 ya sheria za nchi, kifungu cha 4 cha sheria hiyo kinasema: “Ni kinyume cha sheria kwa mtu yeyote kumiliki au kubeba silaha ya moto bila ya kuwa na kibali cha kufanya hivyo,” alifafanua.

Alionya vyombo vya dola kuwa havipo juu ya sheria katika utendaji wao wa kazi, hivyo ni vema wakazingatia sheria za nchi.

Jaji Bomani aliongeza kuwa tasnia ya habari ina jukumu kubwa la kuandika habari zitakazokuwa chachu katika kudumisha umoja na mshikamano wa nchi.

Alisema bila ya tasnia hiyo kupiga vita mambo yote ambayo madhumini au matokeo mi kuvuruga amani ya nchi au kuchochea chuki na mfarakano katika jamii kama ilivyojitokeza siku za karibuni taifa litaangamia.

Bomani alisema kila mmoja anapaswa kujua kuwa amani ikivurugwa au kuvunjika itakuwa ni vigumu kuirejesha kwasababu madhara yake ni makubwa kwa wananchi.

Alisema vyombo vya habari vijiepushe na itikadi za vyama pamoja na kuzingatia maadili katika utendaji kazi wao wa kila siku.

“Wanahabari shurti wawe wenye ari ya kujipatia elimu na wanaopenda kujiendeleza kielimu, na ikiwezekana, wajikite katika mambo fulani ili waweze kuelewa na kutafsiri matukio mbalimbali ndani na nje ya nchi,” alisema.

Bomani alisema vyombo vya habari viwasogeze Watanzania wawe wamoja, washiriki shughuli za maendeleo kwa pamoja bila kujali dini au itikadi zao za kisiasa.

“Mwanahabari anapozungumzia matumizi ya nguvu kupita kiasi yakifanywa na vyombo vya dola, kigezo chake kinakuwa ni nini? Hili ninalozungumza limekuwa likitokea mara nyingi sana hapa nchini katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni,” alisema.

Mwandishi mwandamizi Makwaiya wa Kuhenga alisema magazeti ya zamani yalikuwa na mchango mkubwa wa kudumisha amani ya nchi na umoja wa kitaifa.

“Sasa hali ikoje katika zama hizi za gulio? Nimegusia kidogo mambo ya leo ya viongozi wa kisiasa kujialika kwenye hafla za kidini. Wapo wengi hao! Kuna mwiko gani unaowakataza? Gulio lina mwiko?” alihoji Wakuhenga.

Wakuhenga alisema pamoja na gulio la wanahabari ni lazima wajue wana wajibu mkubwa kuhakikisha nchi haiendi kubaya.

Naye Ndimara Tegambwage, alisema serikali imeendelea kulitambua Baraza la Habari (MCT), na haki zake; ilitumie kwa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma (mfano NACTE).

Ndimara alisema Sheria juu ya vyombo vya habari itamke waziwazi kuwa taarifa za serikali zitapatikana bila kikwazo, ilinde waandishi na vyombo vyao vya habari; na ifute vipengele vya kubamiza au kuondoa uhuru wa habari vilivyomo katika sheria nyingine
 
bora hawa wazee ambao wamebaki waweze toa muongozo kwenye hi serikali kwa sababu ni hatari sasa.
 
Wazee kama hawa ndo tunu ya taifa. Mwingine anajisemea tu Piga tu..wapigeni bila kutafakari athari ya hicho anachokisema. Hajui kuwa hakuna dola iliyowahi kuwashinda wananchi kama wakiamua. Hajui piga tu inaweza kumrudia yeye pale nguvu anazozitegemea zitakapokuwa zimeshindwa, mabomu yameisha, risasi zimeisha mwisho anakiona kikundi kikimfuata wakati huo hana mlinzi. Chuki na mapigano hayana mwenyewe. Yoyote aweza kushinda hivyo si vema kujidhania kuwa wewe utakuwa salama. Vinginevyo MWAFRIKA NA MPENDA AFRIKA GADDAF asingeshindwa ila hakusoma nyakati na hakujua kuwa kuna siku anaweza kufikiwa kirahisi. Ni vema kutafakari maneno yetu kabla ya kuyatoa na pili kujiridhisha kama hayakiuki sheria. Mwenye busara hukaa kimya pale ambapo hana uhakika sana na kile anachotaka kusema.
 
Inafariji kuona kwamba kuna watu wenye heshima zao wanaiangalia tanzania bila jicho la itikadi. Tunaomba na wengine, haswa waliowahi kuwa viongozi wa kitaifa, watoe busara zao hadharani kwa kumuunga mkono Jaji Bomani na pia kuendelea kuonya pale haki inapopindishwa bila kujali anayepindisha.
 
Wakuu wa vyombo hivyo wanateuliwa na rais kwa hiyo siyo rahisi kujiepusha na itikadi ya vyama.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Kwanza vyombo vya usalama vyenyewe vimebweteka sana katka uweledi. hadi sasa wanang'ang'ania ushahidi wa Mbowe kuhusu bomu la Arusha badala ya wao wenyewe kufanya uchunguzi na kuja na kitu cha kuweza kuwasifia. Hawawezi wanakalia mambo mengine kabisa.

Hivi ma-expert wa uchunguzi kutoka China wameishia wapi?
 
wazee wenye hekima nchi hii wabebaki wachache sana; hongera mzee wetu Bomani kusema ukweli, lakini kwa sababu wameshaweka pamba masikioni na madaraka ni matamu, sidhani kama watakusikia.
 
Asante mzee Bomani,nadhani ili ni somo hata kwa wale wazee wanasheria wasiojua sheria!kama ulivyosisitiza,uelewa mdogo unachangia jambo ili!nadhani ujumbe umewafikia,na jamii imejua ni jinsi gani waliyo wepesi
 
Back
Top Bottom