Boko Haram wamewaua wanajeshi 5 wa Cameroon

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Wanamgambo wa Boko Haram wamewaua wanajeshi watano wa Cameroon na raia mmoja kwenye shambulizi kaskazini mwa nchi, wizara ya ulinzi ya Cameroon imesema Jumanne.

Shambulizi hilo lilifanyika Jumatatu usiku karibu na mpaka na Nigeria, ambako mashambulizi ya kundi hilo lenye itikadi kali ya kiislamu yameongezeka.

Taarifa ya wizara ya ulinzi imesema “kundi la magaidi wenye silaha nzito wa tawi la Boko Haram, wakiwa ndani ya magari kadhaa walishambulia kituo cha jeshi karibu na Kijiji cha Zigue, kilomita chache kutoka mpaka na Nigeria.

Taarifa zimeongeza kuwa baadhi ya wanamgambo waliuwawa, bila kutoa maelezo zaidi. Wapiganaji wa Boko Haram na kundi jingine lililojitenga, la Islamic State in West Africa (ISWAP), wamekua wakiendesha mashambulizi mabaya dhidi ya maafisa wa usalama na raia kaskazini mwa Cameroon, pamoja na kwenye nchi jirani za Nigeria, Niger na Chad
 
Back
Top Bottom