Bohari ya Dawa (MSD) yashusha shehena ya dawa ya kuacha pombe

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,112
Reaction score
7,158


Bohari ya Dawa (MSD) imeingiza nchini shehena ya kwanza ya Naltrexone, dawa inayotumika katika matibabu ya uraibu wa pombe, hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa watu wenye tatizo hilo.

Uingizaji wa dawa hiyo umefanyika kupitia ushirikiano kati ya MSD na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, katika mpango wa kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya zinazotumika kudhibiti uraibu wa pombe nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya MSD iliyotolewa leo, Septemba 23, 2026, na Meneja Mawasiliano wa taasisi hiyo, Etty Kusiluka, Naltrexone itapatikana na kuratibiwa na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe.

Amesema MSD itaendelea na ununuzi wa dawa hiyo kwa ajili ya taasisi hiyo ili kuhakikisha inapatikana kwa wanaohitaji huduma.


Soma Pia: Dawa kuacha pombe kuwasili Tanzania

Naltrexone ni miongoni mwa dawa zinazotumika katika matibabu ya uraibu wa pombe na inaweza kusaidia kupunguza hamu ya kunywa kwa baadhi ya wagonjwa inapotoa pamoja na ushauri nasaha na huduma nyingine za kitabibu.
 
Pombe ni UBATILI ni jambo jema sana..... huenda ikasaidia kupunguza waraibu...
 
TBL
SBL
TCC
Hao ndio vinara kulipa kodi.
Nyie walokole wenye utitiri wa makanisa kila kona ebu tuonyeshe mchango wenu katika kuongeza pato la taifa
TUBUNI na kuiamini injili, ya MUNGU mpeni MUNGU na kaisari mpeni vyake
 
Dawa ni mtu mwenyewe akiamua izo dawa nikama external factors tuu mtu akishindwa kwa izo dawa anaweza kuwa sugu kabisa wa pombe
 
Naona wanataka kushusha mapato ya Kodi ya vileo

Sina hakika kama TBL watafurahia hili
 
Baada ya mwili kuona taa ya check engine inawaka na kuzima hakuna alie niambie niache pombe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…