BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (HESLB) imesema haitoongeza kiwango cha mikopo hata wanafunzi wakiandamana kwenye ofisi zake. Msemaji wa bodi hiyo, Veneranda Malima, alisema hawawezi kuongeza viwango vya mikopo kwa sababu ada iliyopandishwa na vyuo vikuu hawaitambui Alisema bodi hiyo inatambua viwango vya ada ilivyopewa na serikali mwaka 2008/2009 hivyo ongezeko lolote la ada litakalotokea litapaswa adaiwe mwanafunzi na si bodi.
Alibainisha kuwa serikali ilitoa maelekezo hayo kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na vyuo vyote lakini vyuo vimekaidi agizo hilo na vimeamua kuongeza ada mara dufu.
Aliongeza kuwa vyuo hivyo sasa vinawashawishi wanafunzi wao kwenda kwenye bodi ya mikopo kudai nyongeza ya ada.