Hakuna haja ya kulalama tulishajitambua tangu mwaka jana kwenye motto ya wale wagombea. Ya UKAWA ilisema elimu mpaka chuo kikuu ni bure na ya CCM ilisema elimu mpaka darasa la saba ni bure.
Na nikiangalia tulimchagua Rais wetu mpendwa kwa kura nyingi za NDIOOOO kwa sababu motto yake tuliielewa na nimpongeze Rais wetu kwa kusimamia yale aliyoahidi.
Kwani tumeshaona shule za msingi elimu ni bure, madawati yametengenezwa ya kutosha. Hili la mikopo kwa wote hakusimamia hilo jamani tusiichoshe serikali yetu hakuna namna.