BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya awamu ya pili waliopangiwa mikopo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya wanafunzi 5168 wa awamu ya pili wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 19.9 bilioni.

Taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari na Mkurugenz Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru inasema hadi leo (Jumanne, Novemba 17, 2020), jumla ya wanafunzi 52,473 wa mwaka wa kwanza wamepangiwa mkopo yenye thamani ya TZS 170.02 bilioni.

Basru alisema Novemba 11, mwaka huu HESLB ilitangaza orodha ya Awamu ya Kwanza waliopangwa mikopo iliyokuwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 47,305 ambao walipangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 150.03 bilioni.

“Wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni kutembelea katika akaunti zao za SIPA walizotumia kuomba mkopo na watapata taarifa za kina kuhusu mkopo.” amesema Abdul-Razaq Badru leo (Jumanne, Novemba 17, 2020) Jijini Dar es Salaam.

Kuhusu wanafunzi waombaji ambao maombi yao yalikua na upungufu, Badru amesema HESLB imetoa muda wa siku tano (05) kuanzia kesho (Jumatano, Novemba 18, 2020) kurekebisha taarifa zao na kuzituma kwa njia ya mtandao.

“Tuna wanafunzi wachache ambao maombi yao yana upungufu ambao kuanzia kesho wataweza kuingia katika akaunti zao za SIPA walizotumia kuomba mkopo na kurekebisha kwa kuweka nyaraka sahihi na tutazifanyia uchambuzi na wenye sifa watapangiwa mikopo mapema iwezekanavyo,” amesema Badru.

katika mwaka 2020/2021, Serikali imetenga kiasi cha TZS 464 Bilioni kwa ajili ya kugharamia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu 145,000 wakiwemo wanafunzi 54,000 wa mwaka wa kwanza na wanafunzi 91,000 wanaoendelea na masomo.
 
Duuuh hatari sana haya mambo ila mungu awajalie wote wenye uhitaji wapate maana hakuna namna zaidi ya kuja kusoma ili utimize malengo tu basi.
 
haijulikani kwasababu kila mtu na akaunt yake wangetoa list ingekua unajua kwaiyo wamebak kama wanafunzi minimum 2000 iv sijui ndo wale walio kosea au nakwa wale ambao not yet finalised
 
Ndio Mkuu nipo hapa nafuatilia until now accounts hazijabadilika
Endelea kusubiri bila kuchoka mkuu, wengi ninaowajua, zaidi ya watu 15,wakikosa batch ya Mwanza mpaka Sasa account zao hazijabadilika pia.

Wakati batch ya kwanza inatoka, Kuna dogo hakuna mabadiliko yoyote kwenye account yake, Ila baada ya siku mbili ikasoma kapata mkopo. Najua unaelewa namaanisha nini kusema hivi.
 
Endelea kusubiri bila kuchoka mkuu, wengi ninaowajua, zaidi ya watu 15,wakikosa batch ya Mwanza mpaka Sasa account zao hazijabadilika pia.

Wakati batch ya kwanza inatoka, Kuna dogo hakuna mabadiliko yoyote kwenye account yake, Ila baada ya siku mbili ikasoma kapata mkopo. Najua unaelewa namaanisha nini kusema hivi.
apo lazima matumbo joto presha
 
Back
Top Bottom