Bodi ya Mikopo kufanya hivi ni ukata au ni adhabu

True legacy

Member
Dec 16, 2016
76
43
Kuna watu wana furaha tena tele wakiona namna bodi hii ikitoa matamko dhidi ya wadaiwa wa mikopo, tena kwa karaha ni kweli ni haki yao lakini musumeno hukata pande zote leo wao kesho kwako, haki za watu zizingatiwe,siyo kwa namna hii.

kwa wadahiliwa wa mwaka 2006 mpaka 2012 naamini walijaza fomu zenye mashariti sawa, nitaomba wenye hiyo mikataba au kopi zake wasome vinzuri na washee hapa vifungu hivyo, ili tutafute haki.

nakumbuka mdogo wangu mmoja alinipatia huo mkataba na moja ya vipengelee vilivyokuwemo ni pamoja na mkopaji atalipa deni ndani ya miaka 10 baada ya kumaliza chuo, deni hilo halitakuwa na riba , mkopaji atarejesha sawa na kiasi alichokopeshwa na kwa makato ya 8% ya gross salary na mkopaji atalipa mara baada ya kupata ajira.
hii ya kuongeza kiasi cha makato kinatoka wapi?,

ni sheria ipi ya fedha inayomuongezea makato mkopaji baada ya kuingia mkataba?. wenye mikataba hii tusaidiane kuisoma vinzuri, mnyoge mnyoge haki yake mpeni. watu wanadaiwa mamillioni ya shillingi mara mbili na zaidi alichopewa hawana kazi, madeni ya yanaongeza kila kukicha na wanasakwa, hapana hii siyo sahihi, wanasheria na nyie mnadaiwa na hii kazi yenu tafute haki za wezenu ukimya hausaidii. Nchi hii ni yetu sote tusioneane kulinda vyeo.
 
Mimi siku wakinipata Na kunikata lazma niende kukata rufaa maakamani. Spendagi ujinga kwenye swala LA pesq

Mhimili wa Mahakama
Na unaokata hayo Makato upi umejichimbia zaidi Ardhini?

Majaji wenyewe Siku hizi wameufyata kwa Huyu Mwamba, hakuna Safari bila ya kibali Tena uambatanishe na gharama za safar na Nani analipia ndo itakuwa Wewe na kimkopo chako cha loan board?
 
Hebu tuamkeni wafanyakazi kulipinga hili! Tusisubiri kuanza kuonja haya machungu. Hii sio haki kabisa na tukikaa kimya tumeumia
 
Mkataba sharti uheshimiwe na pande zote.Sijajua bodi wanapata wapi jeuri ya kuvunja mkataba waziwazi.Halafu kitu kingine ni hili suala la kuita watu wadaiwa sugu wakati mkataba wa miaka 10 kulipa deni haujaisha.Mtu aliye graduate 2006 kurudi nyuma ndo anapaswa kuitwa mdaiwa sugu maana kwa mujibu wa mkataba kashindwa kulipa deni.
 
Mimi nimemaliza 2005 nimejiunga CHUO 2002 na sijawahi jaza form za mikopo wala Hiyo bodi ya mikopo haikuwepo nalipaje wakati ilikuwa ruzuku ya serikali mi sikuomba mkopo ila nimesomeshwa na full govt sponsorship
 
STUDENT'S LOAN AGREEMENT FORM (MKATABA WA MKOPO KWA MWANAFUNZI)

Naomba niandike kiswahili kama nilivyonakili kutoka katika form ya mkataba-HESLB-SLF 2

1.0 Parties to this agreement
Mkataba huu ni kati ya Bodi ya mkopo ya wanafunzi wa elimu ya juu hapa inajulikana kama "Bodi" (na) ambapo katika mkataba huu atajulikana kama "mwanafunzi"

2.0 Terms and Conditions: (Kanuni na masharti)
2.1 Fomu za mkataba wa mkopo huu zitasainiwa kila mwaka kwa kiasi cha nyongeza au mafungu ya mkopo ambayo kwa pamoja yatakuwa sehemu ya mkataba huu.

****tuendelee kipengele cha 2.12 ambacho ni muhim****

2.12 The loan shall be due for repayment one year after completion of the course of study, not withstanding that the students is at liberty to start repayment the loans at any time during the grace period and shall be repaid fully within a miximum of ten years. (Mkopo utaanza kurejeshwa mwaka mmoja baada ya kuhitimu, lakini mwanafunzi yuko huru kuanza kulipa muda wowote baada ya kuhitimu masomo na mkopo wote ni lazima urejeshwe katika muda usiozidi miaka kumi)
 
STUDENT'S LOAN AGREEMENT FORM (MKATABA WA MKOPO KWA MWANAFUNZI)

Naomba niandike kiswahili kama nilivyonakili kutoka katika form ya mkataba-HESLB-SLF 2

1.0 Parties to this agreement
Mkataba huu ni kati ya Bodi ya mkopo ya wanafunzi wa elimu ya juu hapa inajulikana kama "Bodi" (na) ambapo katika mkataba huu atajulikana kama "mwanafunzi"

2.0 Terms and Conditions: (Kanuni na masharti)
2.1 Fomu za mkataba wa mkopo huu zitasainiwa kila mwaka kwa kiasi cha nyongeza au mafungu ya mkopo ambayo kwa pamoja yatakuwa sehemu ya mkataba huu.

****tuendelee kipengele cha 2.12 ambacho ni muhim****

2.12 The loan shall be due for repayment one year after completion of the course of study, not withstanding that the students is at liberty to start repayment the loans at any time during the grace period and shall be repaid fully within a miximum of ten years. (Mkopo utaanza kurejeshwa mwaka mmoja baada ya kuhitimu, lakini mwanafunzi yuko huru kuanza kulipa muda wowote baada ya kuhitimu masomo na mkopo wote ni lazima urejeshwe katika muda usiozidi mia
SASA Kwanini watu hawahoji huku sheria ipo wazi
 
Pigeni 8% ya mshahara wako then uone kama baada ya miaka 10deni litaisha. Nakumbuka Walio wengi wanadaiwa zaidi ya 12-15mln
 
Mimi walinipa mkopo mwaka wa kwanza. Wa pili wakaninyima et sikufanya updating. Watatu nikapata na sikupata pesa ya research. Mwaka wa pili nilipata maisha magumu sana. Ila nashukuru mwaka wapili ndyo akili ilinikaa sawa nikawa entrepreneur mpaka sasa sina muda wa ajira zao naendelea na biashara zangu nikipata pesa nitawalipa. Miaka 10 bado kufika. Yani sasa ndyo ninamitatu.
 
Mimi wamenikopesha nimeshajiajiri na maisha Yanaenda vizuri Sina ajira sasa wanisake hadi Siku wakichoka watalala tu
 
Back
Top Bottom