Bodi ya ligi yafanya mabadiliko

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
TANZANIA

- Bodi ya ligi Tanzania (TPLB) imebadilisha kanuni kuhusu kufuzu michuano ya kimataifa Shirikisho CAF.

- Awali ilikuwa iwapo bingwa wa ligi kuu akitwaa pia ubingwa wa (FA) mshindi wa (2) FA ndiye anaye iwakilisha nchi kwenye michuano ya Shirikisho CAF.

- Lakini kwa sasa itakuwa iwapo bingwa wa ligi kuu akitwaa ubingwa wa FA pia basi mshindi wa pili (2) wa ligi kuu ndiye ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.yaani Shirikisho (CAF).

- Bodi imedai lengo la kubadili kanuni hiyo ni kuongeza ushindani kwenye ligi kama utaratibu huu ungetumika mwaka jana msimu huu Simba na Yanga wangewakilisha nchi kimataifa, nini maon yako juu ya utaratibu huu?
 
Huo sasa ni utaahira wamewabeba YANGA kwa lipi? Maana kanuni hizi zitaanza msimu huu ulioanza, maana yake mshindi wa pili wa msimu huu ulioanza ndy atawakilisha nchi,au ushatabiri Yanga watakuwa washindi wa pili tena??
Yanga hamna uwezo wa kuchukua ubingwa wala shirikisho labda washindi wa pili msimu uliopita walijaribu kumbeba akakutana na kipigo kitakatu sijui kama umeelewa we nyani
 
TFF wajanja sana.

Kwanini hii kanuni isingetumika msimu uliopita?

mimi naona bora Ibaki vile vile.

Mshindi wa kwanza wa ligi aende ligi ya mabingwa africa. Na Mshindi wa kombe la azam aende shirikisho africa..


Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
TFF wajanja sana.
Kwanini hii kanuni isingetumika msimu uliopita?...
Walichobadili ni kwa mshindi wa pili wa kombe la Azam hatopata nafasi ya kushiriki kombe la shirikisho la Africa na nafasi hiyo itachukuliwa na timu iliyoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu endapo mshindi wa kombe la Azam ndiye huyo huyo aliyebeba kombe la ligi kuu.
 
Hawatendi haki kwa timu ndogo ambazo HAZIPO ligi kuu. Ila Zina uwezo wa kucheza kombe la azam na kushika nafasi ya pili..
Walichobadili ni kwa mshindi wa pili wa kombe la Azam hatopata nafasi ya kushiriki kombe la shirikisho la Africa na nafasi hiyo itachukuliwa na timu iliyoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu endapo mshindi wa kombe la Azam ndiye huyo huyo aliyebeba kombe la ligi kuu.

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Wakitaka ligi kuu iwe na ushindani wabakishe nafasi moja ya uwakilishi kimataifa, msimu uliopita walibadirisha kanuni baada ya kupatikana nafasi nne za uwakilishi lakini juhudi za kuwabeba upotolo pamoja na kuwanyima nafasi kagera bado ilishindakana na yule refa mpaka sasa hukumu yake halijatolewa kwanini tusiamini kuwa tff wanataka kubeba timu kubwa
 
Tanzania ndio nchi iliyo na mambo ya ajabu kwenye kila kitu kwaiyo saizi kombe la azam alina manana.
Kombe la Azam lina maana sana isipokuwa TFF vigeu geu wanatoa maamuzi yanayoamka nayo vichwani mwao hawajaweka sheria maalumu juu ya kufuzu klabu bingwa na shirikisho Africa na ndio maana ilipotokea zinatakiwa timu nne ziwakilishe nchi ndipo wakakurupuka kwa kutoa nafasi kwa Simba ambaye ndiye bingwa, Yanga aliyeshika nafasi ya pili, Azam aliyekuwa mshindi wa kombe la Azam na KMC ambaye alishika nafasi ya nne kwenye ligi.

Hapa unaona kabisa TFF walimuondoa mshindi wa pili wa kombe la Azam kutopata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, ambaye mshindi wa pili alikuwa ni Lipuli na badala yake wakampa nafasi KMC kwa kuangalia msimamo wa ligi kuu. sasa imekuaje msimu uliofuata wampe timu iliyo nafasi ya pili kombe la Azam ndiye awakilishe nchi kimataifa? Maana yake wanajiamulia tu mambo ilimradi.

Haya makombe dizaini ya kombe la Azam, hata nchi za ulaya zipo. Mfano Italy wanaita Copa Italy, uingereza pia ipo FA cup, Spain wanaita copa del rey, ufaransa wanayo coupe de France.

Vyama vya wenzetu wameanzisha michuano na sheria rasmi kabisa inayotumika kuendesha michuano hiyo na namna ya uwakilishi wa washindi katika michuano ya kimataifa. Na katika michuano yote ya timu za ulaya, bingwa wa FA, Copa del rey, Copa Italy wanapata nafasi ya kushiriki michuano ya Europa league lakini timu zinachoingia nazo fainali na kupoteza (mshindi wa pili ) hawaambulii hiyo nafasi ya kwenda kucheza Europa league.
 
Kombe la Azam lina maana sana isipokuwa TFF vigeu geu wanatoa maamuzi yanayoamka nayo vichwani mwao hawajaweka sheria maalumu juu ya kufuzu klabu bingwa na shirikisho Africa na ndio maana ilipotokea zinatakiwa timu nne ziwakilishe nchi ndipo wakakurupuka kwa kutoa nafasi kwa Simba ambaye ndiye bingwa, Yanga aliyeshika nafasi ya pili, Azam aliyekuwa mshindi wa kombe la Azam na KMC ambaye alishika nafasi ya nne kwenye ligi..
Aisee
 
Back
Top Bottom