Bodi ya Ajira vipi?

Master Legendary

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
382
250
WanaJF hii Bodi ya ajira inaanza majukumu yake lini maana yake TUCTA wametutosa wafanyakazi wamegeuka Chama cha siasa,wafanyakazi tunateswa sana na tofauti ya Mishahara serikalini haiwezekani Graduate katika Serikali hiyohiyo alipwe take home Laki 3 af mfagiaji Bandarini Form Four alipwe Laki saba, Mhandisi EWURA, TANAPA, TRA alipwe Milioni 4 halafu wa kwenye Hamashauri alipwe Laki tano.

Hii haikubaliki jamani uchungu wa kusoma ni uleule tunaomba hii bodi ipunguze hii tofauti ya Mishahara iwe ndogo iwe kama Kenya kwamba keki ya taifa ya Mishahara igawanywe kwa tofauti ndogo katika viwango sawa vya Elimu eg Graduate mwenye 1st Degree popote pale serikali Mshahara wake uanzie Mil 1.3 hadi Mil 1.5 hakuna kulipa chini au zaidi ya hapo na Maposhoposho yote yafutwe.

Hii itapunguza sana matabaka yaliyoko sasa ambapo Graduate huyohuyo mwingine ana uwezo wa kujenga nyumba ya Mil 200 kwa miaka mitatu wakati mwingine hata Kiwanja hana uwezo wa kununua,Matokeo yake wananyanyasana tu mtaani huyu anasalimia ndani ya Prado hata Kioo hashushi mwingine analoa jasho na kumaliza soli za viatu kwa kutembea.

Na hii ndiyo chanzo cha kukithiri kwa Rushwa na kujuana kwenye ajira katika baadhi ya Taasisi.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 

Sizinga

JF-Expert Member
Oct 30, 2007
8,466
2,000
Mkuu umeongea la Maana sana. Ndo maana huko Halmashauri kuna Ongezeko Kubwa la PanyaBuku
 

theki

JF-Expert Member
Nov 1, 2013
2,724
1,195
Hii Tanzania yetu kila kitu siasa,hiyo sijui Tucta mwakani utasikia chama cha siasa wapo kwenye mchakato.Haya maswala uliyoyaongea ndio yalitakiwa yapewe kipaumbele kwenye katiba jinsi yakuwalinda waajiriwa sector zote.Tatizo wajumbe nao daah Tunamwachia Mungu tuu.
 

vurumai

Senior Member
Feb 9, 2014
178
0
Umeongea point sana kaka ubarikiwe. Hii yote ni kutokana na kuwa na serikali yenye viongozi waliokosa ubinadamu na kujawa na ubinafsi. Naomba MUNGU tupate kiongozi mzalendo atakayewajali wananchi wote bila kuweka matabaka kama sasa.
 

Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,869
2,000
Umeongea point sana kaka ubarikiwe. Hii yote ni kutokana na kuwa na serikali yenye viongozi waliokosa ubinadamu na kujawa na ubinafsi. Naomba MUNGU tupate kiongozi mzalendo atakayewajali wananchi wote bila kuweka matabaka kama sasa.

Ila chini ya utawala wa ccm,ni ndoto ya mchana.
 

MZAWA JF

JF-Expert Member
Apr 4, 2014
2,492
2,000
Ndg umeongea point sana! mm inaniuma sana kuna kilaza mmoja yuko TRA aliungaunga elimu hadi diploma alafu analipwa laki tisa wakt mm nimefaulu vzr na degree yangu nzuri tu kwn halmashauri nalipwa 460,000/= inauma sana nafikiri tunatakiwa vijana tupiganie hilo kwa nguvu. Mbaya zaidi siku hz hakuna demokrasia ya kuchagua sehemu ya kazi, sekretariet ya ajira wanawafanyia usaili watu alafu wanawapangia maeneo ya kazi.. Huko Hazina,tra,bot nk wanapeana wenyewe kwa vimemo! INAUMA SANA ndo maana mm ctaki kufanyakazi hadi kustaafu, natafta mtaji wa biashara niwah fao la kujitoa kabla mafisadi hawajabadili sheria ya fao la kujitoa nichukue changu nisepe! Namuomba mungu anijalie niandae watoto wangu kutokuajiriwa kabisaaaa! God bless us
 

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,123
2,000
Jamaa umeongea point. Kama kuna wadau wa tume ya ajira au wanaoweza kumfikishia hii info Mama Waziri tutafurahi zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom