Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Hao sikuizi wanajiona wako juu ya sheria, wakati asilimia 90 hawana leseni na wanaendesha kihatari sana. Ningekuwa na uwezo ningewatembezea kichapo mpaka wapagawe!
Nchi hii kila kukicha kunazuka majanga ya Taifa. Hawa Bodaboda ni janga kubwa sana la taifa. Mtu anapewa pikipiki na mjomba wake anajifunzia uwani akijua kuiondoa tu kesho yupo na abiria morogoro road anayumba kila mahali! Hawajui chochote kuhusu usalama barabarani unakuta huyu anakupita kulia mwingine kushoto; ukimgonga tu mmoja basi wanakuja hata wa kutoka kibaha kazi ni kukushambulia na kuondoka na roho yako. Hawajui nani alikuwa na kosa wala nini wao hata ukizozana na mmoja wao akasema tu huyu alikuwa anataka kuniibia bodaboda basi ujue ndio mwisho wako huo. Wameua watu wengi sana wasio na hatia.
Madereva wa Boda Boda ni JANGA LA TAIFA inabidi litafutiwe ufumbuzi.