GE2025 Bodaboda Tarime wahimizwa kudumisha amani

GE2025 Bodaboda Tarime wahimizwa kudumisha amani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Afisa Mnadhimu Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Joswam Kaijanante amewataka maafisa usafirishaji maarufu kama Bodaboda wa wilayani Tarime kudumisha na kuilinda amani ya nchi hii.

Ametoa wito huoOktoba 17, 2025 katika kikao cha Jeshi la Polisi Tarime Rorya na Maafisa usafirishaji kilichofanyika katika ukumbi wa TTC Tarime.

Naye Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Polisi Tarime Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi Jumanne Mkwama amewataka Bodaboda hao kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama kupitia falsafa ya ulinzi shirikishi.

Aidha ,Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mrakibu wa Polisi Khamis Wembo aliweza kuwafundisha Bodaboda elimu ya usalama barabarani

Mwishoni Mkuu wa operesheni Mkoa wa Polisi Tarime Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi Festo Ukulule amewataka maafisa usafirishaji kuwa mabalozi katika jamii na kuungana na Jeshi la Polisi katika kukemea wale wote wanaotaka kuvuruga amani yetu tunayojivunia Watanzania.
1761217330115.png


1761217345593.png
 
Back
Top Bottom