Bodaboda ni kifo

Edsger wybe Dijkstra

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2019
Posts
244
Reaction score
491
Ewe mama/ baba unaempakia mwanao au wanao wawili kwenye boda boda kupelekwa shule acha ufala, upumbavu na uvivu. Boda boda ni kifo!

Ewe mdada wa chuo unaependa urembo wako na uzuri wako, boda boda ni kifo.

Ewe boda boda tafuta kazi ya nyingine ya kufanya achana na huo upumbavu wa boda boda!
 
NI KWELI MKUU ILA NAHISI UNAHUKUMU SANA.CHA MUHIMU ITOLEWE ELIMU ZAIDI YA USALAMA JUU YA USAFIRI HUU PENDWA NA NAMNA YA KUUENDESHA KATIKA MAZINGIRA SALAMA ZAIDI.

Unataka bodaboda waache kazi yao waanze kukaba watu usiku?
 

Boda boda ni hatari hasa kwenye busy road lakini nje ya mji huko kwenye barabara zetu za vumbi ni nzuri kutumia.
 
Mmmh Boda boda jamani, wakifuatiwa na ndugu zetu bajaji Mungu awasaidie sana
 
Uko sahihi kabisa mkuu..

Maana takwimu za vifo kwa mwaka 2020 zinaonesha kuwa wote waliokufa NI KUTOKANA NA BODA BODA.
 
Elimu zaidi inahitajika kutolewa kwa hao bodaboda maana imeajiri wengi na watu wanalea familia zao kupitia bodaboda wakiaacha watafanya shughuli gani? Au warudi kuwa wezi?
 
Uko sahihi kabisa mkuu..

Maana takwimu za vifo kwa mwaka 2020 zinaonesha kuwa wote waliokufa NI KUTOKANA NA BODA BODA.
Wewe ni mtata. Kwa nini ushindwe kutambua kwamba just one soul lost so recklessly ni hasara kubwa kwa taifa letu!???
 
Nilichojifunza bodaboda ni usafiri mzuri pia wengi wamejiajiri na kuingiza kipato.

Lakini ni usafiri hatari zaidi kuliko usafiri mwingineo pale utakapo utumia kinyume na utaratibu.

Mwendo kasi na kutozingtia sheria ndo chanzo kikubwa cha kuonekana bodaboda ni kifo.

Utakuta abiria unamwamuru dereva aendeshe spidi kali huku hujui uwezo wa dereva kucontrol chombo na yeye kuhofia kukosa ujira/pesa anavuta mafuta yote.

Ajali nyingi ni mwendokasi na uzembe.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…