DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Waendesha bodaboda jiji la Mwanza wamefanya maandamano ya amani ikiwa ni maandalizi ya kumpokea mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM DKT. Samia Suluhu Hassan.
Wakizungumza Jijini Mwanza na waandishi wa habari, baadhi ya bodaboda hao akiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Bodaboda Wilaya ya Ilemela Nuru Abdu amesema lengo ni maandalizi ya kumpokea mgombea huyo kwa kusaidia kupunguza faini za usalama barabarani na kuwawekea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao.
Mgombea Urais wa CCM Tanzania, anatarajiwa kuwasili jijini Mwanza Oktoba saba mwaka huu na kufanya mikutano ya hadhara na kuomba kura kwa wananchi waweze kumchagua katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.