unayosema ni kweli, leo nimeshuhudia first hand tukio kama hilo, ilikuwa hivi,
wakati natembea kuelekea kazini asubuhi maeneo ya usalama wa taifa, makumbusho mara mbele yangu nikaona bodaboda kama nne zikiwa na abiria wa 3 kila moja zikija kwa kasi mbele yangu, huku wameshika mawe kuangalia pembeni naona kuna breakdown imebeba bajaji pamoja na gari ya ulinzi, inavyoonekana ndio iliyohusika kwenye ajali na bodaboda, bahati mbaya kwa yule dereva wa gari ambaye alikuwa amekaa nyuma kwenye breakdown kulikuwa na ka foleni na mvua ilikuwa imeanza kunyesha basi walivyomfikia wakaanza kumvuta na kumtoa kwenye breakdown, yule dereva akachomoka akakimbilia usalama wa taifa, bahati nzuri wanajeshi kama 6 hivi wakatoka wale maboda boda wakakimbia kurudi uelekeo wa mwenge. Na wakati wote kwenye msafara wa breakdown kulikuwa na trafick officer, hadi wale wanajeshi wakaanza kumkebehi.
Yaani hii nchi inaanza kuwa lawless, halafu waendesha boda boda wenyewe wanatisha kama ma rebel wa liberia au sierra leone.
ZIPIGWE MARUFUKU!!!