Bodaboda badilikeni, mnaboa

Bodaboda badilikeni, mnaboa

Basi Nenda

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
20,789
Reaction score
47,984
Niende moja kwa moja kwenye mada yangu. Kuna tabia za hawa jamaa wa bodaboda zinaudhi au kutusumbua, nazifafanua hapa chini.

1. Boda wakikuona tu unakuja wanaanza kupiga honi na wakati mwingine anawasha pikipiki anakufuata, sasa mnadhani sisi ni vipofu? Kama ninahitaji pikipiki nitakuita au kukufuata

2. Unapita zako mjini karibu na kituo chao wanakuita "oi brother twende" wengine wanapiga honi kabisa

3. Mtu upo mjini kwenye mizunguko yako boda anatoka huko speed kali sana alafu wanapiga yowe kabisa "uwiiiii" huku wanafanya pikipiki zinatoa sauti fulani ya kushtua sana kama baruti

4. Boda anakukuta unatembea kwa miguu unafanya mazoezi siku hyo anapunguza speed "brother twende" na anaona kabisa una kitambi na jioni hiyo hakuna jua kali

5. Boda anakuona umebeba ki mzigo chako kidogo tu umeenda mjini ana assume hujaja na usafiri na huwaoni kituo chao mpaka wakuite

Bodaboda, kuna wanasiasa waliwateteeni kwamba mtafutiwe ajira rasmi hiyo haina pesa na ni hatari mlikuja juu kwamba mnapata Tsh 1m+ kwa mwezi, basi acheni kutusumbua

NB: Kwa ambao mtakuja kusema ninunue gari, nawajibu in advance kuna vi-baby walker vya watu huwa ninaazima kufanyia mizunguko hivo sio kwamba natembea kila muda kwa mguu

Na lengo hasa la kuandika hapa, kuna mmoja jioni ya leo nimepita mjini kituoni kwao akaniita nilikuwa namsikiliza mtu kwenye simu sikugeuka nikamsikia anatoa kauli kama vile "anajidai hasikii"
 
Kuna michezo yao mingine ya hovyo kweli, wanashikana makalio. niliona hilo zaidi ya mara 3 nikashangaa sana,wenyewe wanasema ni utani. Ilikuwa sabasaba Dodoma wanaopaki upande wa double M.

Kuna kauli zao nyingine ni tata mno nanukuu "boda hali mpaka akaliwe kwa nyuma"
Tabia za boda zinatofautiana na mazingira.
 
Kwaiyo wakikwambia oiii brother twende nawewe unawajibu BASI NENDA kama jina la ID yako hapo..

Dawa yao tembea kikakamavu, vaa sura ya kazi hutaona wanakusogelea.
itabidi nifanye hivo, ki ukweli ninachukia sana hizo tabia
 
Kuna michezo yao mingine ya hovyo kweli, wanashikana makalio. niliona hilo zaidi ya mara 3 nikashangaa sana,wenyewe wanasema ni utani. Ilikuwa sabasaba Dodoma wanaopaki upande wa double M.

Kuna kauli zao nyingine ni tata mno nanukuu "boda hali mpaka akaliwe kwa nyuma"
Tabia za boda zinatofautiana na mazingira.
Aisee ,hawa watu wana shida sehemu au itakuwa kuna kitu wanatumia ni boda wachache utakuta akili zipo vizuri
 
Ukiwa hauna mpango wa kupanda boda hizo honi na kuambiwa twende huwa zinakera. Ila ukiwa una mpango wa kupanda boda halafu kijiweni hamna anayeonesha shobo inakera.
Kikubwa ni kuvumiliana tu.
 
Aisee ,hawa watu wana shida sehemu au itakuwa kuna kitu wanatumia ni boda wachache utakuta akili zipo vizuri
Kwaiyo kukalibisha mteja ofisini kwako nikukosa akili? na vipi kwenye vituo vya daladala na hata stend za mabasi mbona wanafanya hivyo tena mpaka wanakugasi kabisa nao ni bodaboda?
 
Back
Top Bottom